Na Bryceson Mathias
Siku zote Tembo alikuwa akipita na Miguu yake iliyo kama kinu ardhini, huku akiwa hajui anapokanyanga chini anaua zaidi ya sisimizi 100.
Kutokana na adha ya kupoteza maisha ya wadudu wenzao, Sizimizi nao siku moja Tembo akiwa amepumzika akiakisi Utawala wake ardhini; Walimpamba kwenye Mkonga wote na kuanza kumgasi na kutembea tembea mwilini mwake.
Usumbufu ule uliumuudhi Tembo na kuanza kuupigiza Mkonga kwenye miti na mawe ili tu aweze kuwatoa, lakini sizimizi wale walisababisha Tembo yule akafa kwa majereha makubwa.
Kero za Muungano na Madhaifu ya Tanzania Zanzibar na Tanzania Bara; zilidharauliwa kutatuliwa kwa sababu za kupuuza au vinginevyo; Hivi sasa zimezaa mnyukano wa kuhitaji ya Serikali Tatu.
1984, kulitokea kilichoitwa “kuchafuka kwa hali ya hewa ya kisiasa Zanzibar”. Msingi wake ilikuwa ni mpango wa baadhi ya viongozi wa Zanzibar kutaka Serikali Tatu.
Ingawa jaribio hili halikufanikiwa, Zanzibar iliruhusiwa kutunga Katiba Mpya mwaka huo huo.
Katika Katiba hiyo, Zanzibar iliondoa madaraka ya sheria zinazotungwa na Bunge kutumika moja kwa moja Zanzibar. Katiba ya Zanzibar iliweka masharti kwamba sheria za muungano zipelekwe kwenye Baraza la Wawakilishi kabla ya kutumika Zanzibar.
1991, Tume ya Jaji Nyalali ilipendekeza muundo wa Serikali Tatu. Ingawa pendekezo hili halikukubalika, Zanzibar iliamua kuwa na bendera na nembo yake na baadaye sharti likawekwa kwamba meli zinazoingia Zanzibar ni lazima zitumie bendera ya taifa yenye nembo ya Zanzibar. Kwa maana nyingine, Zanzibar ikaanza kutumia Bendera ya Taifa iliyo tofauti.
1991, Tume ya Jaji Nyalali ilipendekeza muundo wa Serikali Tatu. Ingawa pendekezo hili halikukubalika, Zanzibar iliamua kuwa na bendera na nembo yake na baadaye sharti likawekwa kwamba meli zinazoingia Zanzibar ni lazima zitumie bendera ya taifa yenye nembo ya Zanzibar. Kwa maana nyingine, Zanzibar ikaanza kutumia Bendera ya Taifa iliyo tofauti.
1992, Zanzibar ilijiunga na Organisation of Islamic Conferece (OIC) na Bunge lilipitisha Azimio la kuzitaka Serikali zote mbili kushirikiana katika kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo na matatizo mengine ya Muungano na kutoa taarifa Bungeni katika kipindi cha mwaka mmoja.
1993, wakati wa Mkutano wa Bajeti, Wabunge kutoka Tanzania Bara (G55) walipeleka Bungeni hoja ya kuundwa kwa Serikali ya Tanganyika. Hoja hiyo ilipitishwa.
Katika kipindi chote hiki, kulikuwa na malalamiko kutoka kila upande. Kwa upande wa Zanzibar baadhi ya malalamiko yalikuwa yafuatayo;
Serikali ya Tanganyika imevaa koti la Serikali ya Muungano ambalo linaisaidia Tanganyika zaidi kuliko Zanzibar. Taswira hiyo imeifanya Tanganyika kuwa ndiyo Tanzania na Watanganyika ndiyo wamekuwa Watanzania; na Wazanzibari wamebaki kuwa Wazanzibari.
Mambo ya Muungano yamekuwa yakizidi kuongezeka na hivyo kuathiri uhuru wa Zanzibar (Autonomy) na kufifisha hadhi ya Zanzibar (Identity);
Kuvunjwa kwa makubaliano ya Hati ya Muungano kwa kuificha sura ya Tanganyika katika Muundo wa Serikali ya Muungano;
Kumuondoa Rais wa Zanzibar kuwa Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano; Kutokuwepo kwa uwazi wa mapato na matumizi ya fedha za Serikali ya Muungano;
Kutokuanzishwa kwa Akaunti ya Fedha ya Pamoja; Kuwepo kwa mkanganyiko wa ugawaji wa mapato na jinsi ya kuchangia gharama za uendeshaji wa shughuli za Muungano baina ya Serikali ya Muungano na Serikali ya Zanzibar;
Kuwepo kwa chumi mbili tofauti zinazoshindana katika nchi moja; Zanzibar kutoshirikishwa kikamilifu na Serikali ya Jamhuri ya Muungano katika masuala ya kupata misaada na mikopo kutoka nje ya nchi;
Zanzibar kulalamika kuwa kuna baadhi ya mambo yamefanywa kuwa ya Muungano kupitia kutungwa kwa sheria na Bunge la Jamhuri ya Muungano kwa mambo yasio ya Muungano na baada ya hapo mambo hayo kupata hadhi ya Muungano;
Kwa upande wa Tanzania Bara, baadhi ya malalamiko
Yalikuwa; Zanzibar imekuwa nchi huru, ina bendera yake, ina wimbo wake wa Taifa, ina Serikali yake na imebadili Katiba yake ili kujitambua kuwa ni nchi;
Zanzibar imebadili masharti ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ambayo inasema sheria za Muungano zinazotungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano zitumike sehemu zote za Muungano, badala yake Katiba ya Zanzibar inaelekeza kuwa ili Sheria itumike Zanzibar ni sharti ipelekwe mbele ya Baraza la Wawakilishi. Maana yake ni kuwa, Katiba ya Zanzibar ipo juu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano;
Zanzibar imetunga sheria kuhusu fedha ambalo ni suala lililo kwenye madaraka ya Muungano;
Zanzibar imetunga Katiba ambayo imechukua madaraka ya Rais yaliyomo katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano yanayoeleza kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano ana madaraka ya kugawa nchi katika maeneo ya kiutawala Mabadiliko ya Kumi ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 yameitambua Zanzibar kuwa ni nchi na yanampatia mamlaka Rais wa Zanzibar kuigawa nchi katika maeneo ya kiutawala;
Masharti ya kikatiba yaliyowekwa na Katiba ya Zanzibar kuhusu mchango wa Zanzibar katika uendeshaji wa Mambo ya Muungano yanapingana na masharti ya Katiba ya Muungano.
Muundo wa Muungano uliopo umepoteza utambulisho wa kihistoria wa Tanganyika na fursa ya watu wa Tanganyika kutetea maslahi yao ndani ya Muungano;
Wananchi wa Tanzania Bara kutokuwa na haki ya kumiliki ardhi Zanzibar wakati wenzao wa upande wa Zanzibar wana haki ya kumiliki ardhi Tanzania Bara;
Wabunge wa Zanzibar huchangia mijadala kwa mambo yasiyo ya Muungano na ambayo kwa uhakika wake ni mambo ya Tanganyika na kwamba Wabunge wa Tanganyika hawana nafasi ya kuchangia katika Baraza la Wawakilishi kwa mambo yasio ya Muungano yanayohusu Zanzibar;
Na kwa mujibu wa Sheria ya Mzanzibari, 1985, Watanzania ambao ni Watanzania wa Bara hutakiwa kutimiza sifa maalum ili kuweza kupata haki za kiraia huko Zanzibar ilhali Mzanzibari huweza kupata haki ya kiraia wakati wowote na popote katika ardhi ya Tanganyika. Haki hizo za kiraia ni pamoja na kugombea uongozi na kupiga kura.
Aidha katika hali tunayokwenda nayo, ni vizuri Chama Tawala na Serikali iliyoko Mmadarakani, ijitathimini issitake kung’ang’aniza mambo wanayotaka wao ili kulinda vitumbua vyao visiingia Mchanga, na badala yake wakubali matakwa ya wananchi, maana kifo cha Tembo kilikuwa kibaya.
Nasema hivyo kwa sababu, Wananchi walioko nje ya Bunge wanaofuatilia Mchakato, na Mapendekezo
No comments:
Post a Comment