Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Monday, July 22, 2013

Chadema, CCM, NCCR sasa wavutana kwa Muungano


 
  
      Madiwani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Chama cha NCCR Mageuzi ambao  ni wajumbe wa Baraza la Katiba la Wilaya ya Buhigwe Mkoa wa Kigoma wametofautiana kuhusu mapendekezo ya Rasimu ya kwanza ya  Katiba juu ya muundo wa Muungano kuwa wa Serikali tatu. Tofauti hizo zilitokea jana wakati Diwani wa CCM Kata ya Mnamila, Eveline Muhungu aliposimama kuchangia kuhusu mapendekezo yake juu ya Muungano ambapo alitaka  Muundo wa Serikali kwenye Rasimu ya kwanza ya Katiba ubadilishwe na uwe wa Serikali mbili. Hatua hiyo ilisababisha Diwani wa Chadema, Kata ya Janda Emmanuel Petro kusimama na kusema  kuwa hakuna haja ya kuwa na Serikali mbili na muundo sahili wa Muungano ni kuwa na Serikali tatu.
       Mapendekezo hayo yalipingwa vikali na Diwani wa Kata ya Mzenze, NCCR Mageuzi, Abesta Mkeya ambaye alisema suluhisho la migogoro ya Muungano na kuwaenzi waasisi wa taifa hili ni kuwa na muundo wa Serikali moja, lakini sio tatu wala mbili. Hata hivyo madiwani hao walionyesha wazi kuwa wanachokijadili  kwenye baraza hilo ni misimamo ya vyama vyao na siyo maoni waliyotumwa na wananchi. Maoni ya madiwani  hao yanakuja huku ikiwa tayari  Chama Cha Mapinduzi kimeshatangaza msimamo wake kuwa mapendekezo yao ni kuwa na  muundo wa Serikali mbili, jambo ambalo linapingana na vyama vingine vya siasa ikiwa ni pamoja na Chama cha Wananchi, (CUF) ambao msimamo wao ni muundo wa Serikali tatu.
       Hata hivyo, Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji mstaafu, Joseph Warioba alishaonya wajumbe wa mabaraza hayo kuacha kuwasilisha misimamo ya vyama vyao na badala yake wawasilishe maoni watakayo agizwa na wananchi. Akichangia katika kikao cha baraza hilo, Diwani wa CCM, Viti Maalumu, Evelina Muhungu alisema muundo wa Serikali tatu  utakuwa mzigo kwa wananchi kwa madai kuwa Tanzania bado haina uwezo wa kiuchumi utakaoweza kuhudumia Serikali hizo. “Mimi napendekeza kuwa muundo wa Serikali ya Muungano uwe wa Serikali mbili ili kupunguza mzigo kwa wananchi, kwani kwa hali yoyote ile wao ndiyo watakuwa wawajibikaji wa kuhudumia Serikali hizo,” alisema Muhungu.
      Kwa mujibu wa mapendekezo ya Rasimu ya Kwanza ya Katiba Ibara ya 57 (1) inasema Jamhuri ya Muungano itakuwa na muundo wa shirikisho lenye Serikali tatu ambazo ni (a) Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , (b)Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na (c)Serikali ya Tanzania Bara. Muhungu alisema, “Ifahamike kwamba  muundo wa Serikali tatu ni kuwapa mzigo wananchi, kwani wao ndiyo watatozwa kodi kubwa  kuendesha Serikali hizo.
Source; Mhando A. (July 2013).Chadema, CCM, NCCR sasa wavutana kwa Muungano.Retrieved from Mwananchi

No comments: