Na Mwl. Anthony Thomas Gella
KITENDO cha Serikali kupeleka muswaada waSheria ya kulibadilisha bunge la kutunga sheria nakuisimamia Serikali kuwa “Bunge maalumu la katiba”na chama cha Mapinduzi wakiongozwa na Rais waJamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye piaMwenyekiti wa Taifa wa CCM Mhe Jakaya MrishoKikwete si tu kinasababisha vurugu pale bungeni bali piandiyo chanzo cha vurugu zote zinazoonekana palebungeni.
Rais Kikwete pamoja na kumpelekea ushauri, kwakumwandikia waraka wenye kichwa cha habari “RaisKikwete Linda Zama Zako” na waraka huo kupokelewaIkulu tarehe 25/10/2013 saa 4:30 asubuhi na kuandikwakatika gazeti hili makini Toleo Na. 3243 la tarehe2/10/2013.
Katika waraka huo pamoja na mambo mengine,kubwa nililomshauri Rais Kikweteasilitumie/asilibadilishe bunge hili la kutunga sheria nakuisimamia Serikali kuwa “Bunge maalumu la Katiba”.Nilimshauri kuwa bunge hili limekaa kisiasa zaidi kulikouzalendo kwa nchi yao.
Waraka huo pia ulienda mbali zaidi, si tu nilimkatazakulitumia bali pia nilimwelekeza jinsi gani apate “Bungemaalumu la Katiba”. Nilimweleza kwa kuwa Rasimu yaKatiba imepatikana kutokana na maoni ya wananchi nivema na wajumbe wa bunge maalumu la katibawapatikane kutokana na wananchi, kama Rasimuilivyopatikana. Wajumbe hao pia wapatikane kwakuchaguliwa na wananchi bila kupitia vyama vya siasa nawaende kwa kazi moja tu ya kujadili Rasimu kwamanufaa ya wananchi wote. Wajumbe wa aina hiiwasingekwenda na misimamo ya chama kamatunavyoona pale Dodoma kwa kuwa upatikananji wakehaukupitia kwenye chama.
Katika waraka huo pia nilimweleza madhara kadhaaya kulibadilisha “Bunge la kutunga sheria nakuisimamia Serikali” kama ambavyo wakati wa kutungasheria ilivyotokea katika bunge hilo walishindwanampaka wengine wakatoka nje, hiyo ilikuwa sheria mojatu. Tutawaaminije watupendekezee katiba ambayo inazaidi ya ibara 227 pamoja na vifungu vyake?
Mambo yanayoendelea pale Bungeni Dodoma,ukianzia na kupitisha Rasimu za kanuni pamoja namarekebisho ya kanuni hizo ni dalili tosha kuwa kilenilichomtahadharisha Mhe Rais Kikwete katika“Waraka” wangu huo kinajionyesha wazi kuwa hawajamaa wamekaa kiitikadi zaidi, mfano ulio wazi niwajumbe wanatokana na CCM wao wana msimamo wawazi wakiongozwa na msimamo wao (CCM) katika sualala muundo wa muungano wa Serikali mbili ndiyo murua.
Msimamo ambao unapingana kabisa na maoni yawananchi hapo ndio umuhimu wa ushauri wangu niliotoakatika waraka ule unapoonekana. Kama Mhe Rais angeuchukua ushauri wangu, kuwa wajumbe wa Bungemaalumu la Katiba wachaguliwe na wananchi moja kwamoja bila kupitia vyama vya siasa tusingekuwa tunayaonayanayotokea Bungeni Dodoma sasa, badala yake utulivu,amani vingetawala bunge lile na tungepata katibainayopendekezwa mapema kabla siku 70 hazijaisha.
Kwa mwenendo unoonekana pale bungeni kamabaadhi ya wajumbe watalazimisha mambo ambayohayapo kwenye Rasimu yaingie na yaliyo kwenye Rasimuyaondolewe kitendo ambacho kitatafsiriwa na wanateteamawazo/maoni ya wanachi kama kuwadharau,kuwatukana na hata kuwasaliti wananchi waliotoamaoni bunge hili litavunjika.
Wajumbe wa bunge hili maalumu la katiba,wakumbuke pia kuna wakati niliwatahadharisha katikamoja ya makala zangu iliyoandikwa na gazeti hili makiniyenye kichwa cha habari “Bunge maalumu la katibakipimo cha wabunge kuchaguliwa tena 2015”.
Katika makala hiyo niliwatahadharisha wajumbe wabunge hilo ambao pia ni wabunge wa kuchaguliwa,watapimwa na watanzania katika maeneo yao (jimbolake) kama kweli ni mzalendo kwa nchi yao au niwazalendo kwa vyama vyao. Watapimwa jinsiwatakavyokuwa wanachangia ibara mbalimbali za rasimuna jinsi atakavyopigia kura Rasimu ambayo imetokana namoani yao. Ndipo watakupima unafaa kurudi bungeni2015? Wakumbuke pia kupigia kura ya “hapana” ibaraau kifungu kilichotokana na maoni yao watakupima kuwaumewadharau, umewatukana au kuwasaliti na weweujiandae kusalitiwa ukirudi jimboni kwako kuomba kura.
“Nawashauri wajumbe wa bunge maalumu lakatiba, kama mnawapenda wapiga kura wenu namnatamani kurudi mjengoni wekeni mbali itikadi,misimamo ya vyama vyenu mtakapoanza kupitisha ibaraya kwanza hadi ya sita hakikisheni siku ya Alhamisi naIjumaa wiki hii mhakikishe mnaheshimu maoni yawapiga kura wenu kwa kupigia kura ya “ndiyo” ibaraya kwanza na ya sita kwa kufanya hivyo si tu mtakuwasalama majimboni bali pia ni kulifanya bungelisivunjike. Tatizo lenu ninyi siyo ndege wenye rangimoja,na sijui kama mtaruka pamoja”. Na ikitokeandege wenye rangi mchanganyiko wakaruka pamojasi tu mtaandika historia bali pia mtakuwa mmeitufamethali ya ndege wenye rangi moja ndiyo hurukapamoja. Katika kumbukumbu, badala ya methalimpya itazaliwa na kuchukua nafasi yake inayosema“ndege wenye rangi mbalimbali wanaweza kurukapamoja”.
Aidha uamuzi wenu wa kuheshimu maoni yawananchi kwa kupigia kura ya kukubaliana na maoni yawananchi (ndiyo) si tu mtakuwa mmeandika historia yakufuta methali ya ndege wenye rangi moja tu, ndiyowanaruka pamoja bali pia mtakuwa mmemwingiza katikahistoria Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika historiamaalumu yakuwaletea watanzania katiba inayotokana namaoni yao wenyewe.
Kwa kufanya hivyo pia mtakuwa mmenisaidia namimi kuniingiza katika historia kuwa, nilichokisemakatika makala yangu kwenye gazeti hili makini Toleo Na.3204 11/11/2013 yenye kichwa cha habari “Rais Kikweteana dalili za kuingia katika historia”. Nilisema hivyobaada ya Rais Kikwete kunifurahisha kwa kitendo chakecha kuamua watanzania waandike katiba yao wenyewe,kupitia kutoa maoni pamoja na chama chake kupitiawasaidizi wake aliyekuwa Waziri wa Sheria na KatibaSelina Kombani, Mathias Chikawe na MwanasheriaMkuu wa Seriklai wa sasa Fredrick Warema kusemawazi kuwa katiba tuliyo nayo haina matatizo inawafaawatanzania.
“Kama kuna wakati Rais Kikwete alitumia vizuri falsafayake ya “akili za kupewa changanya na zako” ni31/12/2012 alipowatangazia Taifa kuwa watanzaniawaandike Katiba yao wenyewe”. “Kama kuna wakati RaisKikwete amefeli kutumia falsafa yake ya “akili zakupewa changanya na zako” ni wakati wa kulizinduabunge maalumu la Katiba”
Rais Kikwete alianza hotuba yake kwa kutumia akiliyake hadi kushangiliwa si tu bunge hilo hasa IbrahimLipumba na Freeman Mbowe bali pia na watanzaniawote. Alipoanza kutumia akili za kupewa na ndipo baadhiya watu walizima TV zao na kuendelea na majukumumengine pale hotuba ilipokuwa inashangiliwa na upandemmoja (CCM).
“Nawatakia kila la kheri Wabunge wa BungeMaalum la Katiba ili mfanye kile ambacho watanzaniawanakitaka”.
Na Mwl. Anthony Thomas Gella
0656 907751/ agella72@yahoo.com
No comments:
Post a Comment