Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kinatoa tamko la awali kwa umma kuhusu
ukiukwaji mkubwa wa taratibu, kanuni na sheria zinazosimamia uchaguzi,
zilizofanyika kwenye mchakato wa uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Chalinze,
ambao umehitimishwa Aprili 6, mwaka huu, kwa wapiga kura wa jimbo hili kupiga
kura;
Ukiukwaji
huo ni kama ifuatavyo;
Tume
ya Taifa ya Uchaguzi kuongeza wapiga kura wapya kinyume cha sheriaKinyume
kabisa na Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, kifungu cha 15(5), kinachosema;
“Kwa
madhumuni ya kifungu hiki, Tume itapitia upya daftari la kudumu la taifa la
wapiga kura mara mbili kati ya kipindi kinachoanza mara baada ya uchaguzi mkuu
na tarehe inayofuatia siku ya uteuzi,”
Tume
ya Taifa ya Uchaguzi imekiuka kifungu hiki cha sheria kwa kufanya kile
wanachoita wao ni ‘uhakiki wa mwaka 2014’ wa daftari ambao wanadai lengo lake
lilikuwa ni kupunguza idadi ya wapiga kura waliokufa au kuhama
au kuandikishwa mara mbili, lakini badala ya wapiga kura kupungua, uhakiki huo
uliofanywa na tume bila kushirikisha wala kuwataarifu wananchi wa Jimbo la
Chalinze, umeongeza idadi ya wapiga kura wapya katika jimbo hili kwenye
uchaguzi huu mdogo.
Vile
vile, kutokana na kitendo hicho cha NEC kuongeza idadi ya wapiga kura wapya
kwenye daftari kimesababisha kuongezeka kwa vituo vya kupigia kura tofauti na
ilivyokuwa mwaka 2010, ambapo Jimbo la Chalinze lilikuw ana jumla ya vituo 286
na sasa vimekuwa 288.
Kutangaza
matokeo kinyume cha Sheria ya Taifa ya UchaguziMsimamizi wa Uchaguzi mdogo wa
Chalinze, katika kufanya majumuisho ya kura, alienda kinyume cha Sheria ya
Taifa ya Uchaguzi, kwa kutangaza matokeo ya jumla bila kufanyika majumuisho ya
kituo kimoja baada ya kingine, kama sheria inavyomtaka.
Kitendo
hicho kilikuwa kinyume na Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, kifungu 80(3),
kinachosema;
“Baada
ya taarifa zote za matokeo na masanduku ya kura yaliyo na karatasi za kura za
uchaguzi wa bunge kupokelewa kutoka vituo vya kupigia kura katika jimbo,
Msimamizi wa Uchaguzi, baada ya kuamua uhalali wa kura zozote zenye mgogoro na
kabla ya kujumlisha kura hizo, atatangaza kwa sauti matokeo ya kila kituo cha
kupigia kura katika jimbo kimoja baada ya kingine.”
Badala
yake, Msimamizi wa Uchaguzi alitangaza matokeo ya jumla kwa kila kata, bila
kufanyika kwa majumuisho kama sheria inavyotaka, jambo ambalo linapelekea
matokeo yaliyotangazwa kutokuwa halali kisheria, huku yakitofautiana na matokeo
tuliyonayo kwa mujibu wa fomu za matokeo.
Matumizi
ya rasilimali za umma kuibeba CCM na mgombea wakeTangu mwanzo wa kampeni CCM,
kinyume cha sheria zinazosimamia uchaguzi, wametumia rasilimali za umma
kumfanyia kampeni mgombe wao, kushawishi na kuelekeza wapiga kura.
Kuna
mifano mingi katika suala hili; upo ushahidi unaonesha kuwa Rais Jakaya Kikwete
alikuwa akifika jimboni hapa kwa kutumia magari ya serikali na watumishi wa
umma, ambapo alihusika kufanya kampeni za ‘mtu kwa mtu’.
Makamu
Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar), Ally Mohamed Shein, ambaye alikuja Chalinze
kwenye mkutano wa ufungaji wa kampeni za chama chake huko Miono, naye alitumia
rasilimali za umma, k.m; magari na watumishi (wakiwemo kutoka vyombo vya ulinzi
na usalama), waliokuwa kwenye msafara wake, kufanya kampeni za chama cha siasa,
kushawishi na kuelekeza wapiga kura, kinyume kabisa na sheria na taratibu za
uchaguzi.
Mama
Salma Kikwete ambaye ni kiongozi mwandamizi wa CCM, kwa muda takriban wote wa
kampeni alikuwa akitumia rasilimali za umma kama vile magari (yaliyokuwa na
namba za ikulu) na watumishi, kufanya kampeni za kumnadi mgombea wa chama
chake.
CCM
kufanya kampeni siku ya uchaguziRais Jakaya Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa
CCM, alifanya kampeni siku ya kupiga kura, akiwa kwenye kituo cha kupigia kura,
ambapo alinukuliwa na na kutangaazwa moja kwa moja kupitia vyombo mbalimbali
vya habari, akisema yeye amempigia kura mgombea wa CCM.
Kitendo
hicho cha Rais Kikwete ambacho kililenga kufanya kampeni, kushawishi na
kuelekeza wapiga kura, ni kinyume na Sheria ya Uchaguzi, kifungu cha 104 (1),
ambacho kinasema;
“Hakuna
mtu atakayefanya mkutano siku ya kupiga kura au; ndani ya jengo lolote ambamo
upigaji kura katika uchaguzi unaendelea, au mahali popote ndani ya eneo la mita
200 ya jengo hilo…kuonesha upendeleo au nembo nyingine inayoonesha kuunga mkono
mgombea fulani katika uchaguzi.”
Kifungu
cha 104 (2) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, kinasema;
“Mtu
yeyote atakwenda kinyume na kifungu hiki, atakuwa amefanya kosa…”
Vishawishi
vya rushwa kwa ajili ya kujitoaKinyume na Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, kifungu
cha 91B, ambacho kinasema; “Mtu yeyote atakayemshawishi au kumsababisha mtu
mwingine kujitoa kuwa mgombea katika uchaguzi kwa kupewa malipo, ukuwadi wa
malipo au ahadi ya malipo na mtu yeyote….atakuwa amefanya kosa la rushwa na
iwapo atatiwa hatiani atatumikia kifungo kisichozidi miaka mitano,” mgombea wa
CCM aliwatumia makuwadi wake kumshawishi mgombea wa CHADEMA ajitoe kwa ahadi ya
kupatiwa cheo atakachokuwa tayari, kati ya ukuu wa mkoa au wilaya, mahali
popote nchini.
Imetolewa
leo Bagamoyo, Aprili 7, 2014 na;
John
Mrema
Mkuu wa Operesheni ya Uchaguzi
Mdogo-Chalinz
No comments:
Post a Comment