Tarehe 21 /5/2013 Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) L iberatus
Sabas ambaye ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha aliongea na waandishi wa
habari juu ya shutuma zangu juu ya ujumbe wa maneno mfupi niliopokea kutoka kwa
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bwana Magessa Mulongo siku ya tarehe 25.04.2013 kutoka
kwenye namba anayotumia mkuu wa Mkoa namba 0752960276 namba ambayo imesajiliwa
kwa jina la Magessa Mulongo kwenda namba 0764150747 namba ambayo imesajiliwa
kwa jina la Neema Lema namba ninayo tumia Mimi , ujumbe unaosema “
Umeruka kihunzi cha kwanza nitakuonyesha kuwa mimi ni Serikali , ulikojificha
nitakupata na nitakupa kesi ninayotaka mimi “
Nimesikitishwa na kufedheheshwa sana na taarifa hii ambayo sasa
inathibitisha bila mashaka kuwa Jeshi la Polisi Arusha hasa Mkuu wake anatumika
na sina shaka kusema kuwa yeye ni KIPEPERUSHI cha Mkuu wa Mkoa , baada ya Mimi
kupokea ujumbe huu tarehe 25/4/2013 nilitoa taarifa kwa vyombo vya habari na
nia yangu ya kwenda mahakamani juu ya vitisho hivi .
Haya yafuatayo ni maswali ya msingi ninayojiuliza bila kupata
majibu sawia kuhusu taarifa ya Jeshi la Polisi na Mtandao wa simu wa Vodacom .
1) Kwani nini Jeshi la Polisi walikataa kuchukua maelezo yangu
Mimi juu ya tuhuma hizo nzito dhidi ya Mkuu wa Mkoa ambaye amenitumia meseji
kupitia simu yake ya mkononi kama ninavyolalamika ? lakini pia ni muda
takribani mwezi umepita tangu nimetoa malalamiko yangu je katika kipindi chote
cha mwezi mzima Jeshi la Polisi waliona ni busara kwenda Kampuni ya Vodacom
kutafuta mawasiliano yangu na Mkuu wa Mkoa bila hata kuchukuwa maelezo ya
mlalamikaji ambaye pia kwa nafasi yake katika Jamii ni Mbunge ?
2) Nilipokuwa rumande Msaidizi wa Mkuu wa Makosa ya Upelelezi
Arusha alinifuata na kuniomba nimpe simu yangu, nilimwambia sina nimemwachia
Mke wangu na walimtafuta Mke wangu na kumuomba hiyo simu na kumuhakikishia kuwa
akiwapa simu wataniachia na kunifutia kesi na Mke wangu aliwajibu kuwa simu
alidondosha kwenye gari ya Polisi ile ambayo walinichukua nayo usiku wa siku
waliyonikamata , waliita ile gari wakatafuta hiyo simu na walipokosa walichukua
pochi ya Mke wangu na kumwaga vitu vyote na kuanza kuitafuta simu na kumpekua ,
Je Polisi hapa walikuwa wamekusudia nini ?
3) Kwa namna ya kawaida sana ya upelelezi baada ya Polisi na
Vodacom kukuta simu ninayotumia imesajiliwa kwa jina lingine katika msingi wa
kawaida wa utafiti Kama ambavyo naelewa au kufikiri vyema huyu mwenye Jina hili
angetafutwa kwani meseji ilionekana imetoka kwa Magessa Mulongo na imekwenda
kwa Neema Lema , lakini aliyekuwa analalamika ni Godbless Lema , je kama Polisi
sio Kipeperushi cha Serikali walipata wapi ujasiri wakutoa maelezo waliyotoa
wakati kwenye usajili wa mitandao ya simu namba 0764150747 imesajiliwa kwa jina
la Neema Lema bila hata kuchukua nafasi ya kumtafuta Neema Lem a kujua ni nani
huyo ambaye simu yake inatumiwa na Mtu mwingine ? na ni kwanini Polisi
hawakusema kuwa mimi nimedanganya kwani namba hiyo sio yangu ni ya Neema Lema ?
4) Mimi kama mteja ni nayetumia namba 0764150747 nimehiifadhi
namba ya Magesa Mulongo 0752960276 kama ( RC ARUSHA VODA) na ndio jina
lililokuja na ujumbe wa vitisho katika simu ninayotumia . Vile vile katika
barua ya Vodacom kuna maelelzo ambayo ni ya mashaka , kwamba namba ya simu ya
Magesa Mulongo ilituma meseji kwenda namba 0764150747 yenye usajili wa jina la
Neema Lema kuwa ni kweli kuwa meseji ilitumwa na namba ya Mulongo isipokuwa
Center number sio ya Vodacom , swali , kama namba ya Mulongo ni ya Kampuni yao
ndio iliyotuma meseji basi hata hiyo center number ni ya kwao kwani kama
ingekuwa sio ya kwao Kampuni ya Vodacom isingeweza kuona taarifa zake katika
mfumo wake wa mawasiliano na kuzitolea taarifa hivyo kama wameweza kuwa na
taarifa zake maana yake ni kuwa mawasiliano hayo yamepita katika mitandao yao
ndio maana Kampuni ya Vodacom imepata taarifa za mawasiliano haya na
kuyathibitisha kwa Polisi bila hata Kampuni yenyewe kuchuka nafasi ya kumtafuta
mlalamikaji na kujua nini kilichotokea kwenye simu yake , lakini vile vile mimi
kama mteja sina wakati wa kukagua center number pindi napotumia simu yangu na
sijawahi kufanya hivyo na wala sijawahi kuzingatia kwani sio wajibu muhimu
katika matumizi ya simu yangu ya mkononi.
5) Wakati Polisi walipoita vyombo vya habari dhana muhimu hapa
ilikuwa ni kutaka kumsafisha Mkuu wa Mkoa na ndio maana barua ya Vodacom kwenda
Polisi iko kwenye mitandao ya kijamii jambo mabalo Polisi au Vodacom
wasingepeswa kufanya hivyo kama kungekuwa hakuna malengo ya kisiasa katika
taarifa hii lakini kitendo cha Polisi cha kutoa taarifa bila kuona meseji
kutoka katika simu ninayotumia huu ni uhuni mwingine ambapo ni wa msingi kwa
Jeshi la Polisi kwani taarifa zinaonyesha kuwa Polisi wote ambao wamekuwa
watesaji na waonevu kwa Viongozi wa Upinzani wamekuwa wakipanda vyeo na kupata
thamani kubwa machoni kwa Watawala dhalimu na mifano halisi ya wazi iko mingi.
6) Ni dhahiri kwamba zinatumika njia nyingi kumsafisha Mkuu wa
Mkoa kwa masilahi ya Serikali . Katika kesi ya uzushi niliyofunguliwa na Polisi
ujumbe huu wa meseji utatumika kama ushaidi na mahakama itaona na kufafanua
ukweli halisi , hivyo wote wanoangaika wasubiri kwani hivi punde tutakutana
mahakamani .
GODBLESS J LEMA ( MP)
26/5/2013

No comments:
Post a Comment