Na Bryceson Mathias
TAARIFA zinazotolewa na Wenyeviti wa Kamati za Bunge Maalum kwa Wandishi wa Habari wanaonyimwa kuingia kwenye vikao vyao ili wawahabarishe Wananchi, kimsingi zinaonekana kama ni Matapishi au Matangazo yaliyochujwa si habri.
Kutokana na Vigezo na Misingi ya Taarifa kuwa Habari, ni lazima ibebe sifa zake ikiwa ni pamoja na Ukweli na Usahihi, tofauti na inavyofanywa na wenyeviti hao kuwapa wandishi anachotaka, Matangazo au ‘Press Release’, hivyo wandishi sasa hawatoi habari ila Matangazo ya Bunge hilo.
Sababu za Bunge kuonekana linawalisha watanzania matapishi ya Habari, zinatokana na kinachosemwa ni Kanuni ya 77 ya Bunge hilo ambayo haiwaruhusu Waandishi kuingia katika Vikao vya Kamati zake, na kupelekea wandishi waandike matangazo ya vikao hivyo na si Habari.
Wakati watanzania wanataka kuona na kusikia habari sahihi zinazojadiliwa na Wabunge kufikia maridhiano yatakayowapa nafasi ya kupiga kura sahihi ya maoni; Bunge hilo na Kiti, inaonekana vimefikia kukiuka na kuwaingiza Mkenge Viongozi wa Dini waliomo humo.
Maandiko ya Dini yanasema, Mtoto akiomba Samaki huwezi kumpa Nyoka, na akiomba Mkate humpi Jiwe, lakini Wenyeviti hao wanachotoa kwa Wandishi baada ya Majadiliano ya Kamati, si walichokubaliana, ila kinakuwa kimepungua au kuongezwa kwa faida ya Watawala.
Wananchi wakiwa na shauku na Imani ya kupatiwa Katiba ya Matakwa yao, Bunge hilo kupitia wenyeviti, kwa kutumia Kanunu Gandamizi ya 77, sasa inawalisha wananchi kisichokuwepo kwenye Majadiliano yao hali inayowafanya wandishi wawachokonowe walivyo mitaani.
Hapo ndipo ninaposema wananchi wanalishwa matapishi na viongozi wa Dini wakihusishwa na Dhambi ya Uasi dhidi ya wananchi ambao ni Watoto wa Kiroho, wakijikuta wanawalisha Nyoka badala ya Samaki na Mawe badala ya Mikate.
Pasipo sababu ya Msingi Bunge hilo pia, limetengeneza Historia ya kuongeza Sheria Kandamizi ya 18 kwa Wandishi wa Habari wanazozipinga, ambapo imeundwa ya kuwazuia kuingia na kuandika Habari sahihi, wakitishwa, “Chombo kitakachoandika habari zinazokiuka Bunge hilo kitatimuliwa”.
Mbali ya Wenyeviti hao kuwalisha Wananchi Matapishi na Matangazo ya mwenendo wa Mjadala huo, pia limeanza kutengeneza Ubaguzi na Utengano miongoni mwa Vyombo vya habari, ambapo wanatoa upendeleo kwa baadhi ya Vyombo na kuvipa habari na matukio kwa uharaka, na vingine kunyimwa.
Ukweli huo unajidhihisha kwenye Habari na picha zinazojli magazetini na Runinga za kila siku, ambapo vyombo vya vigogo wenye mlengo fulani wa upande mmoja, na vile vya serikali, unakuta vina taarifa na habari zenye msisitizo wa mwelekeo wao, jambo linalowapotosha wananchi ukweli halisi.
Mimi naamini, Wandishi makini waliolishwa Ueledi wa Habari ambao wananchi ni waajiri wao wa kwanza, hawawezi kukubali watanzania walishwe utapiamlo, matapishi na kusomeshwa matangazo, wataingia mitaani kwa Hoja ili Kanuni hiyo ibadilishwe, kama zinavyobadilishwa kanuni zingine.
Ni Imani yangu pia, Vyombo vya Haki za Binadamu na Baraza la Habari Tanzania (MCT) vilivyo mdhibiti wa Bidhaa Feki ya habari nchini, vimebaini habari feki inayotengenezwa na Utawala wa Bunge la Katiba, ambapo Katibu wa Bunge hilo amepewa Meno ya kuwanyamazisha kupitia Kanuni ya 77.
Nilikuwa najiuliza, hivi Wana habari wakiamua kuingia barabarani na mahakani kukataa kuandika habari zilizochujwa na kuwa makapi, matapichi au matangazo yaliyopo bungeni humo na wakaungwa mkono na wananchi alaumiwe nani ?
No comments:
Post a Comment