Breaking news: Polisi waamua kutumia mabomu ya machozi na kupiga raia
Polisi wamelipua mabomu mengi ya
machozi muda huu kuwatanya Wananchi waliokusanyika katika viwanja vya Soweto
ili kwenda kuaga miili ya marehemu wanaosafirishwa leo.
Polisi wameanza kupiga mabomu wakati
wabunge wa CHADEMA walipoanza kuhutubia maelfu kwa maelfu ya wafuasi wake. Hali
ni mbaya sana hata watu wametelekeza magari na pikipiki zao, wabunge wote nao
wamekimbia na mbaya zaidi wanapiga mabomu kila mahali.
Hali ni tete, mabomu yanarindima sana
hali ni tete magari ya mevunjwa gari la Lissu laharibiwa, pikipiki zinavunjwa
na polisi bila sababu.
Wametumia risasi za moto kupiga watu, gari la Tundu Lissu
limevunjwa vioo na jeshi la polisi. Wameumiza watu wengi sana! Hali ni mbaya
sana!
Kufuatana na mgogoro wa serikali na wananchi wa Arusha, barabara
inayounganisha kalolen na polisi central mpaka pale benki kuu arusha pamefungwa
na inaonekana kuna pilikapilika nyingi central zinazoashiria hali si shwari
Huku upande walipo wanaCHADEMA kukirindima mabomu
Kwa kweli hali ni ya hatari na wabunge kadhaa wa Chadema
wameshikiliwa, polisi wanatumia nguvu kubwa kupita kiasi. Baadhi ya vyombo vya
usafiri vilivyoachwa eneo la tukio polisi wanaviharibu kadiri wawezavyo.
Usafiri wa abiria katika barabara ya Moshi-Arusha umesitishwa na hakuna gari
zinazopita latika barabara hiyo. Majeruhi ni wengi na wamepelekwa hospitali.
Mabomu
yalilipuliwa baada ya naibu mwenyekiti kuhitimisha kwa kuwaomba wananchi
waliojikusanya eneo la Soweto waende ktk hospitali ya Mount Meru kwa ajili ya
kwenda kuwaaga marehemu. Awali palitokea mabishano kati ya polisi na viongozi
wa Chadema kuhusu mkusanyiko uliokuwapo hapo. Polisi walisema AICC wamekataa
uwanja wao wa Soweto usitumike ktk shughuli yoyote. Bado vyombo vilivyoachwa
uwanjani na wananchi vinaendelea kuharibiwa na polisi na baadhi ya wananchi
wamejificha ktk fensi na baadhi ya nyumba zilizopo ktk uwanja huu.
Tutawaletea taarifa zaidi.
Poleni Makamanda wote.
No comments:
Post a Comment