Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Tuesday, June 25, 2013

Kesi ya Chadema yaendelea kupigwa kalenda hadi Juni 24


       Kesi ya vigogo wawili wa Chadema wanaotuhumiwa kumtolea lugha ya matusi Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi, Mwigullu Lameck Nchemba, imeendelea kupigwa kalenda baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi kudai kuwa haijakamilisha kuandika uamuzi wa ama washtakiwa wana kesi ya kujibu ama la. Uamuzi huo uliokuwa utolewe Juni 24, mwaka huu, uliahirishwa na kudaiwa kuwa ungetoka juzi, pia uliahirishwa na sasa unatarajiwa kutolewa Julai Mosi. Hakimu anayesikiliza kesi hiyo, Ruth Massamu, alisema bado anamalizia kuandika uamuzi huo na kwamba siku hiyo si lazima washtakiwa kufika mahakamani hapo hata wadhamini na wakili wa washtakiwa watatosha kusikiliza uamuzi huo.
     Vigogo hao ni Ofisa Sera na Utafiti wa Chadema makao makuu, Mwita Waitara (Mwikwabe (37) na Dk Kitila Mkumbo Mshauri Mkuu wa chama hicho. Vigogo hao wanatuhumiwa kutenda kosa hilo Julai 14, mwaka jana saa 10:00 jioni. Kwa mujibu wa Mwanasheria wa Serikali, Seif Ahmed, washtakiwa bila halali, walimtusi Mbunge Mwigullu kuwa ni malaya, mzinzi na mpumbavu huku wakijua wazi kuwa kitendo hicho ni kinyume na sheria. Seif alisema,washtakiwa hao bila halali, walitenda kosa hilo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Nguvumali kwa lengo la viongozi wa Chadema kuzungumza na wananchi. Kesi hiyo tangu kuanza kwake imekuwa ikisogezwa mbele mara kwa mara huku upande wa mashtaka ukisubiri kwa hamu haki itendeke.
Source: Andres G. (June 2013). Kesi ya Chadema yaendelea kupigwa kalenda hadi Juni 24. Retrieved from Mwananchi

No comments: