Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Saturday, June 22, 2013

Mwigulu Nchemba nusura azichape na Msigwa leo


     Katika tukio lililotokea leo kwenye ukumbi wa St.Gasper Dodoma ambako wabunge wote wapo kwenye semina ya masuala ya ukimwi ambayo inaendelea kumetokea mtifuano na nusura Mwigulu arushe ngumi baada ya Mch.Msigwa kumuita kuwa ni muuaji na hivyo atubu kutokana na damu za watoto wadogo na wakina mama wa Arusha ambao amekatiza maisha yao kwa sababu ya ukatili ambao hauwezi kuendelea kuvumiliwa kamwe.

       Tukio hili lilifuatia baada ya wabunge wa CHADEMA ambao wameanza kurejea Dodoma kwenye Semina hiyo walipokuwa wakiwaambia wabunge wa CCM kuwa Bunge linarejea jumatatu kwani sasa limeshamaliza kukaaa kama kamati ya matumizi , hivyo litarejea kwani wabunge wa CHADEMA watakuwepo hali iliyozidisha hasira za wabunge hao ambao wengi wanaonekana kuwa na hang over za jana ktk kumuaga Sitta.

     Mwigulu alinyanyuka kwenye kiti na kumfuata Msigwa na kumshika kifuani ila wabunge wenzake walienda kuamulia ugomvi huo na hali bado iko tete, semina inaendelea 


Source: Haki Sawa ( June 2013).Mwigulu Nchemba nusura azichape na Msigwa leo. Dodoma. Retrieved from JF

No comments: