Hali ya utulivu NDANI ya ccm inaelekea kuvurugika sana (kama nilivyodokezewa na mdau wa NDANI kabisa), na woga uliowakumba sasa umekuwa hasa baada ya UKAWA kulikacha Bunge la Katiba (iliyokuwa karata ya CCM kujihalalishia kuendelea kukaa madarakani), na hivyo kukosea na kufanya UKAWA 'Wakatoka na hoja thabiti' zenye ushahidi wa wazi kwa wananchi kuwa wao CCM kwa makusudi, (wakitumia pia baadhi ya wale 201) ndio walikuwa CHANZO cha uchochezi, ubaguzi na kuvuruga maoni ya WANANCHI, Jambo ambalo wanakiri endapo UKAWA watajitangaza vyema kwa umma, ambao umeshakata tamaa, 'watawamaliza kwa hoja za kweli' ...kosa kubwa ambalo litawawia ngumu sana kwa Ccm kujitetea au kusahihisha hata waendapo kuwaelezea.
Jambo la pili, ni hoja za kuhusianisha baadhi ya vyama na udini, ukabila, ukanda, uchu wa madaraka, na uchochezi, mambo ambayo wao CCM wenyewe wameyatumia hapo awali kudhoofisha vyama wanavyoviogopa, lakini sasa WAO CCM 'wamekamatwa ready handed' ndani na nje ya Bunge la Katiba wakiyaimba, kutenda na kuhamasisha wengine wayatende (dhidi ya wananchi wenzao), bila kufichana au kuogopa. Hii imewafichua sana mbele ya umma uliokuwa unafuatilia vikao vya Bunge na vyombo vya habari, Ccm wanaweweseka sana kwa hili.
Jambo la tatu, baada ya UKAWA kuonekana kuwa sasa 'hawana tena mzaha' (compromise) na siasa mbovu za CCM na hivyo kuonekana kama wanasimama imara zaidi kwa ajili ya umma, sio kwa Katiba mpya pekee bali kuendelea hadi uchaguzi MKUU wa 2015 na kuendelea, hii imezidi kuwafanya CCM ngazi zote kujaa woga mno na kuweweseka kuogopa 'Kupotea' ktk uchaguzi MKUU ujao. Hii hatari wameiona wazi na hawajui nini kitatokea kama kweli UKAWA wataamua kumsimamisha mgombea MMOJA ktk ngazi zote, kama Urais, ubunge, udiwani nk...! Ccm watajipanga kukwamisha dhamira hiyo...na endapo itawakwama...wanajiandaa kimkakati, kisaikolojia ikiwa ni pamoja na 'kujilinda'.
Mwisho, CCM baada ya kuuona UKAWA ikiivuruga ktk Mikutano ya kushtua ya Kibandamaiti Unguja jana na wa leo hii Pemba, inaanza kujipanga vyema kwa Uchaguzi mkuu 2015, kwa kuanzia kuchomekea ktk midahalo na hotuba zao jambo watakaloliita hoja ya 'kukubali serikali ya umoja wa kitaifa' ikiwa ni karata yao ya mwisho ya kuzugia (kama walivyofanya wenzao wa vyama tawala Zimbabwe, Zbar, Kenya, nk ) kama maandalizi 'kisaikolojia' endapo watashindwa kupenya na kushinda ktk uchaguzi MKUU ujao. Kwa karata hii, CCM wanajua watafanya 'Zimbabwe style' kujijumuisha na kutafuta muafaka na 'mshindi' wa UKAWA, (ili kujilindanda) na baadaye kuua nguvu za UKAWA na kufifisha upinzani Mfano wa yaliyomkuta Tsivangirai, Zimbabwe. Hii ni ni dalili ya kweli MAANA hata JK alivyokuwa anamtambulisha mwakilishi toka Serikali ya Zambia (Dr Guy Scott, ambaye ni mzungu aliyetokea chama cha upinzani)...JK alidokeza Jambo kwa kusema ...'huu ndio umuhimu wa serikali ya 'Umoja wa Kitaifa''... hapo JK alidokeza hali ya baadaye ambayo inaweza kutokea hapa endapo CCM itashindwa 2015.
Je, TUPO tayari kwa Ccm kuja style hii? Je, UKAWA ipo na 'picha kubwa' ya baadaye ambayo maCCM yanajipanga kuja nayo?
Naomba kuwasilisha kwa mjadala...! Mjumbe hauwawi..
No comments:
Post a Comment