Kwa mara ya pili mfululizo sasa katika chaguzi ndogo imethibitika pasipo shaka kabisa kwamba CCM inazidi kuporomoka kwa kasi kubwa mbele ya macho ya wananchi na Chadema kupanda, ingawa kwa polepole.
Katika uchaguzi mdogo wa Chalinze Mgombea wa CCm (Riz) amepata kura 20,812 lakini mwaka 2010 mgombea wa chama hicho marehemu Bwanamdogo alipata kura 32,924. huo ni mporomoko mkubwa sana, wa kura zaidi ya 12,000. Ingekuwa mporomoko wa kura 1,000 au 2,000 isingestusha sana.Kwa upande wa Chadema -- chama hiki hakika kimepanda - mwaka 2010 kilipata kura sifuri Chalinze kwa maana hakikuweka mgombea. Lakini safari CDM imeibuka na kura 2,628 na kuipita CUF iliyoambulia kura 473 tu. Mwaka 2010 mgombea wa CUF Kingwala Miraji alipata kura 2,837.Kwa vyovyote vile hongera Chadema kwa kupanda na poleni CCM kwa kuporomoka ingawa mmeshinda kiti. Je huu mporomoko wa CCM ndiyo freefall?
Counterpunch/MwanaHALISI Forum
3 comments:
uchambuzi wako cio wa kisayansi jifunzi kwana statiatic ndio utoe hizo taarifa cikutudanganya hapa nakufariji kwenye hamna.

Post a Comment