Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Thursday, May 1, 2014

JK; Haya yalistahili kusemwa na wajumbe wa Bunge la Katiba?

Na Bryceson Mathias

WANANCHI wengi tumejiuliza; Baadhi ya Wajumbe walioteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kwa ajili ya Bunge Maalum la Katiba walistahili kuwemo na Je Matusi, Kejeli na Mipasho hii; Ilistahili bungeni?  Lakini pia tunahoji, yaliyosemwa na Wabunge hao Mahiri yalistahili?

Nasema hivyo kwa sababu, nafasi iliyowateua na Ueledi wao wa Vinywa, haufanani na kile tulichokitarajia kwao, ili kipelekee walambe Mamilioni ya Kodi yetu kwa siku 90, huku wakituachia Matusi, Kejeli, Mipasho na Vitisho hata vya kutaka kuuua Mungano?

Baadhi ya kauli tata zilizotolewa na wanaojiita waheshimiwa ni pamoja na, Asha Bakari Makame, Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT) wa Chama cha Mapinduzi (CCM). 

Makame ambaye Uadilifu na Ueledi wake unatakiwa uigwe na Jamii anayoiongoza, alishangaza watu alipomtolea Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Ismail Jussa, kuwa anafanana na watu wenye mabusha nyuma ambao ndiyo huufyata.

Tusingetegemea Mteule wa Rais, Makamu Mwenyekiti wa UWT ambaye angepaswa awe Kioo cha Nyumba, Ndoa, Familia, Jamii na Taifa, abwatuke Matusi, Kejeli na Mipasho kama hiyo! Je alaumiwe nani kama si Rais aliyemteua na wanawake waliomchagua?.

Alikwenda mbali zaidi na kumwambia Jussa kuwa ana matatizo ya kiafya, si mwanamume kamili, kwani ameshindwa kuoa, hana watoto wakati ana umri mkubwa! Msemaji huyu, anafaa kweli kuwa Kiongozi na Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba?

“Huyu Jussa anasema kwamba tumeufyata, hapa tuwekane sawa, maana ya kuufyata ni mtu kuwa na mabusha pale yanapokuwa nyuma ndiyo kuufyata kwa hiyo yeye ndiyo ameufyata, ana busha huyu,” alisema Makame ambaye angekuwa Mu-Islam Safi anayemuogopa Mungu.

Najiuliza; Wanawake wa UWT ambao wangeiga tabia na Mwenendo wake wa Ueledi ndani ya CCM, UWT na Jamii ili wawaelekeze akina Mama na Vijana wanaoukulia umoja huo; Je, waige tabia hiyo? Anaifundisha nini Jamii?

Mwanakhamis Kassim Said; Yeye alijigamba: “Mimi nilikuwa namwomba baba yangu mdogo, Maalim Seif Sharif Hamad, awarejeshe watu wake bungeni kwa sababu ya mpira unachezwa ndani. Hatutakii mema humu, tena ana Choyo na Husuda. 

“Namwomba baba mdogo atuache, alichokitaka amekipata, anazunguka saa 24 na king’ora Dar es Salaam, Unguja. Mheshimiwa Mwenyekiti Baba mdogo kila mara yuko kwenye Ndege,  mara Uingereza, mara Canada mara wapi! Hicho ndicho anachokitaka amekipata.”

Kwa Haiba ya Kijamii ya kumuheshimu Baba yako Mdogo, unaweza kumumwagika maneno machafu mbele ya watu ukizingatia umeteuliwa na Rais wa Nchi? Aibu waliyoifanya; Inamwaibisha aliyewateua ya kwamba hawakustahili.

Mohamed Seif Khatibu: “Nimejifunza baadhi ya wanasiasa wa upinzani ni vinyonga. Maalim Seif ni kinyonga, wakipita kwenye mvua wanakuwa na rangi ya mvua, kwenye jua wana rangi ya jua, baharini wana rangi ya bahari.”

Kapteni John Komba alitangaza kuingia msituni Bunge likipitisha Serikali tatu, akimshutumu Mwenyekiti wa Tume, Jaji Joseph Warioba na timu yake kuwa waasi kama Adamu na Eva kutokana na kupendekeza serikali tatu. Komba ana Uwezo wa Msituni? Msituni si Kuimba!

Bernard Membe; Tume ya Warioba itakumbukwa kwa kuratibu mauaji ya Muungano na Bunge nalo litakuja kulaaniwa kwa kubariki mauaji hayo, huku, Paul Makonda akiwaita Ukawa ni watoto wa mashetani.

 Waride Bakari Jabu alidai wanaotaka Muungano uvunjike lakini Tanganyika iwepo asili yake   ni Mkongo; hivyo anasema Muungano utakuwepo na utaendelea kuwapo.”

No comments: