UTATANISHI NA UKIMYA KATIKARASIMU YA KATIBA MPYA
MHADHARA WA KUAGA KIGODA CHA
MWALIMU IGODA CHA TAALUMA CHA MWALIMU
NYERERKE
Copyright © Issa Shivji, 2013
Kwa dhati kabisa ningependa
kuwashukuru wanakigodawenzangu, Ng’wanza Kamata, Saida-Yahya-Othman naBashiru
Ally, kwa mazungumzo marefu na mabishanomakali ambayo yamenisaidia kunoa hoja
zangu na kuwazayasiyowazika. Shukrani zangu kwa Walter Rodney Luanda naBashiru
Ally, waliosimamia uchapishaji wa Mhadhara katikamuda mfupi wa siku mbili.
Walter amekuwa bega kwa beganami kwa miaka mitano yote ya uNyagoda wangu.
Amefanyakazi za Kigoda kutokana na imani na msimamo wake na siokiajira
tu.Mwishowe, namshukuru sana, kwa moyo mkunjufu, SaidaYahya-Othman ambaye
amehariri Mhadhara kwa ustadi wamtaalam wa lugha katika masaa ishirini na nne,
tena katikasiku yake ya mapumziko maalum.
Shukrani
1. Naialika kaumu, tutafakari
pamoja,Kuhusu Tunu muhimu, Rasimu ilizotaja,Kati ya Tunu adhimu, mojawapo ni
umoja,Kabla ya Ukombozi, Umoja hauwi Tunu
2. Umoja hauwi Tunu, Kwa taifa
tegemezi,Bali umoja ni Tunu, baada ya ukombozi,Umoja hasa ni mbinu, ya kuunda
mapinduzi,Kabla ya ukombozi, Umoja hauwi Tunu.
3. Uchumi wa nchi yetu, ni uchumi
tegemezi,Na hasa kilimo chetu, siyo cha kimapinduzi,Na pia elimu yetu, ni
chombo cha ubaguzi,Kabla ya ukombozi, Umoja hauwi Tunu.
4. Tanzania nchi yetu,
sasa haina amani,Uhuru na utu wetu, kwa sasa viko rehani,Fikra na mila zetu,
havina tena thamani,Kabla ya ukombozi, Umoja hauwi Tunu,
5. Tutafakari maoni, ya
waliotangulia,Ya Mkwawa na Fanoni, na ya Bibi Titi pia,Umoja walithamini, hoja
waliujengea,Kabla ya ukombozi, Umoja hauwi Tunu.
6. Umoja imara hasa, siyo
uliopo sasa,Huu umoja wa sasa, ni umoja wa mikasaMikasa ya kisiasa, na hila za
wenye pesa,Kabla ya ukombozi, Umoja hauwi Tunu.
7. Umoja si mapatano, baina ya
wala tonge,Umoja si mikutano, ya Jangwani na Kisonge,Umoja ni muungano, wa
tabaka la wanyonge,Kabla ya ukombozi, Umoja hauwi Tunu,
8. Umoja sio ubia, wa
mitaji ya ‘mabwana’,Umoja ni ujamaa, wa watu wasonyonyana,Umoja kwa wenye njaa,
ni nyenzo muhimu sana,Kabla ya ukombozi, Umoja hauwi Tunu.
9. Mhimili wa umoja,
ni dira ya ukombozi,Na adui wa umoja, ni mifumo kandamizi,Na kitanzi cha umoja,
ni sera za kibaguzi,Kabla ya ukombozi, Umoja hauwi Tunu.
10. Tunataka ukombozi,
wa fikra za wanyonge,Tunataka mapinduzi, ya uchumi wa wanyonge,Tunataka
mageuzi, ya Umoja wa wanyongeKabla ya Ukombozi, Umoja hauwi Tunu
UMOJAHAUWI TUNU,KABLA YAUKOMBOZI
– Na Mwalimu Bashiru Ally
5
UTANGULIZI
Niliposimikwa mnamo tarehe 18
Aprili 2008 kuwa Profesa waKigoda cha Taaluma cha Mwalimu Nyerere katika
Umajumui waAfrika, nilitoa mhadhara wa uzinduzi juu ya ‘Umajumui wa
Afrikakatika Fikra za Mwalimu’. Sasa ninakaribia kumaliza muda wanguhapo tarehe
31 Agosti 2013, nimeona si vema nikiondoka bilakutoa mhadhara wa kuaga Kigoda,
wanakigoda na wanachuowenzangu, na wale wote waliokuwa pamoja nasi katika
shughulina mijadala yetu.Tumepanga mhadhara huu mapema kidogo kwa sababu
mbili.Moja, wanafunzi, vijana wa Kigoda, wanaondoka leo kwendakwenye likizo yao.
Ya nini kutoa mhadhara wakati wenyewehawapo?
Pili, mapema mwezi ujao, pamoja na
wasomi wenzangu wawili, tumejipangia kwenda nje ya
nchi kufanya utafiti wa kuandika wasifu (biography) wa
Mwalimu. Kwa hivyo, tukaonatarehe ya leo ni mwafaka.Nimegawa mhadhara huu
katika sehemu kuu nne. Hoja yanguambayo itaeleza udhani (hypothesis) wangu
ulioniongozakuchambua Rasimu ni sehemu ya kwanza. Sehemu ya piliitazumgumzia
dhana ya ‘ukuu wa katiba’ ya shirikisho, yaani
supremacy of the federal
constitution . Kwa kirefu kidogo, ‘moyo’wa
rasimu, yaani muundo na taasisi za muungano, nitazichambuakatika sehemu ya
tatu. Sehemu ya mwisho, ambayo ni ya nne,kabla sijahitimisha mhadhara wangu,
itakuwa juu ya matumainiya wananchi ya Tanzania Mpya.
HOJA
Awali ya yote ningependa kuweka
wazi, mosi, mtazamo wanguutakaoniongoza katika kuchambua Rasimu ya Katiba Mpya;
pili,jambo ambalo ninaliona kuwa ni ‘moyo wa Katiba,’ na tatu udhani(au
hypothesis) wangu.
Mtazamo
Kwanza, kwa wananchi walio wengi,
mchakato wa Katiba mpyaulitoa matumaini ya mwanzo wa kujenga Tanzania Mpya:
nchina jamii zitakazojikita kwenye kujali wavuja jasho, zenye msingiwa haki ya
kijamii (social justice), na sio tu haki ya kisheria (legaljustice).
Tulitarajia kwamba tutatafakari kwa makini hali halisiya watu wetu kwa kipindi
cha miongo mitatu iliyopita ambacho kimetufikisha kwenye hali hii ya
leo. Tulifikiri tutatafuta njia mbadala itakayorudisha imani na
matumaini ya watu katikamifumo yetu ya utawala, siasa na uchumi - mfumo
unaowekamazingira na nafasi pana kwa wananchi walio wengi kuendelezamapambano
yao ya kujikomboa.Kwa dhati kabisa, tungechagua njia mbadala
itakayojengamshikamano palipo na utengano; itakayotuelekeza kwenye usawa,palipo
na mpasuko wa kitabaka, itakayo imarisha Muunganokwa mtazamo wa Umajumui wa
Afrika, palipo na mwelekeowa kurubuni wananchi na kugawanya madaraka. Na
tulitarajiakwamba Katiba Mpya itatangaza rasmi matumaini haya nadhamira hii
bila kupinda dhana au kutafuna maneno.Haya ndio yalikuwa matumaini yetu ya Katiba
Mpya na haya ndioyatakayoniongoza katika kuchambua Rasimu. Ila nitatumia
piautaalaam wangu wa kisheria, nilioupata kutokana na wananchiwenyewe
waliogharimia elimu yangu. Huu ndio mchango wangumdogo kwa jamii iliyonilea.
7
‘Moyo wa Katiba’
Pili, moja kwa moja, niseme kwamba
moyo wa katiba yetu, aumchakato wowote wa kuwa na katiba mpya, ni Muungano.
Hililinatokana na hali halisi ya kihistoria ya katiba zetu. Suala laMuungano
ndilo limesheheni mambo muhimu ya mfumo wakidemokrasia na jamii. Kwa hivyo,
muundo wa Muungano siosuala la idadi ya serikali – moja, mbili, tatu, mbili na
nusu n.k. –bali ni suala la demokrasia.Isitoshe, maoni yaliyokuwa yanakusanywa
yalikuwa juu ya Katibaya Muungano, wala sio katiba ya Tanganyika au katiba ya
Zanzibar.Na Rasimu iliyokabidhibiwa kwetu kwa ajili ya kujadiliwa pia niRasimu
ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa hivyo,uchambuzi wangu, kwa
sehemu kubwa, ni kuhusu Muungano.
Udhani (hypothesis)
Baada ya kuisoma Rasimu kwa kina,
mimi nadhani kwambamasharti mengi ya Rasimu na muundo wake mzima ni matokeo
yamivutano mikali katika Tume. Bahati mbaya hatuna mwenendo wamajadiliano ya
Tume wala taarifa yao rasmi, hata taarifa ya awali.Lakini usomaji wangu wa
awali unaniambia kwamba Rasimu hiini maelewano kwa maana ya compromise, na sio mapatano, aumwafaka, kwa maana ya consensus.
Nijieleze kidogo.Katika maelewano au compromise, pande
zinazokinzana hatimayezinakubali kwa shingo upande ili kutokukwamisha
maamuzi.Pande zote zinapata kidogo na kupoteza kidogo, na kila upandehuwa na
mkakati wake wa kupata zaidi katika duru ya pili.
Kwa hivyo, maelewano kamwe hayawezi
kuwa kwa moyo safi.
Maelewano au compromise, yanazaa uamuzi legelege.Mapatano au consensus,
kwa upande mwingine, ni maafikianoyanayofikiwa baada ya mjadala mrefu, kila
mmoja akilenga kuthibitisha hoja yake na kwa njia
hii kusadikisha wenzake
8
kwamba hoja yake ni sahihi. Baada
ya kufikia uamuzi wa mwafaka, kila mmoja anatoka akiwa ameridhika
na amefurahi. Katika compromise , kila mmoja anatoka amenuna. Ni
wazi kwambahuwezi ukapata mwafaka fastafasta. Lazima utachukua
muda.Ili nieleweke vizuri, nitoe mifano miwili, mmoja mwepesi,mwingine mzito.
Ib. 1(3) ya Rasimu inasema: Hati ya Makubaliano ya Muungano iliyorejewa
katikaIbara ndogo ya (1), ndio msingi mkuu wa Jamhuriya Muungano wa Tanzania na
Katiba hii, kwa kadriitakavyorekebishwa, itakuwa ni mwendelezo waMakubaliano
hayo.Maana ya aya hii ni:Hati ya Makubaliano ya 1964 ni msingi wa Katiba hii
(yaaniRasimu); naKatiba hii ni mwendelezo wa Makubaliano.Ukiangalia kwa jicho
la kisheria, , ukisema Hati ndio msingi, maanayake ni kwamba Hati bado
inaendelea kuwa na nguvu ya kisheriana ndio sheria kuu inayotawala Katiba.
Lakini Hati iliweka serikalimbili; sasa, iweje rasimu inayozungumzia serikali
tatu iwe namsingi ambao ulijengeka kwenye serikali mbili?La pili, Katiba
iliyojikita kwenye serikali tatu haiwezi, kwa vyovyotevile, ikawa mwendelezo wa
Hati.Ni kweli kabisa kwamba Hati ya Makubaliano ya 1964 ni chanzocha Muungano.
Historia hii, kama inavyostahili, imewekwa kwenyeUtangulizi. Lakini masharti ya
katiba yenye nguvu za kisheriahayawezi tena kurudia historia. Ukitaja maneno
kama haya katikamasharti ya Katiba, kimahakama inachukuliwa kwamba nia
yakoilikuwa kuipa Hati nguvu ya kisheria. Nina uhakika kabisa kwambahaikuwa nia
ya Tume kuifufua Hati ya 1964 na kuipa nguvu yakisheria.
9. Pia, ninaamini kabisa kwamba Tume
iliyosheheni wanasheriawazoefu na waliobobea huenda walijua na kuelewa
kabisawalichokuwa wanaandika. Kwa hivyo, haiwezekani kwambawalikosea, au
kuteleza, bali ilikuwa ‘kusalimu amri’ na “kuelewana”ili mambo yaendelee.
Ndivyo tulivyopata ibara legalege ambayokisheria haina kichwa wala
mkia.Inawezekana kabisa kwamba ibara hii isiwe na madhara makubwakwa sababu
majaji wenye busara, kwa hakika, hawatatia maananisharti kama hili. Lakini
unaweza kupata jaji ambaye anaegemeazaidi kwenye ufundi na kuitafsiri ibara hii
kama ilivyo. Madharayake yanaweza kuwa makubwa. Vyovyote vile, ibara kama
hiiisiyoeleweka inashusha hadhi ya Katiba.Mfano wa pili, mzito zaidi, ni kuhusu
mipaka ya madaraka. Eneola utawala wa Serikali ya Shirikisho limetajwa kuwa
‘eneo lote laTanzania Bara ikijumuisha sehemu yake ya bahari na eneo lotela
Zanzibar ikijumuisha sehemu yake ya bahari’ (ib. 2). Lakinieneo la utawala wa
serikali ya Bara na serikali ya Zanzibarhalikutajwa. Bila shaka, katiba za
Washirika zitataja maeneo yaona kuna uwezekano mkubwa kwamba kutakuwa na
msuguanona kutoelewana hasa juu ya mipaka ya bahari katika ‘Zanzibarchannel’.
Katiba ya Zanzibar ya Mwaka wa 1984 iliopo, kwa mfano,inataja mipaka ya
Zanzibar kuwa ni ‘eneo lote la Visiwa vya Ungujana Pemba pamoja na Visiwa
vidogo vilivyoizunguka na bahari yakeambayo kabla ya Muungano wa Tanganyika na
Zanzibar ikiitwaJamhuri ya Watu wa Zanzibar.’ (ib.1)Pande mbili za Muungano
zimewahi kutofautiana kuhusu eneolao la bahari, hasa kwa sababu inadhaniwa
kwamba bahariinayopakana na maeneo ya Tanganyika na Zanzibar ina mafuta
narasilimali nyingine. Waziri Tibaijuka alipopeleka ombi Umoja waMataifa
kuongeza eneo la nchi kwa maili 150, mjumbe mmoja waBaraza la Wawakilishi
aliwasilisha hoja binafsi kumlaumu Waziri
10. wa Zanzibar mhusika kwa kuridhia
ombi hilo.
1.Ukimya wa Rasimu juu ya kueleza kwa
uwazi mipaka ya utawalawa Washirika ni wa ajabu kweli kwa sababu ni wazi
kwambahuwezi kuzungumzia utawala wa mamlaka yoyote yale bilakubaini mipaka
yake. Ukimya huu unaweza kuzaa migogoro.Nitaendelea kutoa mifano mingine katika
uchambuzi wanguunaofuata.
***
Sasa, ni juu yangu kuthibitisha
udhani (au hypothesis) wangu.Kabla sijaanza kufanya hivyo, ningependa kusema
kwa dhatikabisa kwamba Tume hii ya watu 32 wenye kuwakilisha maslahitofauti na
hisia mbalimbali ilifanya kazi katika mazingira na halingumu sana. Hayo
yalitegemewa kutokana na mfumo wenyewe waTume. Wachache wetu tulitahadharisha
mapema lakini viongoziwaliosheheni busara wakaamua vinginevyo.Katika hali hii,
mhadhara wangu usichukuliwe hata kidogo kamakuibeza au kuipuuza kazi
waliyofanya akina Mzee Warioba nawenzake. Sina shaka kwamba wengine wao
walipoteza usingizina hata kuteseka moyoni mwao kuhusu maaumuzi
menginewaliyoyafanya. Kwa hili, wanastahili pole zetu, zaidi ya pongezi.
II.
UKUU WA KATIBA(SUPREMACY OF THE
CONSTITUTION)
Magwiji wa katiba (Wheare 1966,
Singh 1994: A-29 na kuendelea,Nwabueze 2003: juz. 1, sura 3, Seervai 1997: juz.
1, sura v, Shivji 1990/2009) wanaafiki kwamba mfumo
wa shirikisho una angalau sifa ku nne. Hizo ni:
11. Kwamba mwananchi anatawaliwa na
serikali mbili, yaani serikaliya shirikisho na serikali ya mshirika;Kwamba kuna
mgawanyo wa madaraka miongoni mwa serikali;Kwamba Washirika, na katiba na
sheria zao, zina hadhi sawa; naKwamba Katiba ya Shirikisho ni sheria kuu
(supreme law).Je, Rasimu inakidhi sifa hizi? Kwa maoni yangu, kwa kiasi
kikubwa,mfumo wa shirikisho katika Rasimu unakidhi sifa tatu za awali.Kila
mwananchi pande zote mbili atatawaliwa na serikali mbili;Wabara watatawaliwa na
Serikali ya Shirikisho na Serikali ya Bara,Wazanzibari watatawaliwa na Serikali
ya Shirikisho na serikali yaZanzibar. Pia kuna mgawanyo wa madaraka kati ya
serikali tatu.Washirika, yaani Bara na Zanzibar wana hadhi sawa (ib.
61(5)).Sifa inayotatanisha ni ya mwisho, ile inayosema kwamba Katibaya Shirikisho
ni sheria kuu. Nitazichambua ibara zinazohusika.Kabla sijafanya hivyo, nieleze
kwa muhtasari tu maana na dhanaya Ukuu wa Katiba (supremacy of the
constitution).‘Ukuu wa Katiba’ maana yake ni sheria zote, madaraka, majukumuna
mamlaka yanatokana na katiba na katiba ndio chanzo chauhalali wa utawala.
Katiba yenyewe inapata mamlaka yake kutokakwa wananchi katika ujumla wao. Ndiyo
maana, katika msamiatiwa kawaida, tunasema katiba ni sheria mama. Nikitumia
msamiatihuo kwa katiba ya shirikisho, naweza nikasema kwamba katibaya
shirikisho ndio mama na baba wa shirikisho. Katiba na sheriaza Washirika,
ingawa zina mamlaka kamili katika maeneo yao,zinatokana na katiba ya shirikisho
na zinapata uhai wao wa kisheriakwa mujibu wa katiba ya shirikisho. Muhimu
zaidi ni kwamba,kama kuna masharti ya katiba au sheria za Washirika
ambazozinakinzana na katiba au sheria za shirikisho zilizopitishwa kwamujibu wa
katiba ya shirikisho, basi sharti husika inakuwa batilikwa kiasi kile. Kwa
lugha ya kimombo dhana hii inaitwa supremacy
12. clause, yaani kipengele cha ukuu wa katiba
ya shirikisho. Katikakatiba zote za shirikisho duniani kuna kipengele cha
ukuu;Marekani, Australia, India, Canada n.k. Sitazinukuu zote isipokuwambili,
Katiba za Marekani na Australia. Ibara ya VI ya Katiba yaMarekani inasema:
This Constitution, and the Laws of
the United States whichshall be made in Pursuance thereof; and all Treaties
made,or which shall be made, under the Authority of the UnitedStates, shall be
the supreme Law of the Land; and theJudges in every State shall be bound
thereby, any Thingin the Constitution or Laws of any State to the Contrarynotwithstanding.
Na kifungu 109 cha Katiba ya
Australia kinasema hivi:When a law of a State is inconsistent with a law of
theCommonwealth, the latter shall prevail, and the formershall, to the extent
of the inconsistency, be invalid.Kwa kifupi, vipengele vyote viwili
vinasisitiza ukuu wa katibaya shirikisho. Na hii ina mantiki na umuhimu wake
usiopingika.Ukitaka shirikisho liwe imara na liwe na nguvu, basi hakunabudi
Washirika wakubali kutambua na kutii masharti ya katibaya shirikisho. Bila
hivyo, shirikisho litayumba na kutakuwa namigogoro kutokana na vipengele vya
katiba na sheria na vitendovya vyombo vya Washirika kukinzana na kugongana kila
mara.Sasa tuangalie vipengele vya Rasimu vinasemaje kuhusu ukuu waKatiba ya
Shirikisho. Ibara 8(1) inasema:Bila ya kuathiri masharti ya Katiba za Washirika
waMuungano kwa mambo yasiyo ya Muungano, Katibahii itakuwa sheria kuu katika Jamhuri ya
Muungano.(Msisitizo wangu)
13. Hii ina maana kwamba ukuu wa Katiba
ya Shirikisho ni kwamambo saba tu ya muungano yaliyotajwa katika nyongeza;
lichaya mambo hayo, katiba za Washirika ni sheria kuu katika maeneoyao kwa
mambo yote mengine yaliyosalia ( residual powers).Tuendelee. Ibara ya 61(4) inasema:Washirika wa
muungano watatekeleza majukumu yaokwa kuzingatia masharti ya Katiba hii na
Katiba zao.‘Kuzingatia’ sio kubanwa; Kiingereza chake ni ‘to take accountof’,
‘to bear in mind’. Unaweza ukazingatia masharti ya Katibaya Shirikisho na baada
ya hapo ukatenda kinyume chake, lakinihata hivyo utakuwa hujavunja katiba. Hii
inaeleweka zaidiukisoma ibara ndogo inayofuata inayotaka Washirika
kutekelezamajukumu yao kwa masuala yasiyo ya Muungano ‘kwa mujibu’wamasharti
ya katiba zao. ‘Kwa mujibu’ inaleta maana ya kubanwa,huwezi ukakiuka. Kwa
hivyo, masharti ya Katiba ya Shirikisho yanakushawishi ; masharti ya katiba ya
Mshirika yanakushurutisha.Niangalie ibara nyingine ya mwisho ambayo
inakaribia kidogokuuzungumzia ukuu wa Katiba ya Shirikisho. Ibara
109(5)inasema:Bila ya kuathiri kutumika kwa Katiba ya Tanzania Barana Katiba ya
Zanzibar, Katiba hii itakuwa na nguvuya sheria katika Jamhuri ya Muungano kwa
mamboyanayohusu Muungano na endapo sheria nyingineyoyote itakiuka masharti
yaliyomo katika Katiba hii,basi sheria hiyo nyingine, kwa kiasi
kinachokiukaKatiba hii, itakuwa batili.Kuna dhana mbili zilizotumika katika
kipengele hiki: ‘mamboyanayohusu’ (Muungano) na ‘sheria’. Bila shaka
‘mamboyanayohusu Muungano’ ni dhana pana zaidi kuliko ‘mambo ya
14. Muungano’. Mambo ya Muungano ni
yale saba yaliyotajwa katikanyongeza. Mambo yanayohusu Muungano ni hayo saba
pamojana yale yote yaliyozungumziwa katika Katiba ya Shirikisho. Kwamantiki
hiyo hiyo, neno ‘sheria’ haliwezi likawa na maana panazaidi ya sheria inayohusu
mambo ya Muungano yanayotungwa naBunge la Shirikisho kwa mujibu wa ibara 109.
Kwa hivyo, ukuu waKatiba ya Shirikisho unaozungumziwa katika ibara hii ni juu
yashughuli za Muungano tu. Sheria yoyote juu ya mambo yanayohusuMuungano
ikikiuka masharti ya Katiba ya Shirikisho, sheria hiyoni batili. Lakini hii
haihusu katiba na sheria za Washirika.Uchambuzi wangu wa ibara hizi zote
zinazohusu hadhi ya Katiba yaShirikisho katika uhusiano wake na katiba na
sheria za Washirika,unaweza kuhitimishwa kama ifuatavyo:Mosi, hakuna popote
pale katika Rasimu tunapokuta Ukuu waKatiba ya Shirikisho (kwa maana ya supremacy clause) umewekwakwa uwazi na ufasaha, kama ilivyo katika
katiba nyingine zashirikisho nilizozitaja hapo awali.Pili, vipengele
vinavyohusika, ama vinatatanisha au viko kimya, auyote mawili, kuhusu kipengele
cha ukuu.Tatu, hii, kwa maoni yangu, haikutokea kwa makosa au kwakuteleza bali
ni tokeo la maelewano kwa maana ya compromise.Nathubutu kusema
kwamba kama jambo hili lingejadiliwa katikaTume, kungekuwa na mvutano mkali
sana.Mwisho, utatanishi na ukimya huu utapalilia vyanzo vya migogorona mivutano
kati ya mamlaka ya Washirika na Muungano siku zausoni. Athari zake haziwezi
kuepukika. Nitatoa mifano michachemuhimu kadri ninavyoendelea na mhadhara
wangu.
15. A.Tunu, Dira, na Malengo Rasimu ina Tunu, Dira na Malengo
ambayo yamesistizwa sanana Mwenyekiti wa Tume, Mheshimiwa Mzee Warioba.
Yaliyomokatika Tunu, Dira, na Malengo ni udugu, utu, umoja, uzalendo,uwazi,
n.k. na haya yamerudiwarudiwa. Kwa upande wangu,sitasemea hayo. Kwa kadri
nijuavyo, hakuna utawala popote paleduniani, uwe wa kibepari, kijamaa au wa
mabavu, utakaopingahizi Tunu, hata kama hawatekelezi. Lakini jambo
mojawapoambalo liko kwenye utangulizi (ib. 1(2)) na Malengo (ib. 11(1)) nisuala
zima la kujitegemea. Kwa mfano, lengo kuu mojawapo katikaMalengo (ib. 11(1))
linasema na ninanukuu:Lengo Kuu la Katiba hii ni kulinda, kuimarisha
nakudumisha udugu, amani, umoja na utengamano wawananchi wa Jamhuri ya Muungano
kwa kuzingatiaustawi wa wananchi na kujenga Taifa huru lenyedemokrasia, utawala
bora na kujitegemea (msisitizowangu).Nimechagua ibara hii kuizungumzia kwa
sababu kujitegemeakuna nafasi ya kipekee katika historia yetu ya kisiasa.
Mwalimuna Sokoine walikuwa wanasistiza sana umuhimu wa kujitegemeakwa hoja
kwamba tusipojitegemea tutapoteza uhuru wetu.Pamoja na hili, kwetu sisi mtazamo
wa kujitegemea uliendanana ujamaa, ujamaa na kujitegemea. Haya
mawili yalikuwa kamachanda na pete. Sasa ujamaa umefutwa kabisa katika Rasimu
kwahoja kwamba ni itikadi (kana kwamba soko huria, ubinafsishajin.k. sio
itikadi). Kwa vyovyote vile, kidole kimekatwa, tumebakina pete
inahengihengi.Niendelee na mfano wangu. Sura ya Pili inazungumzia
MalengoMuhimu. Malengo yapo katika Katiba ya sasa lakini Malengoyalivyowekwa
katika Rasimu, yanaturudisha nyuma hatua mbili.
16. Kwa nini? Kwanza, katika Rasimu
Malengo ni mwongozo kwahivyo hayabani kisheria. Katika Katiba iliopo Malengo
yana nguvuya sheria (ib. 7(1)) ingawa sio kimahakama (ib 7(2)). Pili
Malengokatika Rasimu ni kwa ajili ya vyombo vya Muungano tu (ang. ib.10(1) na
ib. 238(1) maana ya neno ‘serikali’). Katika katiba iliopoMalengo yalibana
vyombo vyote vya serikali zote mbili. Lakini hata kama yangekuwa yanabana vyombo
vya Washirika,bado yasingekuwa na nguvu ya sheria kwao. Hii ni kwa sababuya
kutokuwa na kipengele cha ukuu. Kwa mfano, inaweza kutokeawashauri waelekezi wa
ndani na nje wakaishauri serikali yaTanganyika kwamba mtazamo wa kujitegemea umepitwa nawakati katika
dunia ya utandawazi. Katika utandawazi kunakutegemeana, sio kujitegemea.
Isitoshe, washauri wataendelea,tukiweka mtazamo wa kujitegemea, ambao
unahusishwa naujamaa, katika katiba, kuna hatari ya kutoweza kuvutia
uwekezajikutoka nje. Kutokana na ushauri huo, katika katiba ya Tanganyika,lengo
kuu linaweza likasomeka hivi:
Lengo kuu la Katiba hii ni kulinda,
kuimarisha na kudumisha udugu,amani, umoja na utengamano wa wananchi wa
Tanganyika kwakuzingatia ustawi wa wananchi na kujenga Tanganyika huru
yenyedemokrasia, utandawazi bora na kutegemeana. Pasipo na shaka, lengo hili
linagongana na lengo kuu la Katiba yaShirikisho. Hata hivyo, ndio lengo
litakalo ongoza vyombo vyaTanganyika kwa sababu Katiba ya Shirikisho haiko juu
ya katibaza Washirika; yaani, inakosa ukuu.Kwa mujibu wa lengo jingine (ib.
11(1)(xi), Serikali inaagizwa‘kuweka utaratibu unaofaa kwa ajili ya kufanikisha
utekelezajiwa haki ya mtu kujipatia elimu …’. Serikali inayomaanishwakatika
kipengele hicho ni Serikali ya Muungano, lakini Serikaliya Muungano haisimamii
elimu kwa sababu elimu sio jambo la
17. Muungano. Na inawezekana kabisa
katiba za Washirika zisiwe nalengo linalofanana na hili. Kwa hivyo, lengo hili
jema halina maana- chombo kinachoagizwa kutekeleza lengo, hakisimamii elimu,na
vyombo vya Washirika vinavyosimamia elimu havibanwi nalengo. Kwa hivyo, jambo
linalopendeza kulisikia ni ganda tupu bilatunda!Kwa hitimisho, nigusie ibara
(10)(2) ambayo inaagiza Serikali yaMuungano kutoa taarifa Bungeni juu ya
utekelezaji wa Malengoangalau mara moja kwa mwaka. Swali ni kwamba malengo
yotemuhimu yanaangukia chini ya mamlaka ya Washirika ambaoni watekelezaji na
hawabanwi na Katiba ya Shirikisho. Katikaukweli huu, hii taarifa
itakayowasilishwa Bungeni itakuwa na ninina itakuwa na maana gani. Kwa kifupi
basi, watekelezaji wakuuwa Malengo hawabanwi na masharti haya; yule ambaye
siomtekelezaji ndiye anayebanwa!
B. Maadili na Miiko ya Uongozi
Mzee Warioba pia amechangamkia
maadili na miiko ya viongoziiliyowekwa katika Rasimu, Sura ya Tatu. Kuna ibara
kama nanepamoja na ibara ndogo chungu nzima juu ya suala la maadili namiiko.
Hizi zinawahusu viongozi wa kuchaguliwa na kuteuliwana ambao watatajwa katika
sheria ya Bunge (ib.14(3)). Bungelinalozungumziwa hapa ni Bunge la Muungano.
Lakini Katiba zaWashirika hazihitaji kufuata au kuwa sambamba na
vipengelehivyo. Wana hiari kuweka au kutokuweka, au kurekebisha aukuchagua vipengele
wanavyotaka kwa sababu maadili na miiko siojambo la muungano na Katiba ya
Shirikisho haiwabani Washirika.Kwa mfano, ib.20(2)(a)(iii) inasema kwamba
kiongozi wa ummahapaswi ‘kujilimbikizia mali kinyume na sheria’. Sasa, sheria
ipiinayozungumziwa hapa? Je kama hakuna sheria ya Washirikainayokataza viongozi
wa umma kujilimbikizia mali, kipengele
18. hiki katika Katiba ya Shirikisho
kitakuwa na uzito gani? Ni wazi,haiwezi ikawa na nguvu yoyote katika maeneo ya
Washirika.Sasa nimulike kwenye haki za binadamu.
C. Haki za Binadamu
Wakereketwa wameshangilia sana haki
za binadamu katikaRasimu na wana sababu nzuri tu kufanya hivyo. Rasimu
imeelezakwa ufasaha haki za binadamu na imeongeza haki nyingineambazo hazimo
katika katiba zilizopo. Kuna mapungufu hapa napale lakini haya yanarekebishika.
Kwa mfano, haki ya wananachikuandamana kuonyesha hisia zao za kulaumu au
kutoridhika najambo fulani haikuwekwa. Pia hakuna haki ya wafanyakazi
kugomakama silaha yao muhimu ya kushinikiza waajiri wao kutekelezamatakwa
yao.Kuna haki mbili muhimu ningependa kuzitaja hapa. Ib. 39(3)inaeleza kwamba
raia wa Jamhuri ya Muungano ‘hatapelekwakatika nchi ya nje yoyote kujibu
mashtaka au kufanyiwa mahojianoya aina yoyote kinyume cha ridhaa yake.’ Hili ni
jambo jema;hususan inapiga marufuku ile inayoitwa ‘rendition’.
3 Pendekezolangu ni kuongeza vipengele viwili kuweka wazi
kwamba nimarufuku raia wa Jamhuri (a) ‘kufungwa au kuwekwa kizuizininchi ya nje
bila ya kufuata sheria ya nchi hiyo; na (b) ‘kuhojiwa na maafisa wa ujasusi au usalama wa
nchi za nje katika eneo la Jamhuri’.
4 Lakini suala ambalo linatatanisha
ni: Hati hii nzuri ya haki zabinadamu ina uzito gani katika maeneo ya
Washirika? Haki zabinadamu sio jambo la Muungano na Katiba ya Shirikisho sio
Katibamama. Je, kama katiba za Washirika zikikosa vipengele vinginevya haki au
kuandikwa tofauti na kuwa na maana na tafsiri tofauti,itakuwaje?
5 Nitoe mfano. Katika kutekeleza haki ya
mwananchikushiriki katika utawala, wagombea huru wanaruhusiwa na
19. Rasimu katika ngazi zote za
utawala. Iwapo katiba za Washirikahazina kipengele kama hicho, basi mgombea huru
atakuwa nahaki ya kugombea uchaguzi katika ngazi ya Bunge la Muunganona Urais
wa Muungano tu, lakini hakuna mgombea huru atakuwana haki kugombea nafasi za
serikali za mitaa au mabunge yaWashirika au urais wa Tanganyika au Zanzibar.
6 Huu ni mfanomwingine wa wananchi kupewa ganda bila
tunda.
Sasa nimefikia sehemu muhimu ya
mhadhara wangu, muundo na
taasisi za muungano.
III. MUUNDO NA TAASISI ZA SHIRIKISHO
Hitimisho langu juu ya muundo wa
muungano ni kwamba, mosi, nitegemezi na, pili, ni dhaifu kwa sababu umejengwa
juu ya msingiwa mchanga wa dhamira na nia nzuri badala ya msingi wa maweya
nguvu za kikatiba zilizowekwa na wananchi wenyewe. Ni kamakwamba suala la
Muungano ni ujirani mwema badala ya umojawa nchi. Nitalifafanua kwa kuchambua
mifano ya maeneo kamamanane hivi.
A.Taasisi Kuu za Kusimamia Muungano
Muungano wa Jamhuri ya Muungano
umeainishwa kama shirikisholenye serikali tatu (ib. 57(1), serikali ya muungano
au shirikisho,serikali ya Tanzania Bara na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
7 Kwa maoni yangu, kwa usahihi zaidi,
hizi zingeitwa dola tatu kwasababu zote zina mihimili mitatu ya dola, yaani,
serikali, bunge namahakama, na mamlaka yao ya utawala. Kwa kukwepa kuainishana
kutaja kwa jina lake dhana inayokusudiwa, ina athari zakeza kutokuelewana na
kuzaa mizozo isiokuwa ya lazima. Mfanomzuri ni yale malumbano yaliyotokea juu
ya Zanzibar kuwa nchiau sio nchi.
8 Inawezekana, kwa busara zake, Tume ilichagua kwa
20 maksudi msamiati uliozoeleka
kuepuka malumbano juu ya maanaya dola na nchi. Tuachane na hili, tuendelee.Kuna
taasisi mbili za mahusiano baina ya serikali hizi tatu -, Tumeya Uhusiano na
Uratibu wa Serikali (ib.102(1) na Mawaziri Wakaazi(ib. 64). Mawaziri Wakaazi
watateuliwa na Washirika na watakuwa na ofisi zao Makao Makuu ya
Serikali ya Muungano. Eneo la Makao
Makuu halijulikani kama litakuwa
katika eneo la Tanganyikaau Zanzibar, au litakuwa linahamahama kati ya
Tanganyika naZanzibar. Vyovyote vile, itabidi serikali ya muungano iombe
serikali za Washirika kuipatia eneo
lake la kujenga ofisi za makao
makuu pamoja na Ikulu ya Rais wa
Muungano.
9 Jukumu mahsusila hao Mawaziri Wakaazi ni kusimamia
uhusiano baina ya serikaliza Washirika, kwa upande mmoja, na kati ya Serikali
ya Muunganona serikali ya Mshirika mhusika, kwa upande mwingine.Tume ya
Uhusiano ina wajumbe sita - makamu wa rais waMuungano, ambaye atakuwa
mwenyekiti, marais wawili waWashirika, Mawaziri wawili Wakaazi na waziri mwenye
dhamanaya mambo ya nje ya Muungano (ib. 102(2). Jukumu na lengo kuula Tume ni
kusimamia na kuweka taratibu na mazingira mazuriya mashauriano, mashirikiano,
na utatuzi wa migogoro baina yaserikali tatu (ib. 103-104). Kwa jumla, Tume ya
Uhusiano siochombo cha utendaji (executive) isipokuwa tu kitahusika katikautatuzi
wa migogoro ambao nitauzungumzia hivi punde. Katikahali halisi ya ulinganisho
wa nguvu za kisiasa, sidhani kwambaTume inaweza kufanya maamuzi yanayobana
pande zote husika, bali, zaidi ni kufikia maelewano,
ambayo pia huwezi kuwa na hakika kwamba yatatekelezwa.
Isitoshe, marais hawa watatuwakitoka vyama tofauti (mbali na wagombea binafsi),
vyenye sera na mielekeo tofauti, hata kufikia
maelewano inaweza kushindikana na kusababisha mivutano na migogro
isiyokuwa na mwisho.Pili, katika usuluhishi na utatuzi wa migogoro, tume
inaweza
21 kufanya uamuzi lakini upande wowote
ambao haukuridhika unahaki ya kukata rufani katika Mahakama ya Juu na uamuzi
waMahakama unakuwa wa mwisho (ib. 104(1)(e) Kwa vyovyote vile,Tume sio ngazi ya
kwanza katika kutatua mgogoro kwa sababupande zote hazilazimishwi kuanzia
mgogoro katika Tume bali zinahiari ya kuanzia ama katika Tume au katika
Mahakama.Kwa kujumuisha, navyoona mie, chombo hiki kikuu cha kiungobaina ya
serikali tatu, kitakuwa na changamoto kama tatu hiviambazo zinaweza zikageuka
kuwa matatizo.Mosi, kuna suala la protokali. Marais kuwa chini ya uenyekitiwa
Makamu wa Rais ina utata. Katika hali ya kawaida, masualaya protokali
yasingekuwa ya kuzingatiwa lakini kwa sababuzisizoeleweka wakuu wa nchi zetu
wanajali sana protokali, labdakudhihirisha ukuu wao.Pili, ambayo ni muhimu
zaidi, hakuna uwiano wa nguvu za kisiasakatika Tume. Kwa vyovyote vile, mwenye
nguvu katika Tumeatakuwa Rais wa Bara - yeye ndiye mtawala wa eneo kubwalenye
wananchi wengi, yeye ndio mwenye rasilimali nyingi,yeye ndiye anatoa mchango
mkubwa wa kuendesha serikali yamuungano, ikiwemo gharama za Tume yenyewe. Kwa
hivyo,tupende tusipende, yeye ndiye atakuwa na sauti nzito. Isitoshe,kutokana
na muundo wa serikali tatu, rais wa Bara hataona aibukujitutumua kinyume na
ilivyo katika serikali mbili wakati raismwenye dhamana ya Bara pia ni rais wa
muungano.Tatu, ikiwa Tume inataka kufanya uamuzi wowote, itakuwa vigumukwa
sababu kila upande unawakilishwa na watu wawili wawili.Nne, katika hali hiyo,
mara nyingi, hasa katika masuala nyeti au mazito ya kitaifa, hata kufikia
maelewano itakuwa vigumu. Kati ya Washirika, unaweza kukuta kila mara
upande dhaifu ambao hojazake zinaelekea kutokubalika, ataomba kikao kiahirishwe
ili arudi
22 kwake kushauriana na wenzake au
kupata maoni ya wananchiwake. Kwa wanasiasa, hii inakuwa ni mbinu ya kuahirisha maafikiano, yaani, delaying tactics.Kwa jumla, na bila kubeza, tathmini yangu ya Tume hii
ni kwambahaina tofauti ya msingi na zile kamati zisizoisha za akina
Shekilangojuu ya kero za Muungano.
B. Bunge la Muungano
Mamlaka ya kutunga sheria juu ya
mambo yote yanayohusuMuungano yamewekwa chini ya Bunge la Muungano. Mambo
‘yoteyasiyo ya Muungano yatakuwa chini ya Bunge la Tanzania Barana Baraza la
Wawakilishi la Zanzibar.’ Bila shaka, mamlaka hayayatatumika kwa mujibu wa
Katiba zao. Kuhusu Bunge, nitagusiamambo matatu yanayotatiza.Moja, ni majimbo
ya uchaguzi wa Bunge la Muungano. Kwamujibu wa ib. 105(3) ‘kila mkoa kwa upande
wa Tanzania Barana wilaya kwa upande wa Zanzibar, itakuwa ni jimbo la
uchaguzi’.Wanahabari wetu waliobobea wamekwishapiga hesabu. Kunamikoa 25 Bara
na wilaya 10 Zanzibar. Kwa kuwa watakuwepowabunge wawili kutoka kila jimbo,
mmoja wa kiume na mwinginewa kike (ib. 104(4), basi tutakuwa na wabunge 70, 50
kutokaBara na 20 kutoka Zanzibar. Pia watakuwepo wabunge watanokuwakilisha
kundi la walemavu ambao watateuliwa na Rais wamuungano. Naona tunaweza kutabiri
kwamba watatu watatokaBara na wawili watatoka Zanzibar ili kuwe na uwiano na
idadiya watu. Jumla tutakuwa na wabunge wa Bara 53, ambayo niasilimia 71, na 22
kutoka Zanzibar, ambayo ni asilimia 29. Kwahivyo, uwiano wa Bara na Zanzibar ni
asilimia 71 kwa asilimia 29,Wabara wakiwa zaidi ya theluthi mbili ya wabunge
wote. Uwianohuu moja kwa moja unapingana na msingi wa kwanza kabisawa
shirikisho. Shirikisho linasimama kwenye usawa wa kisiasa
23 (political equality) wa Washirika bila kujali ukubwa au idadi yawatu wao.
Kwa hivyo, uwakilishi wao hasa katika chombo chakutunga sheria unatakiwa kuwa
sawa.Lakini kuna jambo jingine la kutatanisha. Mikoa na wilaya ningazi za
utawala ambazo haziko chini ya mamlaka ya Muungano.Ugawaji wa maeneo ya utawala
ni mamlaka ya vyombo vyaWashirika, hususan Rais. Kwa mfano, kwa mujibu wa ibara
2Aya Katiba ya Zanzibar ya 1984, Rais ndiye mwenye mamlaka yakugawa maeneo ya
mikoa na wilaya. Sioni sababu ya Zanzibarkukibadilisha kipengele hiki kwa
sababu hawashurutishwi naKatiba ya Shirikisho (Rasimu) kufanya hivyo. Isitoshe,
hakunachochote katika Rasimu kumzuia rais au marais wa Washirikakubadilisha
mipaka na kuongeza idadi ya mikoa au wilaya katikamaeneo yao.Tuchukue mfano.
Kwa sababu zozote zile, rais wa Zanzibaranaamua kugawa Zanzibar katika wilaya
20. Hii itamaanishakwamba kutakuwa na wabunge 40 kutoka Zanzibar, ikifanya
jumlaya wabunge kuwa 95 badala ya 75 katika Bunge. Mabadiliko hayamara moja
yatakuwa yamebadili uwiano kati ya Bara na Zanzibar- asilimia 56 kutoka Bara na
44 kutoka Zanzibar. Na, je, jambohili likitokea katikati ya muda wa Bunge,
kutakuwa na uchaguzimpya? Nimesema rais anaweza kufanya hivyo kwa sababu
zozotezile lakini pia anaweza kufanya hivyo kwa maksudi ili
kujiongezeauwakilishi katika Bunge la Muungano. Kwa lugha ya kimombo,
hiiinaitwa gerrymandering. Vilevile, kwa upande wa Bara, rais
waTanganyika anaweza kuongeza idadi ya mikoa.Pili, Rasimu inaruhusu wagombea
huru na pia uwezo wa wapigakura kumuondoa mbunge wao hata kabla ya kipindi
chake kwasababu zilizotajwa (right of recall) (ib. 124). Mambo haya
yotemawili yanahusika na wabunge wa Bunge la Muungano nasio mabunge ya Washirika.
Kwa hivyo, Washirika wanaweza
24 wakaamua bila kuvunja katiba ya
Shirikisho kwamba katikamaeneo yao hawatakuwa na wagombea huru wala haki
yawapigakura kuondoa wabunge wao. Na hii sio nadharia tu.Viongozi watarajiwa
wamekwishaanza kuonyesha wasiwasi waokuhusu mgombea huru na haki ya wananchi
kuweza kumuondoambunge wao kabla ya muda.Jambo la tatu linawagusa wananchi kwa
karibu sana. Ib. 107(2)(h)inaeleza kwamba miongoni mwa madaraka ya Bunge ni
‘kujadilina kuridhia mikataba yote inayohusisha rasilimali na
maliasilizinazosimamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano.’ Jambo hilini jema
kabisa na la kulifurahia, angalau mikataba hii izungumzweBungeni kwa uwazi
badala ya wananchi kuambiwa kwamba nisiri ya kibiashara. Lakini, rasilimali na
maliasili – ardhi, mafuta,madini, gesiasilia, maji, mapori, n.k. – sio jambo la
Muungano.Rasilimali na maliasili ni chini ya mamlaka ya Washirika nawao ndio
watayasimamia. Katika hali hii, Serikali ya Muunganoitaingia kwenye mikataba
ipi na kuhusu rasilimali gani? Ni mfanomwingine wa wananchi kulishwa maneno
matamu yasiyo nauhalisia. Ni haki hewa.Sasa niangalie taasisi nyingine nyeti na
muhimu, jeshi la polisi.
C. Jeshi la Polisi
Nianze kwa kuweka wazi kwamba
polisi haimo miongoni mwa yalemambo saba ya Muungano kinyume na katiba ilioko
(Nyongezaya Kwanza, jambo la nne). Pamoja na kutamka kwamba Jeshi laPolisi ni
chini ya mamlaka ya Muungano na jeshi ndilo litakuwana jukumu la ‘ulinzi wa
watu na mali zao’ (ib. 227(1), Rasimuinasema kwamba ‘Washirika … wanaweza
kuanzisha vikosi vyaulinzi vitakavyosimamia masuala ya usalama wa watu na
malikatika maeneo yao.’ (ib. 232(1) Bila kutafuna maneno, ibara hiini wazi na
maana yake ni kwamba Washirika wanaweza wakawa
25 na majeshi yao ya polisi, ilimradi
yasiitwe polisi kwa jina, ingawayana majukumu na muundo unaofanana kabisa na
ule wa Jeshi laPolisi. Kwa hivyo, utakuta kuna majeshi matatu ambayo
majukumuyao ni yale yale. Katika hali hii huwezi kuepuka migongano nakama
tujuavyo vikundi vyenye silaha vikigongana, unaoathirika niusalama wa wananchi.
Bila shaka, waandishi wa Rasimu walionauwezekano huo; usuluhishi wao ni
kuongeza kipengele kinginekinachosema, ‘Vikosi vya ulinzi vya Washirika wa
Muungano,vitatekeleza majukumu yao kwa ushirikiano na Jeshi la Polisi laJamhuri
ya Muungano ili kuepusha mgongano wa mamlaka …‘ (ib. 232(2). Tuwe wa kweli,
jambo muhimu kama uwezekanowa migongano kati ya majeshi unaweza kweli kuliachia
nia nadhamira njema ya kushirikiana? Tena kikatiba? Busara inahitajikwamba
angalau kikatiba unaweka mazingira na masharti yakuepuka migongano, sio kuweka
mazingira ya migongano na halafuukasema washirikiane ili kuepuka migongano.
Haileti maana walahaina mantiki. Ndio maana huwezi ukawa na vikosi vya
usalamazaidi ya kimoja vyenye majukumu yale yale wakifanya kazi katikamaeneo yale
yale. Kama busara ingetumika, basi ‘polisi’ ingewekakatika orodha ya mambo ya
muungano na lingeundwa jeshi mojatu la polisi la Jamhuri ya Muungano. Na
ingekuwa marufuku mtu,taasisi au serikali nyingine yoyote kuunda vikosi vya
usalamahuru nje ya jeshi la Jamhuri.Kwani wajumbe wazito wa Tume hawakuwa na
busara auhawakuliona hili? La hasha, wajumbe wengine katika Tumewana busara
tele, utaalam wa mambo ya kikatiba na tena wanauzoefu wa kuendesha nchi kwa
zaidi ya robo karne. Kwa hivyo,ninashawishika kueleza vipengele hivyo kama
maelewano, tenazaidi ya maelewano, kuhalalisha kinachoitwa ‘idara maalum’katika
Katiba ya Zanzibar ilioko (Sura ya Kumi). Idara maalumya Zanzibar inajumuisha
Jeshi La Kujenga Uchumi (JKU), KikosiMaalum cha Kuzuia Magendo (KMKM) na Chuo
cha Mafunzo (cha 26 wahalifu) (ib. 121(2). Rais wa
Zanzibar ana mamlaka kamili juu yaidara maalum na tena kikatiba anaitwa
‘Kamanda Mkuu wa IdaraMaalum’.Rasimu hii ikipita kuwa sheria kama ilivyo, mimi
sitashangaaikiwa Zanzibar itarekebisha Katiba yao katika ibara ya 26(1)ambayo
ilivyo inasomeka: ‘Kutakuwa na Rais wa Zanzibar ambayeatakuwa Mkuu wa Nchi ya
Zanzibar, Kiongozi Mkuu wa Serikaliya Mapinduzi na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi.’ Baada yamarekebisho, ibara inaweza ikasomeka: ‘Kutakuwa na Rais
waZanzibar ambaye atakuwa Mkuu wa nchi ya Zanzibar, KiongoziMkuu wa Serikali ya
Mapinduzi, Mwenyekiti wa Baraza laMapinduzi na Kamanda Mkuu wa Vikosi vya
Ulinzi na Usalama.’Na hii haitakuwa kinyume cha Katiba ya Shirikisho kwa
sababu,moja, polisi sio jambo la muungano na, pili, Katiba ya Shirikishoyenyewe
inaruhusu.Vilevile Tanzania Bara wanaweza likaufuata nyanyo na kuwa navikosi
vyao vya usalama na ulinzi. Hali halisi ilivyo, vikosi hivyovya Bara au
Tanganyika vitakuwa na uongozi wa kitaalam, silahaza kisasa na nguvu zaidi
kuliko Jeshi la Polisi la Jamhuri ambalolitajikuta halina fedha za
kujiendesha.Nitatoa mfano mmoja wa kuonyesha migongano hatarishiinayoweza
kutokea katika hali halisi. Ingawa mfano huu ni wakudhania, sio kama
hauwezekani kutokea. Rais wa Jamhuri kwatathmini yake anaona kuna hali ya
hatari katika eneo mojawapo laBara ambao inahitaji kudhibitiwa mara moja. Kwa
mujibu wa ib.81, baada ya kushauriana na Baraza la Ulinzi na Usalama wa
Taifa,kikao ambacho hakikuhudhuriwa na Rais wa Bara, anatangazahali ya hatari
na kupeleka kikosi cha FFU kuidhibiti. Utangazwajiwa hali ya hatari sio jambo
la muungano (kinyume na Katibailioko ambayo inasema mamlaka juu ya hali ya
hatari ni jambola Muungano, Nyongeza ya Kwanza). Rais wa Bara pia anapeleka
27.kikosi chake cha usalama kudhibiti
hali hii na kumtaka Rais waJamhuri aondoe mara moja kikosi cha FFU. Rais wa
Jamhurianakaidi ushauri huu. Kwa vyovyote vile, kutatokea mgongano kwasababu katika
hali halisi vikosi vyote viwili vina hadhi sawa, kikosicha Bara kwa mujibu wa
Katiba ya Bara na kikosi cha Jamhuri kwamujibu wa katiba ya muungano. Lolote
linaweza kutokea katikahali kama hii ambalo haliwezi kutabirika.
D. Mahakama ya Rufani na Mahakama
ya Juu
Mahakama katika ngazi ya Jamhuri ni
mbili, Mahakama ya Juuna Mahakama ya Rufani. Mahakama ya Rufani ni
mahakamainayosikiliza rufani kutoka mahakama kuu za Washirika kamatulivyozoea
isipokuwa sio ngazi ya mwisho. Uamuzi wa Mahakamaya Rufani unaweza kupingwa
katika Mahakama ya Juu na uamuziwa Mahakama ya Juu ni wa mwisho.Mahakama ya Juu
ndio mahakama mpya. Pamoja na kusikilizarufani zote kutoka Mahakama ya Rufani,
ina majukumu mahsusiya kusikiliza kwa mara ya kwanza na kuamua mambo matatu ––
kusikiliza na kuamua mara ya kwanza na mwisho mashauriyanayohusu uchaguzi wa
Rais wa Jamhuri;– kusikiliza na kuamua mashauri kuhusu tafsiri ya Katibaya
Shirikisho yanayoletwa na serikali yoyote kati ya tatuzilizopo;– kusikiliza na
kuamua migogoro baina ya serikali hizoinayoletwa na mmoja wao.Pia ina mamlaka
ya kutoa maoni ya kishauri kwa Serikali yaMuungano au Serikali za Washirika.
Rasimu haiko wazi kwambainatoa maoni pale tu inapoombwa au inaweza kufanya
hivyo kwautashi wake yenyewe.Mahakama ya Juu ina Jaji Mkuu na Naibu wake na
majaji saba
28.wengine, jumla ya majaji wakiwa
tisa. Mahakama ya Rufani inaMwenyekiti na majaji wengine 17. Kwa jumla kuna
majaji 27 katikaMahakama za Jamhuri (Sio mzigo mdogo huu!) Kuna
vipengelevinavyosisitiza uwiano wa uwakilishi kutoka pande mbili
zamuungano.Jambo la kutatanisha katika muundo huu ni hili. Mahakamaya Juu na
Mahakama ya Rufani sio miongoni mwa mambo yaMuungano. Pamoja na ukweli huu,
ib.158(3) inaweka mamlaka yakutunga utaratibu na sababu za rufani mikononi mwa
Washirikakwa mujibu wa katiba na sheria zao. Matokeo yake ni kwambaWashirika
wanaweza, wakitaka, kuamua mashauri yapi yaendekatika Mahakama ya Rufani ya
Jamhuri na yapi yazuiliwe.Kwa mfano, Katiba ya Zanzibar ya 1984 iliopo inazuia
kesi zozotezinazohusika na tafsiri ya Katiba ya Zanzibar, na kesi za
Kiislamuzilizoanzia katika Mahakama za Kadhi kusikilizwa na Mahakamaya Rufani,
hii pamoja na kwamba Mahakama ya Rufani ni jambo laMuungano (nyongeza ya pili).
Inawezekena kabisa kwamba baadaya Rasimu kuwa sheria, katiba za Washirika
zikasema kwamba –– kesi zote za tafsiri za katiba zao;– kesi zote za uchaguzi
pamoja na uchaguzi wa marais wao;– kesi zote za uhaini dhidi ya serikali zao;–
kesi zote sinazohusu ukiukwaji wa haki za binadamu aumaadili na miko ya
viongozi; n.k.hazitapelekwa katika Mahakama ya Rufani ya Jamhuri na badalayake
zitasikilizwa na kuamuliwa mara ya mwisho na mahakama zaoza rufani au na jopo
la majaji (ya idadi iliyotajwa) wa MahakamaKuu yao. Isitoshe, wanaweza kwenda
mbali zaidi kwa kusemakwamba matokeo ya uchaguzi wa marais wao hayatapingwa
katikamahakama yoyote ile. Wakifanya hivyo, na hakuna sababu yakisheria kwanini
wasiweze, hadhi ya Mahakama za Jamhuri, pamojana kazi yao, itapungua.
29 Sasa niangaze taasisi nyeti ya
Muungano, na hii sio nyingine,isipokuwa Benki Kuu.
E. Benki Kuu
Uchumi unaotegemea uuzaji na
ununuaji wa bidhaa, fedha namzunguko wa sarafu na uhamishaji wa fedha unakuwa
na nafasiya kipekee. Akiba inawekwa kupitia fedha; uwekezaji unahesabiwakwa
fedha; rasilimali zinathaminiwa kwa fedha. Benki Kuu, angalaukinadharia, ni
taasisi nyeti inayosimamia fedha katika sura zakembalimbali. Majukumu muhimu ya
Benki Kuu ni kutoa na kusimamiasarafu na fedha na mzunguko na uhamishaji wake;
kusimamiaujazi wa fedha (money supply) na amana (bank deposits) katikabenki
zote pamoja na za kibiashara; kutunga na kusimamia sera yakifedha (monetary
policy); kuratibu, kudhibiti na kuhakiki mabenkiya biashara na uwekezaji katika
nchi; kudhibiti mfumuko wa bei,ikiwemo bei ya fedha za kigeni (foreign exchange
rate); na hatimayeni benki ya serikali. Kwa muhtasari basi Benki Kuu ni
mtunzaji,mlinzi, mwangalizi na msimamizi wa fedha za taifa pamoja na akibaya
nchi, ikiwa akiba ya dhahabu au fedha za kigeni.Kwa maoni yangu, katika nchi na
uchumi kama wetu, na ili kuepukamisukosuko ya fedha, hakuna budi Benki Kuu
idhibiti na kuongozasoko, badala ya kufuata soko. Benki Kuu ikifuata soko bila
kuwa namsimamo kwa mujibu wa sera ya fedha, na mtazamo wa maendeleowa nchi,
basi litakuwa kama bendera inayopepea kwa kuelekezwana upepo badala ya
kudhibiti mwelekeo wa upepo. Benki Kuuinatakiwa kuwa kinu kinachonasa upepo ili
kujijengea nguvu, siobendera inayoyumbishwa na upepo.Kwa vyovyote vile, huwezi
kuwa na Benki Kuu zaidi ya moja katikanchi moja hata kama ni nchi ya
shirikisho. Je, Rasimu inasema ninikuhusu Benki Kuu?Kwanza, ‘Sarafu na Benki
Kuu’ ni jambo la Muungano. Hii ni tofauti
30. na Katiba ilioko inayosema kwamba,
‘Mambo yote yanayohusikana sarafu na fedha kwa ajili ya malipo yote halali
(pamoja na noti);mabenki (pamoja na mabenki ya kuweka akiba) na shughuli zote
zamabenki; fedha za kigeni na usimamizi juu ya mambo yanayohusikana fedha za
kigeni’ ni jambo la Muungano (nyongeza ya kwanza,jambo la 12). Hii ni pana
zaidi, inataja sio sarafu tu lakini mamboyote yanayohusika na fedha, ikiwemo,
bila shaka, sera za kifedha.Pamoja na hayo inataja usimamizi wa fedha za
kigeni.Pili, Rasimu katika ib. 218 inasema Washirika wanaweza wakawana benki
zao zitakazokuwa na jukumu la ‘kutunza akaunti ya fedhaza serikali husika,
kusimamia Sera za Kifedha na benki za biasharakatika mamlaka zao.’ Nitarejea
kwenye hii hivi punde.Tatu, majukumu ya Benki Kuu yaliyotajwa katika Rasimu
nimanne –‘(a) kutoa sarafu, kudhibiti na kusimamia mzunguko wa sarafu;(b)
kuandaa na kusimamia Sera na Mipango inayohusiana nasarafu;(c) kudhibiti na
kusimamia masuala ya fedha za kigeni; na(d) kusimamia Benki za Washirika wa
Muungano.’Aya (a) na (b) haina shida kwa sababu zinahusika na sarafuambayo ni
jambo la Muungano. Lakini aya (c) na (d) sio mambo yaMuungano. Kwa kuwa masharti
ya Katiba ya Shirikisho, ambayohayahusiki na mambo ya Muungano, hayawabani
Washirika,inawezekana kabisa Washirika wasitilie maanani aya hizi nawakafanya
shughuli zao kupitia benki zao kama kwamba mashartihaya ya kusimamiwa na Benki
Kuu, na fedha zao za kigenikudhibitiwa na Benki Kuu,
yasingekuwepo.Nitahitimisha na kujumuisha hoja yangu juu ya Benki Kuu
kamaifuatavyo:
31. Moja, Benki Kuu iliyotajwa katika
Rasimu inakosa majukumumuhimu ya Benki Kuu za kawaida.Pili, benki za Washirika
zina uhuru wa kutekeleza mamlaka yoteya benki kuu isipokuwa kutoa na kudhibiti
mzunguko wa sarafu.Kwa hivyo, Benki Kuu ya Shirikisho ni Benki Kuu kwa jina
tu.Ukweli ni kwamba inafanana zaidi na baraza la sarafu, yaani‘currency board’,
kuliko Benki Kuu.
F. Mapato na Gharama za Muungano
Rasimu inataja vyanzo vinne vya
mapato ya Muuungano (ib. 215).Vyanzo hivyo ni –‘(a) ushuru wa bidhaa;(b)
maduhuli yatokanayo na taasisi za Muungano;(c) mchango kutoka kwa Washirika wa
Muungano; na(d) mikopo kutoka ndani na nje ya Jamhuri ya Muungano.’Aya (a) na
(b) zimetajwa katika mambo ya Muungano. Ushuru wa bidhaa una utata kidogo.
Ninafikiri hii haimaanishi ushuru wa bidhaa unaosimamiwa na idara ya
forodha kwa maana ya excise duty . Kwa hivyo labda inamaanisha
ushuru au kodi kama value added tax (VAT), sales tax, produce
cess n.k. Kama hii ndioiliyokusudiwa inahitaji ufafanuzi zaidi. Kwa
vyovyote vile, ushuruwa bidhaa unakusanywa mahali pa uzalishaji, uuzaji na
ulaji. Kunamasuala mawili hapa. Moja, Serikali ya Muungano itahitaji vyombo na maofisi katika sehemu mbalimbali
za maeneo yote mawili ya Muungano kuweza kukusanya ushuru.
Hii yenyewe inaweza ikawana gharama kubwa. Pili, ili kuziba nakisi katika
bajeti yake, Serikaliya Muungano itajikuta kila mara inaongeza ushuru huu,
jamboambalo litawaongezea wananchi mzigo. Pamoja na kulipa ushuruhuu wananchi
watakuwa wanalipa kodi na malipo mengine kwaserikali zao.
32. Inaelekea ushuru wa bidhaa ndio
utakuwa chanzo kikuu chamapato ya Serikali ya Muungano. Maduhuli inamaanisha
karona malipo yanayolipwa serikalini kwa huduma mbalimbali (k.m.pasipoti, hati
ya uraia, visa, n.k.). Kuna idara moja tu katika mamboya Muungano ambayo
inaweza kutoa mapato haya, nayo ni ‘uraiana uhamiaji’. Kuna usajili wa vyama
vya siasa pia lakini hii inawalakin nitaozungumzia baadae.Ninahisi kwamba
mapato makubwa ya Muungano yatatokana namchango wa Washirika. Ni wazi kwamba
Bara ndio itachangiaasilimia kubwa sana. Inanishangaza kwamba Rasimu
haitajikabisa uwiano wa mchango kutoka kwa Washirika. Jambo hili ni laawali
kabisa kuandikwa katika rasimu yoyote ya Shirikisho.Hili la mkopo kutoka nje na
ndani sina hakika nalo. Serikali ambayohaina chanzo chake huru cha mapato au
sekta ya uzalishaji auwalipa kodi wakubwa, hususan mashirika, chini yake,
itakuwa nahali ngumu ya kupata mikopo.Kwa jumla, kuna utatanishi na wasiwasi
kwa upande wa mapatoya Muungano. Kwa upande wa gharama, ni wazi kwambakuendesha
serikali ya muungano kutakuwa na gharama kubwa.Kazi inayofanywa na taasisi moja
au idara moja katika muundouliopo sasa itahitaji taasisi mbili. Kwa mfano,
badala ya kuwa naTume moja ya uchaguzi, sasa kutakuwa na tume mbili, moja
yaMuungano na nyingine ya Bara. (Ukiongeza ya Zanzibar kutakuwana Tume tatu za
uchaguzi.) Na hivyo hivyo kuhusu tume nyingine.Ukiangalia juujuu tu, licha ya
taasisi na idara za kawaida katikaserikali, kuna tume karibu nane na mabaraza
mawili yenyewajumbe wazito ambao bila shaka watakuwa na mishaharaminono na
marupurupu poa. Wananchi wamekwishaanzakuonyesha wasiwasi wao kwa kuwaongezea
mzigo wa kubebaserikali kamili nyingine, zaidi ya hizi mbili tulizonazo.
33. G. Mambo ya Muungano
Kama tulivyoona, kuna mambo saba
katika mambo ya Muungano.Sina mengi ya kusema zaidi ya yale niliyoyasema kwamba
polisi,Mahakama ya Juu, Mahakama ya Rufani na mambo yote yahusuyofedha na fedha
za kigeni yangefaa kuwa mambo ya Muungano.Kuna jambo moja la Muungano ambalo
mimi binafsi sioni mantikiya kuwa kwenye orodha hii - ‘Usajili wa Vyama vya
Siasa’. Ukiwaumeshaweka muundo wa serikali tatu, jambo linalofuata ni juuya chama
cha siasa chenyewe kama kinataka kugombea uchaguzikatika eneo moja tu na sio
lingine. Kwa hivyo, unaweza ukawa nachama cha siasa ambacho kinagombea uchaguzi
katika Zanzibartu, au Bara tu, au katika ngazi ya Muungano tu.
H. Michakato ya Katiba na Mengineyo
Kabla sijaenda kwenye sehemu yangu
ya mwisho na kuhitimishaningependa kutahadharisha kuhusu michakato ya katiba
zawashirika. Siku moja baada ya kuzinduliwa kwa Rasimu tulianzakuwasikia
viongozi wachache, na hata wahariri wa magazeti,wakitoa maoni yao juu ya katiba
ya Tanganyika. Wengine walidirikikusema wala hakuna haja ya kusuburi kupitishwa
kwa Rasimu,maandalizi yaanze mara moja. Wachache, wakiwemo viongoziwaandamizi,
walinukuliwa wakisema wala hakuna haja ya kupatamaoni ya Watanganyika kwa
sababu maoni yamekwishatolewakwa Tume ya Mzee Warioba. Na wakaongeza kwamba
wajumbe waTume ya Warioba kutoka Tanganyika wanaweza kugeuzwa kuwaTume ya
Katiba ya Tanganyika. (Nisingeshangaa kama mwingineangesema wala hakuna haja ya
kuwa na Bunge la Katiba, Wabungekutoka Bara katika Bunge lililopo wanaweza
wakajigeuza kuwaBunge la Katiba.) Kiongozi mmoja wa serikali, kutokana nabusara
na uzoefu wake, amekaririwa akasema kwamba mchakatowenyewe hautachukua muda.
Kwamba ukianza mara baadaya uzinduzi wa Katiba ya Muungano mwezi wa Aprili
unaweza
34. ukamalizika Desemba 2014 na 2015
tukawa na uchaguzi waBunge na Rais wa Tanganyika pamoja na uchaguzi wa Bunge
laMuungano na Rais wa Muungano. Mimi binafsi nilibaki kuduwaakuona jinsi
tulivyomeza mwendo wa fastafasta!Kwanza, sio sahihi hata kidogo kuzumguzia jambo ambalo
hatunauhakika nalo hata kidogo. Kwa nini tuwachukulie wananchi wetu nikama
mbumbumbu ambao watakubali chochote wanachoambiwapamoja na rasimu hii? Mabaraza
hayajaijadili; wananchi wenyewehawajaijadili ingawa wameanza kutoa maoni yao,
pamoja nahisia zao za hofu na wasiwasi. Rasimu ya pili haijatoka;
hatujuimarekebisho yatakayofanyika. Bunge la Katiba halijaketi. Hatujuikwamba
litapitisha rasimu hii bila mabadiliko, tena makubwa.Kura za maoni bado.Pili,
nani ameamua kwamba mchakato wa kupata katiba yaTanganyika, ikiwa muundo wa
serikali tatu utapita, utafananana ule wa katiba ya Muungano? Mchakato wa
kupata katiba yaTanganyika unaweza ukawa tofauti kabisa; unaweza ukawa
borazaidi na wa demokrasia pana zaidi. Inawezakana kabisa kwambamchakato wa
katiba mpya ya Tanganyika usianze na tume bali namkutano wa kitaifa wa kujenga
mwafaka.Tatu, sio sahihi kisiasa au kimantiki, kusema kwamba
wananchiwamekwishatoa maoni yao, kwa hivyo hakuna haja ya kurudi kwao.Walipotembelewa
na Tume ya Warioba maoni waliyokuwa wakitoani juu ya katiba ya Muungano, sio ya
Tanganyika wala Zanzibar.Mfano uliokuwa mbele yao ulikuwa wa katiba ya
Muungano, siowa Tanganyika. Labda zaidi ya asilimia 95 wala hawajui
kwambatuliwahi kuwa na Katiba ya Tanganyika. Ni kweli kabisa, maoniyaliyotolewa
mbele ya Jaji Warioba yalikuwa ni manunguniko namatakwa yao. Sasa Tume inasema
haiwezi kushughulikia mambomengi ya msingi, kama vile rasilimali na madaraka ya
umma, kwahoja kwamba katika muundo waliopendekeza mambo haya ni ya
35. Washirika na sio ya Jamhuri ya
Muungano. Je, nani anajua kwambawananchi wameridhika na hoja hiyo? Je wananchi
wakisemakwamba Rasimu irejeshwe kwenye Tume ili Tume ifanye kazi yaziada
kuutafuta muundo ambao utashughulikia kikatiba mamboyao ya msingi?Ukweli ni
kwamba, kuna mengi hatujui wala hatuwezi kutabiri,kiasi kwamba kuanza mjadala
wa mchakato mwingine wakati huo uliopo wenyewe haujafikia tamati,
ni sawa na kupiga ramli. Na, nne, kuna hatari katika kufanya hivyo.
Ni sawa na kuwapotoshea lengowananchi kwa kuanza mjadala mwingine kabisa na
kuwafanyawaache kujadili hili ambalo liko mbele yao. Sina haja ya kuongezazaidi
juu ya suala ambalo ni wazi.Kabla sijahitimisha nigusie, angalau kwa muhtasari,
matumaini yawananchi ya Tanzania Mpya.
IV. MATUMAINI YA TANZANIA MPYA
Tulipoanza mchakato wa katiba mpya,
wengi wetu, pamoja nawananchi wa hali ya chini, tulikuwa na matumaini
kwambatutajadili na kujiwekea hatma mpya ya nchi yetu yenye matumainina
mwelekeo unaojali walio wengi, hususan wavujajasho. Maonimengi yametolewa na
wananchi, mengi yakiwa manunguniko,matatizo na hali ngumu ya maisha kwa jumla.
Ilikuwa ni juu yawajumbe wa Tume, kwa busara zao, na utaalam wao,
kufanyauchambuzi, kuyaainisha maoni na kutafsiri matakwa ya wananchikatika lugha
na dhana ya katiba.Haraka haraka tunaweza kusema kwamba maoni mengi yawananchi
yalijikita kwenye maeneo matatu ya msingi yanayogusamaisha yao kwa karibu.
Moja, ni demokrasia kwa maana yamadaraka ya umma - demokrasia itakayowawezesha
wananchi
36. vijijini na mitaani kuweza
kujiamulia mambo yao wenyewe. Pili, niudhibiti, usimamizi na uangalizi wa
rasilimali na maliasili za taifaili utajiri huo uweze kuwanufaisha wananchi na
vizazi vijavyo.Tatu, ni mpango, mazingira na taratibu zitakazotoa kipaumbelekwa
huduma za lazima na bora kwa wananchi waliowengi, kama elimu, afya, maji safi, makazi
bora, hifadhi ya uzeeni, na ajira stahiki kwa vijana. Kwa
jumla, ilitegemewa kwamba Tumeingependekeza mfumo na muundo wa siasa, utawala,
uchumi, namazingira utakaokidhi matakwa haya.Kwa mfano, madaraka ya umma, kwa
maana ya mfumo wa serikaliza mitaa kuanzia ngazi za chini kabisa kama kijiji,
shehia, mtaana kuendelea, hayajawekewa masharti ya kikatiba.
Rasimuhaikuzungumzia kabisa serikali za mitaa, isipokuwa ibarandogo moja ambayo
inasisitiza kwamba serikali za Washirika‘zitawajibika kustawisha mamlaka ya
wananchi kwa kugatuamadaraka kwa serikali za mitaa zitakazoanzishwa’ kwa
mujibuwa Katiba za Washirika. Hili halina uzito wa maana kwa sababuinawaachia
Washirika mambo muhimu ya kuainisha mfumowa demokrasia. Hoja ya Tume ni kwamba
jambo hilo, pamojana lile la rasilimali na huduma za elimu, afya n.k. sio mambo
yaMuungano na ni juu ya Washirika kuyashughulikia katika katibazao jinsi
wanavyoona inafaa. Ni vigumu kuikubali hoja hii kwasababu Katiba ya Shirikisho,
inatakiwa, kama katiba mama,kuweka misingi ya mfumo na miundo ya mambo haya ya
msingi.Kitakachofanyika na katiba za Washirika ni kufafanua, kwa mujibuwa hali
yao halisi, bila kuivunja misingi iliyowekwa na katiba yaShirikisho. Haieleweki
kwa nini, kwa mfano, haki za binadamuzimewekwa kwa ufasaha mkubwa katika Rasimu
wakati haki zabinadamu sio jambo la Muungano. Kwa nini, kwa mfano, tunu,malengo
n.k. yame rudiwarudiwa katika rasimu wakati hizizinaweza zisitiliwe mkazo katika
Katiba za Washirika? Na papohapo hoja inatolewa kwamba madaraka ya umma na
usimamizi
37. wa rasilimali sio jambo la Muungano
na kwa hivyo hayakuguswana rasimu. Hoja hii, kwa heshima, haina
mshiko.Inaelekea tulitarajia mlima, tukapewa kichuguu. Hata hivyo, labdahatujapoteza
yote. Hii ni rasimu ya kwanza, bado kuna nafasiilimradi tuhakikishe kwamba
mijadala juu ya rasimu haiharakishwina inakuwa huru bila kuingiliwa, na
wananchi kutishwatishwa.Wananchi waielewe vizuri rasimu na maana yake halisi
kwa undaniili waweze kuijadili na kuitafakari kikamilifu na kwa kina.
HITIMISHO
Katika kuhitimisha mhadhara wangu
nitarejea kwenye udhaniau hypothesis yangu. Nilisema kwamba ninavyodhani
mimi,masharti mengi ya Rasimu yalikuwa maamuzi ya maelewano kwamaana ya
compromise na sio mwafaka kwa maana ya consensus.Baada ya uchambuzi wangu,
ninadiriki kusema kwamba muundowenyewe wa serikali tatu uliopendekezwa ni
compromise kati yawale waliosimamia serikali mbili na wale waliopigania
muunganowa mkataba, kwa maneno sahihi, kuuvunja muungano. Wanaserikalimbili
waliona afadhali kuwa na Muungano, hata kama niwa serikali tatu, badala ya
kuuachia uvunjike; wakajifariji kwamatumaini ya dhamira ya wananchi na nia ya
viongozi.Wana-mkataba wakaona kuwa kwa wakati huu wakubali serikali tatu wakijua fika kwamba muundo wa
serikali tatu hautadumu na vyovyote vile utavunjika.Nilisema
pia kwamba compromise inazaa uamuzi legelege.Compromise juu ya muundo, kwa
maoni yangu, imezaa muundowa muungano legelege. Kuna maeneo mengi nimechambuana
kudhihirisha kwamba yatazaa migogoro ambayo hatimayeinaweza kuuvunja Muungano.
Kero za Muungano zitaendelea,safari hii kutoka pande zote mbili.
38 Muungano ukivunjika hakuna
mwananchi atakayenusurika,awe wa Tanganyika au wa Zanzibar. Tuna mifano mingi
ya hivikaribuni. Shirikisho la Sovieti liliposambaratika, likazaa migogorona
vita vya wenyewe kwa wenyewe – mgogoro wa mpaka kati yaUzbekistan na Krygistan;
mgogoro kuhusu maji kati ya Uzbekistanna Tajikistan; vita vya Chechnya
visivyoisha; vita kati ya Azerbaijanna Armenia, n.k. Waliofaidika ni mashirika
ya kibeberu ambayowalitua kama tai kupora rasilimali za Urusi.Shirikisho la
Yugoslavia lilipogawanyika likazaa vita katika eneolile kiasi kwamba mpaka leo
halijatulia. Wanasiasa wenye uchuwa madaraka wakisukumwa na nchi za Magharibi,
wakatumiauhasama wa jadi kati ya makabila na dini kushawishi
mgawanyiko.Makabila na dini zilizofanya kazi kwa pamoja, kwa kiasi fulani,
chiniya uongozi wa Rais Tito, na mfumo wa Shirikisho, yakagawanyika.Leo hii
nchi ambayo ilikuwa na amani kwa zaidi ya miongo mitatuimegawanyika katika nchi
kama saba (Croatia, Serbia, Bosnia,Macedonia, Montenigro, Kosovo na Slovenia).
Na vita badovinaendelea. Waliofaidika ni nchi za Magharibi kupitia NATO
yao.Mwandishi mmoja anaweka wazi maslahi ya nchi za Magharibikatika
kusambaratisha Yugoslavia. Nimnukuu kwa sababu mfanohuu una mengi ya
kutufundisha:Beginning in 1990 Germany and the United Statessought and achieved
the breakup of Yugoslaviain two stages—1992-1995 and 1998-1999. TheGerman
government aimed at this division becauseit wanted to include as territory of
its “vital interest”Slovenia and Croatia, the most economicallydeveloped states
of the Yugoslavian confederation. …Through them Germany would achieve access to
theAdriatic Sea.
39 The United States was interested in
the more recentlyestablished states (Bosnia, Serbia, the former
SocialistRepublic of Macedonia), which controlled the onlyroute from east to
west and from north to south throughthe Balkan mountains. The Balkan area,
along withRomania, Bulgaria, Turkey and the Arab nations, formsa
European-Middle East bloc, which the United Stateswants to control (including
the former states of theSoviet Union—Kazakhstan, Azerbaijan,
Turkmenistan,Tajikistan) for the complete exploitation of the great oilresources
of the Caspian Sea.
10 Na hapa, karibu na nyumbani, Sudan
ya Kusini ilipojitengakumekuwa na migogoro juu ya mafuta, ambayo bado
inaendelea.Nimewahi kusema na ninarudia. Suala la Muungano sio letu tu.Kuna
nchi za kibeberu zina maslahi makubwa ya rasilimali pamojana ya kijeshi katika
eneo letu, hasa Bahari ya Hindi. Tukibezamambo haya nyeti kwa sababu tu ya uchu
wa madaraka ya viongoziwachache, tutawapeleka watu wetu kwenye hali mbaya.
***
Tume imesema, ingawa hatujaiona taarifa
yao rasmi bado, kwambawananchi wengi walitaka serikali tatu. Lakini, kwa
heshima,ningependa kuhoji msimamo huu. Jukumu la Tume halikuwa tukukusanya
maoni na kuhesabu nani amesema nini. Jukumu laTume lilikuwa ni kupokea maoni,
kuyaainisha na kuyachambuaili kupata kiini chake na sababu zake. Wajumbe
walipoambiwa nawananchi wa eneo moja kwamba wajengewe india
ndogondogo,haikumaanishwa hivyo, bali wananchi walikuwa wanadai hospitali;kwa
kuwa viongozi wanapelekwa India kupata huduma za kiafya,basi wao pia wakataka
wajengewe hospitali bora katika maneneoyao na wote, viongozi na wananchi,
watibiwe humohumo nchini.
40. Hatimaye, ukiangalia kwa undani
kero za Muungano, kwamfano, suala lenyewe sio idadi ya serikali bali ni la
demokrasia.Wazanzibari kwa muda mrefu tu wamedai haki yao ya kujiamuliamambo
yao wenyewe; kushirikishwa katika maamuzi muhimu;kutokudhalilishwa, na kupewa
heshima ya mshirika huru. Madaihaya ni halali. Hoja yangu kwa muda mrefu ni
kwamba tusiangaliesuala la Muungano kwa jicho la idadi ya serikali bali kwa
mtazamowa demokrasia. Na tukifanya hivyo tunaweza kubuni muundowa kipekee
kutokana na historia yetu na hali halisi ya Washirikakutokuwa na uwiano wa
uchumi, eneo au idadi ya watu.Muundo wa serikali tatu, au shirikisho kama
unaoainishwa,unajikita kwenye usawa wa kisiasa (political equality). Kwa
msingihuu, uwakilishi, hususan katika vyombo vya kuchaguliwa, haunabudi uwe
sawa bila kujali idadi ya watu. Lakini katika hali yetuya uchumi, mchango wa
Washirika katika gharama za shirikishohauwezi ukawa sawa, wala sio haki, kwa
sababu hatuna usawa wakiuchumi. Kwa vyovyote vile, Tanzania Bara itachangia
asilimiakubwa ya gharama za Shirikisho. Hatimaye, anayelipa mpigazumari ndiye
anayechagua wimbo.Kwa maoni yangu, kama tungekuwa na mtazamo wa kidemokrasiatungeweza
kubuni muundo ambao unakidhi matakwa ya pandezote mbili bila hatari ya kuuvunja
Muungano. Mimi binafsinimewahi kutoa pendekezo la muundo mbadala. Mara ya
kwanzaniliwasilisha pendekezo langu kwa Baraza la Wawakilishi kamamiezi
michache iliyopita. Kwa muhtasari, nilipendekeza dolakamili mbili, la Zanzibar
na la Muungano. Bunge la Muunganolitakuwa na mabaraza mawili, Baraza la
Wananchi na Baraza laNchi. Wajumbe wa Baraza la Wananchi watachaguliwa mojakwa
moja na wananchi wa pande zote mbili kutoka majimboni.Baraza la Nchi litakuwa
dogo lenye, tuseme kama wajumbe 30,15 kutoka Bara na 15 kutoka Zanzibar
wakichaguliwa na Bunge
41. la Zanzibar na wabunge kutoka Bara
katika Baraza la Wananchiilimradi wasiwe wajumbe wa bunge lolote lile. Na
nilipendekezaorodha tatu – moja ya mambo ya muungano, nyingine ya mamboya
kushirikiana (concurrent matters) na orodha ya tatu ni juuya mambo ya pamoja
(joint interest). Kutokana na muda siwezikufafanua; nia yangu ni kudhihirisha
kwamba muundo mbadalaunawezekana.Rasimu imezinduliwa. Imeanza kujadiliwa.
Tuchukue nafasi hiikuijadili kwa makini ili hatimaye malengo na matumaini ya
waliowengi yatimizike. Makamu Mkuu wa Chuo, wanakigoda
wenzangu, rafiki zangu na wageni waalikwa. Mhadhara
huu ulikuwa ni mchango wangu wamwisho katika wadhifa wangu wa Nyagoda wa
Mwalimu Nyererelakini, nikiwa na uzima wa afya, hautakuwa mchango wangu
wamwisho katika mijadala ya kitaifa.Nawashukuru sana kwa kunisikiliza.
Ahsanteni na kila la heri.
No comments:
Post a Comment