Na Bryceson Mathias, Mvomero.
KATIBU wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mvomero, Sadakati Kimati, yuko hatarini kuweka rehani uongozi wake, baada ya kutakatisha nyeti ambapo alitelekeza nyaraka muhimu za Chama hicho Ulevini.
Imedaiwa kwamba; Kutokana na Uzembe wa kutelekeza Nyaraka hizo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero, Wale Kalia, amenekana kutumia Ofisi yake vibaya, akihaha kumnusuru Kimati asikumbwe na Kiboko cha CCM kisimchape, dhidi ya Uzembe aliofanya.
Kalia baada ya kulalamikiwa na Katibu Kimati, amewaandikia Madiwani wawili barua tika kumnusuru huko,
Mtoa habari amedai Kimati akiwa na Madiwani Wawili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ambapo baada ya kupata Vinywaji katika Glosari inayoitwa Pweza - Dakawa, Katibu huyo anadai alitelekeza Nyaraka hizo Muhimu na aliporejea hakuziona.
Katika hali isiyo ya Kawaida, Kalia amewaandikia Barua Kumb. MVDC/C.70/8/3 na Kumb. MVDC/C.70/8/4 za 28/4/2014 Madiwani wa Chadema waliokuwepo eneo hilo la Kinywaji, Joseph Ruanda (Zengwe) na Luka Mwakambaya, akiwataka wajieleze ndani ya siku 14, akiwatuhumu walichukua nyaraka hizo za mikakati.
Imefahamika baadaye kuna Mtu ambaye hajafahamika bado, alimkabidhi nyaraka hizo Kimati akidai ameziokota, na alipozihakiki aliona kama zimerudufiwa kwa nia ya kujipatia kivuli cha nyaraka hizo.
Madiwani hao Zengwe na Mwakambaya (CHADEMA), walipohojiwa na Tanzania Daima kwa nyakati tofauti; Wamekanusha kuhusika na Tuhuma zilizoelekezwa upande wao, na wamekiri kupokea barua hizo na kumjibu Mkurugenzi Kalia kuhusu kutohusika kwao.
Aidha Imedaiwa; Nyaraka hizo zilikuwa na Taarifa ya kumsafisha na kupaka Uzuri wa kazi zenye tija, alizofanya Kada mmoja Mkongwe wa CCM wilayani humo kwa ajili ya kinyang’anyiro cha Ubunge wa Jimbo hilo 2015, ili achuane na Naibu Waziri wa Maji, Amosi Makala.
No comments:
Post a Comment