Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Tuesday, May 13, 2014

Ukawa Moro; Mchunguzi wa Chuo Kikuu Morogoro ni Muongo!:

Na Bryceson Mathias, Morogoro.
GAZETI la Serikali la Kiswahili la kila Siku nchini, limemnukuu Mchunguzi mmoja wa Chuo Kikuu cha Morogoro bila kumtaja ni chuo gani, akidai Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), umeshindwa kufanya Mikutano yake Tanganyika kwa sababu wananchi hawawezi kujitoza.
Propaganda na Uongo hilo umo kwenye Toleo la Mei 3, mwaka huu wenye Kichwa cha Hbari Ukawa wanza Mivutano, ambapo pamoja na mambo mengine limedai Viongozi wawili wa Umoja huo wanataka kurejea kwenye Bunge Maalum la Katiba.
Katika kuumba Uongo huo, Mwandishi amehabarisha Jamii kwamba, viongozi hao wawili wa Ukawa, wantaka kurejea bungeni kuendelea na Mchakato wa Katiba Mpya kwa madai kuwa wamebaini kuna Ujanja wa baadhi ya Vyama vinatumiwa, vinadanganywa na havionekani.
“Tulisusa Bunge kwa pamoja, lakini sasa inaanza kuonekana kuwa, wapo wenzetu wana maslahi binafsi, na kuonekana kututumia sisi kwa manufaa yao ya kisiasa hata kifedha”.ilisema taarifa hiyo ambayo mwandishi anasema eti ilisemwa na Kiongozi mmoja wa Ukawa wakati ni uongo.
Mwandishi wa habari hii alifanya utafiti kwenye vyanzo muhimu ya vyuo vyote vya mkoani Morogoro vinayojihusisha na Siasa iwapo kuna ufukunyuku huo, kilichobaini ni kuwepo kwa Propaganda za Kundi la Chama kinachotarajia kupata Usajili wa Kudumu kuanzia Mei 5, 2014.
Mmoja wa Viongozi ambaye ni Muumini wa Chama kilichoko kwenye Umoaja Ukawa alisema, Uchunguzi wa Mwandishi na Mchunguzi huyo wa Chuo Kikuu Morogoro; Ni Waongo wanatumiwa na Kundi lililoshindwa mbinu za kuwarejesha Ukawa bungeni.
Aidha alisema; Ukawa hawajapatiwa fedha zozote nyingi na Mfadhili au Wafadhili wowote toka nje ya Tanzania kama ilivyoripotiwa na Mwandishi na Mchunguzi huyo; Na kwamba ni wanao ushahidi wautoe hadharani kwa sababu uingizwaji wa fedha zozote unadhibitiwa na BOT.
“Mwandishi kama ana uhakika na anachosema, angeweka wazi jina la Mchunguzi huo wa Chuo Kikuu na‘by line’ yake ili tuwaulize, lakini kwa kuwa wameamua kujificha Msituni, taarifa yao haina chembe ya ukweli, wanataka kuwahadaa watu; ‘Watanzania wa Leo sio wa Jana’.alisema.

No comments: