Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Thursday, May 1, 2014

UVCCM Mvomero yaanika U-Mizigo wa Madiwani.

Na Bryceson Mathias, Turiani, Mvomero

MALUMBANO ya Jumuia ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Mvomero, yameingi hatua mpya ambapo baadhi ya Wajumbe wameanika sababu zinazopelekea wawaite madiwani hao Mizigo, Wazee, Viwete na ambao hawana Tija.

Hayo yamefuatia Vitisho vya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mvomero, Jonas Van Zealand, aliyesema  Baraza la Madiwani wamekubaliana kumpa siku 14 Mwenyekiti wa UVCM, Paschal Boga, athibitishe kwao na ndani ya chama kauli yake hiyo ya kibaguzi ukiwemo uzembe wetu katika vikao.

Mmoja wa wajumbe aliyetaka jina lisitajwe alidai, pamoja na vitisho tunavyopata, Umizigo wa Madiwani hao ni pamoja na kukumbatia udanganyifu wa Diwani mwenzao aliyetoa ‘Taarifa ya Uongo’ mwaka jana kuwa Zahanati ya Mlaguzi ya Mil.36/- ipo kwenye Lenta wakati hata Msingi tu haujamalizika.

“Kuna Mradi wa Maji safi wa Turiani-Mvomero wa Mamilioni ya Fedha, ambao Mabomba yake yametelekezwa Turiani ambapo Jua, Mvua, Giza, Mbalamwezi na Vumbi ni Kanukato.

‘Mradi wa namna hiyo hiyo pia upo Mvomero, Kilosa na Gairo, kiasi ambacho Makandarasi wa Miradi hiyo kwa sasa wameamua kutelekeza vyombo vyao mfano; Mvomero na kuamua kuondoka zao kwa sababu, fedha ya kuwalipa haieleweki iliko”.alisema mmoja wa Madiwani.

Mjumbe mwingine naye alisema, pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri, Jonas Van Zeeland, kujinasifu kuwa Baraza la Madiwani limefanya Kazi kubwa ya kujitoa Muhanga ikiwemo kuwaondoa na kuwashitaki watendaji waliokuwa kikwazo cha maendeleo, alidai,

“Licha ya kumtuhumu aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Sarah Limuma, kwa kufuja Malilioni ya fedha za Halmashauri hiyo, bado madiwani hao hawawezi kukwepa Lawama za uwajibikaji kwa sababu, Uhalibifu na Uzembe mwingi unatokea chini ya usimamizi wao”.

Wananchi wa maeneo ya Miradi ya Maji na Zahanati inayosuasua na fedha kudaiwa kutafunwa walipohojiwa kwa nyakati tofauti walidai, “Pamoja na kwamba Mwenyekiti Van Zeeland amedai Halmashauri imejipanga kuhakikisha wanapata hati safi kwa mara ya kwanza toka ianzishwe 2003, akumbuke ‘Pema usijapo Pema ukipema si Pema tena”.  

Awali Mwenyekiti ambaye katika Kikao cha Baraza la UVCCM cha Februari 15 mwaka huu, aliwatuhumu Madiwani wa Halmashauri hiyo kuwa ni mizigo maana wameshindwa kutekeleza ilani ya CCM.

No comments: