Swali la Ugomvi: Kama maneno
yaliyonukuliwa kusemwa na Prof. Ibrahim Lipumba kuwa chama chake kilifanya
kampeni ya kidini ili kuhakikisha kuwa Kikwete ashinde kwa kura za Waislamu
basi maswali angalau matatu yanahitaji kujibiwa:
1. Je chama cha CUF ni chama cha
Waislamu? kama ndio (ilivyooshiriwa na Lipumba) kwanini kiendelee kuwa chama
cha siasa?
2. Je, Lipumba anastahili kuendelea
kuongoza chama cha kitaifa? Wakati watu wanapigania umoja zaidi baina ya watu
wetu inakuwaje mwenyekiti wa chama cha pili kikubwa cha upinzani nchini kuja na
kauli kali zaidi za kutugawa? Kwanini asiamue kujiuzulu Uenyekiti wa CUF?
3. Je Kikwete na CCM walishiriki vipi
katika mpango huo wa kuhujumu uchaguzi mkuu kwa misingi ya dini? Je CCM walijua
mpango huu wa CUF na Lipumba?
Kusoma
aliyo sema Prof Lipumba nenda hapa Lipumba aibua jambo zito

No comments:
Post a Comment