Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Sunday, April 6, 2014

Tume ya Mabadiliko ya Katiba, isifanywe Makarai ya Zege!

Na Bryceson Mathias

Kama safari tatu sasa nimesema, watanzania wasikubali kufanywa Makarai ya Zege, ambayo hujenga Maghorofa, Makasri, Madaraja na Majumba ya Kifahari lakini mwisho wa siku hutupwa jalalani kama takataka.

SIKU chache baada ya Ikulu ya Rais Jakaya Kikwete kutoa taarifa ya kejeli na kumsuta Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, wananchi walohojiwa kwa nyakati tofauti wamedai, Wajumbe hao wasifanywe Makarai ya Zege.

Karai ni Chombo Muhimu sana cha Ujenzi, ambacho kila mtu mwenye kazi ya Ujenzi hukihitaji kwa unyenyekevu kimsaidie kujenga katika Ujenzi.

Akianze Ujenzi; Karai hubeba Mchanga, Kokoto, Maji, Mawe, Saruji na Mchanganyiko wa Vyote. Hukorogewa Udongo, halioshwi vizuri, hupigwa na Mwiko, na mwisho wa siku hutupwa nje au shimoni kama takataka, huku Makochi na Vitambaa vikifaidi Raha ya Nyumba.

Pamoja na Tume ya Warioba kufanya kazi nzuri ya Kukusanya Maoni ya Watanzania kuhusu Mapendekezo ya Katiba Mpya hadi kukabidhi Rasimu ya pili na kulihutubia Bunge Maalum la Katiba hivi karibuni; Tume hiyo imeanza kufanywa kama Karai la Zege, kazi yake ikisahaulika.

Mara baada ya Jaji Warioba kukabidhi rasmi Ripoti ya Tume na Rasimu ya Katiba kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, Desemba 30, 2014, mbele ya wananchi katika viwanja vya Ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaa, kuna maneno mengi machafu amerushiwa Warioba.

Kama lilivy Karai wakati wa Ujenzi, Tume hiyo ilibembelezwa ikaacha Familia zao, ikaacha kulala Usingizi mnono, wakaacha kufanya kazi zao binafsi ili walitumikie Taifa, walihatarisha maisha kwa kusafiri na vyombo vya Moto; Lakini sasa wamekuwa si Mali Kitu hata Ikulu.

Miongoni mwa maneno machafu aliyoambiwa Warioba ni pamoja na kwamba amemsaliti Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, amekisaliti Chama cha Mapinduzi (CCM), na mara baada ya Hotuba yake Bungeni, yameendelea kusemwa mei kama yeye alikuwa anaamua pekee yake.

Mbali na mengi aliyokashifiwa, hivi karibuni ameambiwa na Ikulu yafuatayo;-,“Toka kumalizika kwa kazi, tangu siku hiyo, Tume haikuwa tena na kazi ya kuandaa Ripoti ama Rasimu kwa sababu kazi hiyo ilikuwa imekwisha na wala isingeweza kuibadili tena Rasimu ya Katiba.

“Kwa maana hiyo, toka Desemba 30, mwaka jana, kupitia miezi ya Januari, Februari mpaka Machi 18, mwaka huu, Sekretariati ilikuwa na muda wa siku 77, zaidi ya miezi miwili na nusu, kufanya maandalizi ya kukabidhi nyaraka na ofisi kwa sababu ilijua kazi yake ilikuwa inamalizika siku ambayo Mwenyekiti wa Tume hiyo angewasilisha Rasimu ya Katiba katika Bunge Maalumu la Katiba.

“Sasa katika muda wote huo, Sekretarieti ya Tume ilikuwa inafanya nini badala ya kuandaa ripoti ya makabidhiano na wakati maofisa wake walikuwa wanaendelea kulipwa mshahara na serikali? Kwa nini walalamike hadharani leo kwa jambo ambalo lilikuwa ni la wajibu wao na wakashindwa kulifanya kwa wakati?” alihoji Msemaji wa Ikulu Salva Rweyemamu.

Hakuna shaka mbele ya Kadamnase ya Watanzania, kuwa wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Warioba, wamefanya kazi nzuri sana na wanastahili pongezi nyingi za wananchi.

Pamoja na lugha ya kejeli iliyotumiwa na serikali dhidi ya Warioba binafsi na kudiriki hata kuniita mnafiki; Je kwa kazi nzuri na ya Uadilifu aliyoifanya, mbali ya kuwa Waziri Mkuu Mstaafu na tena Jaji, hata tu adabu za kijamii anastahiri hayo?.

Je amestahili hayo kwa sababu hakukonga Nyoyo za wanokizana na kilichowasilishwa, au kwa sababu hakuwaridhisha watawala na badala yake Tume yake imekuwa Bega kwa Bega na Matakwa ya Wananchi?.

Ieleweke kwamba, Kejeli zilizotolewa dhidi ya Warioba, hazimuathiri yeye bali zinawaathiri watu wote wenye hekima walioteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kwenye Tume ile.

Tunafahamu walikuwemo Viongozi muhimu wastaafu tena wa kimataifa katika tume ile, walikuwemo Majaji na Viongozi wa Dini humo; Bado sipati picha kama wanastahili kejeli na vituko vinavyosemwa?

Ifahamike pia, Warioba na Tume yake ni Wanadamu kama sisi; Si Mungu, Mitume au Malaika; Ikifika mahali wakachoka kama vile ambavyo wanaowakejeli na kuwasema vibaya wamewachoka na kutowaheshimu; Alaumiwe nani?  Ni rai yangu Ikulu isiwe Kinara wa Kejeli; inajichafua!

No comments: