Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Tuesday, May 13, 2014

Nani Kamdanganya, akampotosha na Kumpumbaza Bulembo?

Na Bryceson Mathias

WAKATI wa Michango ya Bunge Maalum la Katiba; Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdalah Bulembo, alimshambulia aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya kuratibu Maoni na Mapendekezo ya Katiba Mpya, Jaji Joseph Sinde Warioba.

Kwa Majigambo Lukuki ya Uongo, Bulembo alijigamba akijinasifu kuwa, “Jaji Warioba hana nia njema na nchi ya Tanzania, ana chuki sana kwani mwaka 1991 alifutwa kugombea Ubunge, hivyo hana nia njema na nchi ndiyo maana anapendekeza Serikali tatu”.alisema Bulembo.

Sielewi, aliyemdanganya Bulembo, akampofusha na kumpoteza, asema mambo ambayo kwa uhakika anajua Jaji Warioba hakuyafanya, na hahusishwi nayo; ambapo wanaojua ukweli, walibaini, Mwindaji amemuua kwa makusudi Mwindaji mwenzake badala ya Mnyama.

Mtu akikejeli wasiokuwa na watoto, wakati kwenye kundi hilo yupo mtu asiyekuwa na mtoto, ni dhahiri kuwa anamsema asiye na Mtoto!. Kama kweli Bulembo ni mkazi wa Mara; anafahamu fika, aliyekatazwa kugombea Ubunge 1991 ni Bosi wake, Stephen Masatu Wassira.

Je, kwa kusema aliyosema; Bulembo si alikuwa anamsema Kijanja kwa kumzunguka Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu, Stephen Wassira? Maana Wassira 1991 mkoani Mara, ndiye aliyefutwa kugombea Ubunge.

Tunasema haya, Jaji Warioba katika kipindi cha dakika 45, mbali ya kutomtambua Bulembo na kumshangaa kwa uadilifu duni kama Mjumbe Maalum wa Bunge la Katiba, hamtambui;  Hivyo amethibitisha kuwa, mtu aliyefutiwa kugombea Ubunge, ni Wassira.

Pamoja na kuropoka kwa Bulembo; hatuwezi kusema, labda Wassira alimtuma aseme hivyo; Maana katu hatujamsikia masikioni mwetu, wala minong’ono, kwamba Wssira amezungumza maneno hayo popote, isipokuwa kinywani kwa Bulembo.

Ijapo yapo maandiko ya Dini yanayosema, “Yeye aliye dhaifu wa Imani, mkaribisheni, walakini msimhukumu mawazo yake”. Katika hili, Bulembo lazima tumhukumu, maana amesema Uongo wa dunia;  Na kama bungeni kadanganya; Je atashindwa kuidanya Jumuia ya Wazazi?.

Watu waliosoma enzi ya Unga ulioitwa wa Yanga na Mafuta ya kupikia yenye mikono inayosalimiana toka Marekani, wakati huo kati ya masomo yaliyopendwa pamoja na mengine, ni Somo la Historia, ambalo lilitakiwa usikariri miaka bali uielewe.

Wale waliokariri miaka, waliposahau namba moja tu, kila kitu kiliharibika na walifanya vibaya mtihani wa somo hilo. Hivyo wapo baadhi ya Wabunge wa Bunge Maalum la Katiba, wameingia bungeni humo kwa kukaririshwa vitu; Wanaposahau tarakimu moja ni shida.

Tatizo hilo si kwa Wabunge wa Bunge Maalum tu; Jambo hilo lipo pia hata kwa baadhi ya Wabunge wa Bunge la Muungano, ambao wakiandikiwa Maswali na kukaririshwa, muda wa kujieleza ukifika akakosea sehemu moja tu; Kila kitu kimekwenda Mrama anaanza kujikanyaga.

Upo ugonjwa Sugu ulioenea kama Kirusi kwa baadhi ya Watanzania, ambapo ukitaka kuwadanganya na kuwaibia watanzania, andika kitu chako kwa Maandishi! Watanzania walio wengi ni Wavivu kusoma, na hii ndiyo inayosababisha makosa kama ya akina Bulembo.

Naungana na Jaji Warioba katika kauli yake kwamba; Wajumbe wengi wa Bunge Maalum la Katiba wanaokurupuka na kusema, Warioba na Tume yake hawakufuata Hadidu za Rejea; Hawajasoma Rasimu! kila kitu kimo humo, ila wanakurupuka kwa Shinikizo la kitu kidogo.

Hivi kweli Mjumbe anainuka na kusema, Nani aliyemtuma Warioba na Timu yake akachukue maoni; Je hajui Sheria iliyopitishwa na Bunge ndiyo iliyowasukuma kufanya hivyo? Ndiyo maana Mwalimu Nyerere alisema, Kiongozi wa namna hiyo hatufai akalime Mashamba yake.

Viongozi wa namna hii; Ndiyo wale ambao ukiwapeleka jeshini, akipeleka Mguu wa kushoto mbele anapeleka na Mkono wa kushoto badala ya kupeleka wa Kulia; Na hapo ndipo Rais Jakaya Kikwete anasema, Akili za kuambiwa; Changanya na zako! Je; Bulembo alichanya na zake?

No comments: