Takriban wanachama 100 wa CCM, wakiwemo waliokuwa wagombea wa CCM (2) kati ya watano waliokuwa wanagombea kata 5 za Arusha mjini na mabalozi 23, wanajiandaa kuhamia CHADEMA baada ya kuchukizwa na unyama wa viongozi wao kupitia polisi, hasa tukio la juzi la kuua watu. Ilikuwa wafanye hilo tukio la kuhama na kuchukua kadi za CHADEMA hadharani leo wakati wa kuaga miili ya wale watoto wawili Viwanja vya ICC, Soweto. Sasa hiyo kitu imevuja na polisi wameendelea kukubali kutumika kwa kutaka kuzuia mkusanyiko wa CHADEMA kuiokoa CCM isiendelee kuaibika zaidi kila siku'.
No comments:
Post a Comment