Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Tuesday, May 13, 2014

Mulongo; Nani kafanya Uchunguzi wa Ubabaishaji wa Mabomu Arusha?

Na Bryceson Mathias

‘Kesi ya Tumbili, katu hawezi kuhukumu Ngedele’

KUFUATIA Mauaji mbalimbali yaliyotokea hapa nchini yakihusishwa na Ukatili wa Vyombo Usalama; Maombi yaliyotolewa na wadau walitaka iunde tume huru ya kimahakama iongozwe na Majaji kuchunguza mauaji hayo, lakini Serikali haikuona umuhimu.

Katika Sherehe za Siku ya Wafanyakazi (Mei Mosi) mkoani Arusha mwaka huu; zilitawaliwa na hotuba kuhusu milipuko ya mabomu iliyosababisha vifo vya watu na kuwaacha wengine na ulemavu wa kudumu.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo.akizungumzia matukio hayo alisema uchunguzi wa mashirika ya kimataifa ikiwemo ‘Interpol’ umebainisha kwamba matukio hayo si ya kigaidi bali ni mabomu ya kutengenezwa; Jambo linalonifanya nihoji Tume hiyo ni ya Nani na akina nani walioshirikishwa?

“Hao wataalamu wa kimataifa tulioshirikiana nao wanasema wazi kuwa tujiangalie sisi wenyewe hapa Arusha kwani matukio hayo hayana uhusiano na ugaidi, hivyo ni wajibu wetu kusimamia ulinzi ili kuepuka mabomu,” alisema Mulongo.

Maswali yetu muhimu kwa Mukongo ni haya; Kwa nini uchunguzi huo haukufuata Mchakato uliopendekezwa na Wadau kwamba iwepo tume huru ya kimahakama, iongozwe na Majaji, na badala yake imefanywa baina wachunguzi na watuhumiwa? Hiyo siyo huru ni ubabaishaji.

Kama Watalaam wa Kimataifa wanasema kuwa kuhusu mauaji ya Mabomu hayo mjitazame na kujiangalia ninyi wenyewe hapo Arusha; kwa nini wewe Rais wa Mkoa unakuwa na Kigugumizi cha kuruhusu tume huru ya kimahakama inayoongozwa na Majaji?

Je; katika uchunguzi huo uliofanywa; Familia za Waathirika yaani Wadai, walihusishwa? Ieleweke Wadai hao ni pamoja na Viongozi wa Dini wa Kanisa Katoliki la Joseph Mfanyakazi Olesiti Arusha, Chama cha Demokrasia na Maendelo (CHADEMA), na wengine waliohusika.

Kama uchunguzi huo, ulifanywa bila kuwepo kwa Wahusi halisi wa tukio hilo; Hatuna budi kuupuuza na kuukataa kwa nguvu zote, kwamba sio uchunguzi halali na hauna hata Chembe ya Ukweli, isipokuwa ubabaishaji wa kuihadaa Jamii.

Vitabu yote vya dini vinasema; “Nimwambiapo mtu mbaya, Ewe mtu mbaya, hakika utakufa, nawe husemi neno la kumwonya mtu huyo, aiache njia yake, mtu 
mbaya huyo atakufa katika uovu wake, lakini damu yake nitaitaka mkononi mwako.

“Walakini ukimwonya mtu mbaya kwa sababu ya njia yake, kusudi aiache; wala yeye asiiache; atakufa huyo katika uovu wake, lakini wewe umejiokoa roho yako”

Tunatambua ya kuwa kuificha dhambi ya mtu ni sawa na kushiriki dhambi yake, walakini wapo watu kati yetu wanaowafichia wenzao dhambi zao. Hivyo tunategemea kuwa; Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mulongo na iongozi wenzake; Hamuwezi kuwaficha Waharifu ambao wachunguzi wa kimataifa wamesema mnao mkoani humo.

Ninasema hivyo kwa sababu Mulongo ndiye mwenye Nguvu zote za Dolamkoani humo; hivyo kwa kutumia vyombo vyake vya ulinzi na Usalama kama Mwenyekiti wa Ulinzi na Usalama; atawapata wahusika; Lakini kama hamtawapata, ni hakika Damu ya marehemu itatakwa mikononi mwenu.

Je ni kwa nini watu hukaa  kimya juu ya uovu? Watu wengi hukaa kimya na hukataa kuonya kwa sababu ya uwoga na kuwaonea haya wakosaji na kuwakumbatia? Ni kwa sababu ya Rushwa, Kutomwogopa Mungu na Ufisadi na Njaa iliyoikalia Jamii katika Maisha yao ya kila siku.

Pengine ni vizuri sasa,Viongozi wakajua Wananchi hawataki ubabaishaji.




No comments: