i. Sheria ya Kodi ya Mapato, SURA 332.
Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inapendekeza kiwango cha chini
cha kutoza kodi ya mapato ya ajira kwa mfanyakazi (PAY AS YOU EARN) kishuke
kutoka asilimia 14 hadi asilimia 9 ya mshahara wa mfanyakazi.
ii. Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, SURA 147.
Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inapendekeza kufutwa kwa
mapendekezo ya kuongeza kodi kwenye bidhaa za mafuta. Viwango vya sasa vya kodi
na ushuru vibakie E. Kambi Rasmi ya Upinzani inapendekeza kodi mpya kwenye matumizi
ya simu isikubaliwe na ibaki asilimia 12 kama ilivyokuwa zamani.
iii. Sheria ya Ushuru wa Mafuta, SURA 220.
katika sheria hii, Serikali inapendekeza kuongeza kiwango cha
ushuru wa mafuta (fuel levy) kutoka shilingi 200 kwa lita hadi shilingi 263 kwa
kwa lita sawa na ongezeko la shilingi 63 kwa lita. Kambi Rasmi ya Upinzani
Bungeni hakubaliani na pendekezo hili kwani linamadhara makubwa kwa maisha ya
wananchi kwa kuwa linaongeza gharama za maisha kama vile kupanda kwa nauli, bei
za vyakula nk. Hivyo Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inapendekeza kufutwa kabisa
kwa ushuru mpya wa mafuta.
iv. Sheria ya Petroli ( Petroleum Act) SURA 392.
katika sheria hii, Serikali inapendekeza kuanzisha tozo ya
mafuta ya Petroli (petroleum levy) ya shilingi 50 kwa lita ambayo itakusanywa
na Mamlaka ya Mapato (TRA) kwa ajili ya kugharamia mahitaji ya Wakala wa Umeme
Vijijijni (REA). Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inayoongozwa na CHADEMA
inapendekezwa kufutwa kabisa kwa tozo ya mafuta ya petroli ili kuwapunguzia
wananchi ukali wa maisha. Fedha za kwenda REA zipatikane kutoka kwenye
kupunguza misamaha ya kodi.
Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ina mapaendekezo mengine ya
kikodi kama ifuatavyo:
1. Kuondoa ongezeko la Kodi kwenye ngano, ili kupunguza mfumuko
wa bei kwenye bidhaa zitokanazo na ngano kama vile chapatti, mikate, maandazi
nk.
2. Kupunguza misamaha ya kodi hadi asilimia moja ya pato la
Taifa
3. Kupanua wigo wa kodi kwa kuanzisha tozo ya maendeleo ya
michezo (Sports Development Levy) ili kukuza michezo nchini na kugharimia timu
za zinazowakilisha taifa katika michezo ya kimataifa. VAT inayolipwa hivi sasa
kutoka viingilio vya michezo irekebishwe na kuwa ‘sports development levy’.
4. Kuongeza wigo wa kodi kwa kuanzisha tozo ya asilimia moja
(1%) kwa bidhaa zote zinanazoingizwa nchini kutoka nje na tozo ya asilimia
sifuri nukta tano (0.5%) kwa bidhaa zote zinazouzwa nje ya nchi kwa ajili ya
kuboresha miundombinu ya reli hapa nchini. (Railways Development levy on
imports and exports).
5. Kambi ya Upinzani Bungeni inapendekeza kwamba kwa kuwa
utaratibu wa vitambulisho vya taifa umeanza na tayari sehemu fulani ya wananchi
wamepewa vitambulisho na kwa kuwa kwa kupitia mfumo wa TIN na usajili wa magari
kuna watanzania wengi sana wana rekodi za kikodi ni vema sasa sheria ya kodi ya
mapato sura 332 ifanyiwe marekebisho ili kulazimisha kila mwananchi ajaze ‘tax
return’ awe au asiwe na kipato.
6. Kambi ya Upinzani Bungeni inapendekeza kwamba mfumo wa VAT
‘zero rating’ katika jedwali la Kwanza ufutwe na badala yake kwa bidhaa zenye
umuhimu na zilizopo kwenye jedwali la kwanza zipelekwe jedwali la tatu kama
‘special relief’.
7. Kambi ya Upinzani inapendekeza sheria ya Uwekezaji nchini,
TIC, ifanyiwe marekebisho ili Misamaha yote ya kodi iwekwe wazi na kukaguliwa
na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (Transparency and Audit of
Tax exemptions) ili kudhibiti matumizi mabaya ya misamaha ya kodi.
8. Kambi ya Upinzani Bungeni inapendekeza mabadiliko ya Sheria
ya Mawasiliano (EPOCA) ya mwaka 2009 ili kuipa TCRA mamlaka ya kufanya ukaguzi
wa uwekezaji unaofanywa na kampuni za simu hapa nchini kwa lengo la kuzuia
ukwepaji kodi unatokana na kudanganya gharama za uwekezaji.
9. Kambi ya pinzani inapendekeza kuwa tozo mpya kwenye mobile
money transfer litumike iwapo tu tozo kama hili litawekwa kwenye utumaji fedha
kwa njia za benki na njia nyinginezo. Vingenevyo tozo hili ni la kibaguzi na
linapendelea watu wenye uwezo mkubwa dhidi ya wanyonge na hivyo tunatoa wito
kuwa pendekezo hili lisikubaliwe na Bunge.
10. Kambi ya Upinzani Bungeni inapendekeza Bunge
litunge sheria kudhibiti matumizi ya ‘tax havens’ yanayofanywa na kampuni za
uwekezaji na haswa kwenye sekta za Mawasiliano, Madini, Mafuta na Gesi na
nyinginezo. Tanzania ijondoe katika mikataba yote ya kikodi na nchi ambazo ni
‘tax havens’.
No comments:
Post a Comment