Msajili wa Vyama vya Siasa nchini John Tendwa, Akizungumza
katika kipindi cha Hot Mix cha East Africa Television akijibu swali la
mtangazaji wa kipindi Adrian Stepp, amedai kuwa ikibainika kuwa CHADEMA ndio
waliohusika katika kulipua bomu katika mkutano wao wa 15/06/2013 atakifuta.
Alipoulizwa kama
itathibitika kuwa CCM ndio walihusika kulipua bomu hilo amedai kuwa hawezi
kukifuta kwakuwa kwa kufanya hivyo itakuwa ni kufanya mapinduzi ya kalamu.
Kwamba CCM ikifutwa nchi itaparaganyika na kusababisha jeshi kuchukua nchi.
No comments:
Post a Comment