Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Monday, July 22, 2013

Bendera ya CCM yazua tafrani mkutano wa Pinda


       Madiwani wanane wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kati ya madiwani 28 wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea, wamesusia mkutano wa hadhara wa Waziri Mkuu wa Mizengo, Mizengo Pinda,uliofanyika kwenye viwanja vya manispaa hiyo kwa madai ya kusimikwa bendera ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye mkutano huo. Tukio hilo lilitokea Jumamosi kati ya saa 8:30 mchana na 9:00 alasiri wakati madiwani wa halmashauri hiyo wakijiandaa kwenda kwenye mkutano huo wakiwa tayari wamevaa majoha.

     Hata hivyo, madiwani wanane wa Chadema, waliamua kuvua majoho hayo na kuondoka kwenye eneo la Manispaa huku wakidai kuwa katika eneo la mkutano kuna bendera ya CCM kinyume cha utaratibu. Kwa msingi huo, madiwani wanane wa Chadema walikataa kuudhuria mkutano huo.

Source: Mwakanosya G.Bendera ya CCM yazua tafrani mkutano wa Pinda. Retrieved from Ippmedia/Nipashe

No comments: