Na Bryceson Mathias
NAWEZA kusema bila Uoga; Akili ya Serikali nzima ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa sasa imewekeza kwenye kupambana na Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kwa gharama yoyote bila kujua kuwa mwisho wa siku mateso hayo yanawaumiza wananchi wasio na hatia.
Awali Akili ya serikali nzima ya CCM ilikuwa na itaendelea kuwekeza kwa gharama yoyote kupambana na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA bila kujua au kujihoji vilevile kwamba; Mwisho wa siku anayeumia ni wananchi wake.
Ingawa katika kudhibiti kile ambacho wananchi wanakiita haki, Serikali kupitia mabavu ya vyombo vya dola mara zote; Imeua raia wake wasio na hatia katika mikutano na maandamano halali ya amani, ambapo waliouawa ama kuwekwa vilema si ndugu, jamaa wala watoto wao: Hivyo hawana uchungu!.
Ninachotaka niseme sasa; Ni wananchi kufumbuliwa macho na ufahamu, ili wale waliofiwa na ndugu, Jamaa na Marafiki, nao wawapige wana Siasa uchwara wanaotumika kudhulumu haki na kuhatarisha maisha yao; Kwenye Sanduku la Kura.
Kutokana na adha za Nguvu kubwa za dola zilizofanywa siku zilizopita; Huenda walidhani na kufikiri kwa karibu kuwa labda walijua wamewadhibiti Wanaharakati, CHADEMA na wapinzani kwa ujumla, kumbe hawakujua walikuwa wanaangamiza nguvu kazi ya Taifa.
Kwa Tabia ya Mungu; huwezi ukaangamiza kizazi chote kikapotea kabisa; maana hata katika Hasira yake ya Kuangamiza kwa upotofu wa mwanadamu; Nuhu na Familia yake na baadhi ya Wanyama na Ndege waliokolewa na Gharika.
Ni kweli tumepoteza Ndugu, Familia na Marafiki zetu wengi katika kudai haki; Lakini wale waliosalimika, tangu awali; Walisimamisha tena Koo, zilizoendelea kudai Uhuru na haki zao mahala pengi, huku wakiuwekea Kisogo Uoga hadi waliponyakua haki yao.
Ni rai yangu kwa wapenda haki tofauti na wapenda dhuluma kwamba; Machungu yetu ya kupotelewa na Ndugu, kupewa Vilema vya Kudumu, na kupoteza Rasilimali zetu, yawaelekee Wana Wasio hasa na Uchwara kwenye Sanduku la Kura la Chaguzi za Serikali za Mitaa kwa 2014; Na Uchaguzi Mkuu 2015.
Tukiwachapa Bakora za Kura, Mabomu ya Kura, Maji ya kuwasha ya Kura, Virungu vya Kura, na Kupanda Farasi za Kura tulizopiga kwa umakini; Turudi majumbani kwetu kwa Kishndo na Amani Tele.
Hapo ni lazima Siasa Uchwara na Uongo wa Kauli Mbiu zisizo na Tija: Za Kilimo kwanza, Matokeo Makubwa sasa, wakati watoto wetu wanasomea chini na Dawa hakuna; Utatoweka.
Laa kama hatukufanya hivyo; tutaendelea kuwa na Watoto wanaosoma chini ya Miembe, Wanakaa kwenye Vumbi; Hawapati Uji wala Chakula Shuleni; Wenye Shule zenye Mwalimu mmoja; zisizo na Milango na Madawati; Zahanati zenye Muuguzi bila Mganga; Na Madirisha ya Dawa yasiyokuwa na Dawa.
Aidha ifahamike kwamba; Kodi yetu Walalahoi, itaendelea kukatwa ikichezewa na Walalahai; Bidhaa zitaendelea kuwa na bei kubwa; Wanaodhani wamepata kwa kudanganywa na Ubwabwa, Khanga na Skafu, watakuwa wamepatikana; wote tutaende Soko moja na Duka Moja kwa kichapo kilekile.
Hakuna Mtoto anayezaliwa kwenye Tumbo la Mama asikue; ndiyo maana tulikuwa na Radio za Mbao sasa tuna Runinga; Tulikuwa na Masanduku ya Posta sasa tuna Mitandao; Tulikuwa tunakoroga simu kwa kuomba kwa Opereta sasa tunapiga wenyewe na kadharika.
Huyo anayetaka tubaki na Mawazo ya Mababu ya Adamu na Hawa; Hatutakii Mema; Ashindwe; Akome na Kulegea, maana tunataka mawazo mapya; Ni kweli tulikuwa tunakula kwa Mikono na kutumia Miti; Lakini leo tunataka Vijiko.
No comments:
Post a Comment