Mohamedi Mtoi |
Baada ya uchaguzi si vibaya tukaona tathimini na uchambuzi wa uchaguzi na matokeo.
Katika uchaguzi uliofanyika jana kwenye kata 22 Tanzania bara chama tawala (CCM) na chama kikuu cha upinzani nchini (CHADEMA) vilitoshana nguvu kwenye uchaguzi huo ambapo kwenye baadhi ya maeneo vurugu na matumizi ya nguvu ya dola vilitamalaki kutokana na dosari kadhaa.
Tathimini hii fupi haitajikita kwenye uchaguzi mzima, bali ijadili kwa kina cha mantiki katika maeneo matatu (3) tu.
1.0. KABLA YA UCHAGUZI
2.0. UCHAGUZI NA MATOKEO
3.0. HAKIBA YA MANENO
.............................. ..................
1.0.1. KABLA YA UCHAGUZI
• Kabla ya uchaguzi CCM ndio walikuwa wanaongoza kwa kuwa na kata nyingi, walikuwa na kata 20, kata hizo 20 baadae zilikuwa wazi kutokana na baadhi ya madiwani kuhama, kujiuzulu na wengine kufa (sitataja kata moja moja na sababu za kila kata kuwa wazi).
• CHADEMA walikuwa na kata 5, kati ya hizo kata tano madiwani wanne (4) wa Arusha mjini walivuliwa uwanachama na hivyo nafasi zao kuwa wazi, na kata moja ya Isike - Singida diwani alihamia CCM.
• TLP walikuwa na kata moja, kata hii ilikuwa wazi baada ya diwani wake kufariki, hii ni kata ya Minepa - Ulanga mkoani Morogoro.
»» Kwa rejea binafsi, kata zote zilizo kuwa wazi pamoja na halmashauri zake kwenye mabano ni:-
Stesheni (Nachingwea), Nyampu Lukano na Lugata (Sengerema), Genge Tingeni (Muheza), Ibugule (Bahi), Langiro (Mbinga) na Manchila
(Serengeti). Nyingine ni Iyela
(Mbeya), Mbalamaziwa
(Mufindi), Ruzewe Mashariki
(Bukombe), Mianzini (Temeke),
Dalai (Kondoa), Minepa
(Ulanga), Makuyuni (Monduli)
na Bashnet (Babati). kata nyingine ni Kimandolu, Elerai, Kaloleni na Themi (Arusha), Iseke (Singida), Dongobesh (Mbulu), Ng’ang’ang’e (Kilolo), Ifakara (Kilombero), Msanze (Kilosa) na Mnima (Mtwara).
2.0.1. UCHAGUZI NA MATOKEO
• Kata ishirini na mbili (22) ndio zimefanya uchaguzi huku kata moja ya daraja mbili (Arusha mjini) ikiwa haijatangazwa kabisa kuwa iko wazi wakati aliyekuwa diwani (Alfonce Mawazo) Kwa tiketi ya CCM alihamia CHADEMA, huku uchaguzi kwenye kata nne (4) za jimbo la Arusha mjini uchaguzi ukiahirishwa mpaka 30 Juni, 2013 kutokana na mlipuko wa bomu siku ya mwisho ya kuhitimisha kampeni za CHADEMA ambapo watu wawili walifariki na wengine zaidi ya 73 kujeruhiwa.
• Uchaguzi ulifanyika na kugubikwa na matukio yasiyo tia afya demokrasia ya vyama vingi, hata hivyo pamoja na mapungufu na changamoto hizo ambazo tathimini hii haita zigusa kwa kina na uzito wake itoshe kusema kuwa mazingira bado hayajawa rafiki kwa kuzingatia mila na desturi za chaguzi huru na haki kwenye mfumo wa kidemokrasia kwani bado vyama pinzani haviwekwi kwenye mizania linganifu na chama tawala.
» Matokeo katika uchaguzi huo yanabeba funzo na taswira muhimu kwa vyama vikuu viwili shindani (CCM na CHADEMA) na yanatoa somo lenye ukweli mchungu kwa vyama vya CUF, NCCR mageuzi, TLP na vingine ambavyo havikuambulia kiti hata kimoja na vyama vingine kushindwa kusimamisha wagombea.
• Katika uchaguzi huo wa kata 22, CCM walikuwa wanashikilia kata 20 na wamefanikiwa kurejesha kata 15, kwa maana hiyo wamepoteza kata zao 5, CHADEMA walikuwa wanashikilia kata 1 na TLP kata 1, CHADEMA wamefanikiwa kurejesha kata yao 1 na kuichukua kata 1 ya TLP na kata nyingine 5 za CCM, jumla CHADEMA imepata kata 7.
•» KABLA YA UCHAGUZI
Kabla ya uchaguzi wa kata hizo 22 ilikuwa hivi, CCM kata 20, na CHADEMA kata 1, (20-1=19). Tofauti ilikuwa kata 19.
•» BAADA YA UCHAGUZI.
Baada ya uchaguzi ukitafuta tofauti ya kata kati ya CCM kata 15 na CHADEMA kata 7 unapata 8 (15-7=8). Tofauti ni kata 8.
3.0.1 HAKIBA YA MANENO.
• Nguli wa Fasihi Afrika mashariki na kati na mzaliwa wa Pangani mkoani Tanga Bw Shabani Robert alisha tuasa kwenye maandiko yake kuwa "tuweke hakiba ya maneno" nami naweka hakiba ya maneno.
• Ukifanyika uchaguzi wa kata 4 za Arusha mjini hiyo tarehe 30 Juni, 2013 kama ilivyo pangwa, kata ambazo zilikuwa zinashikiliwa na chadema kukamilisha idadi ya kata 26 halafu chadema wakashinda kata zao zote 4, hesabu kwa upande wa chadema itakuwa 7 + 4 = 11. CCM wao wataendelea kubaki na kata zao 15.
• Tofauti itakuwa kata 4, yaani (CCM 15 - CDM 11=4), kwa mnyumbulisho huu bila shaka viongozi wa vyama pamoja na wanachama wanao weza kutembea kifua mbele kati ya wale wa CCM na wale wa CHADEMA, ni CHADEMA na si CCM, NARUDIA, viongozi na wachama wa vyama viwili (CCM na Chadema) wanao taakiwa kutembea vifua mbele kwa mafaniko ni CHADEMA.
• Tofauti ya kuzishikilia kata kabla na baada ya uchaguzi wa kata 4 zilizo baki utaonyesha mwanya mkubwa sana!
» Kabla, CCM 20 chadema 5 (20-5=15)
» Baada, CCM 15 Chadema 11
(15 - 11= 4).
»» Yaani kutoka tofauti ya kata 15 hadi tofauti ya kata 4.
Tunaanza na Mungu, Tunamaliza na Mungu.
No comments:
Post a Comment