Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Monday, March 31, 2014

CCM, NEW ZELAND: TAMKO; HAKI YA KUZALIWA

CHAMA CHA MAPINDUZI TAWI LA NEW- ZELAND
83 Grafton Road, Auckland, New -Zeland

YAH: TAMKO KUHUSU HAKI ZA KUZALIWA ZA WATANZANIA ZETU ZA KUZALIWA KAMA WATANZANIAKATIKA KATIBA YA MUUNGANO WA JAMHURI YA TANZANIA

Tawi la CCM New-Zealand, tunapenda kutoa shukrani za kipee kwa Mwenyekiti wa CCM taifa, Mheshimiwa Rais Wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mh. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuonyesha uongozi uliotukuka wa kuitakia Tanzania katiba mpya ambayo itasaidia vizazi vya leo na hata vya kesho. Kadhalika tunatoa shukrani za kipekee kwa Katibu Mkuu Ndg. Ablrahaman Kinana, Katibu wa Uenezi na Itikadi Ndg. Nape Nauye kwa kuwa mstari wa mbele kwa kuliendeleza chama

Uongozi wa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi tawi la New-Zeland, kadhalika tunapenda kuungana na watanzania wenzetu wapenda maendeleo kote duniani kuwapongeza na kuungana na Ndg. John Mashaka pamoja na Ndg. Kadari Singo mwakilishi wa wana Diaspora Katika Bunge La katiba kudai haki zetu za kuzaliwa katika ardhi ya Tanzania. Tawi la CCM New-Zealand Inawapongeza kwa Juhudi zenu za kuipigania Tanzania. Mmeonyesha ukomavu na uongozi wa kweli

Uongozi wa CCM tawi la New-Zealand, tunapenda kuwasilisha maombi ya wana CCM New-zeland kwa bunge maalum la Katiba. Wana CCM New-Zealand  wanaomba watambulike na kupewa haki zao zote kama wazawa wa Tanzania. Tuna imani Chama chetu sikivu, Chama chetu Makini cha CCM kitasimamia mchakato wa kutupa wana New-Zeland na watanzania wengine duniani hii haki ya msingi, ya uraia.

CCM  tawi la New-Zealand, tunapenda kuwahimiza watanzania popote pale walipo duniani kushirikiana nasi katika mapambano ya kudai hii haki ya kuzaliwa ya watanzania. Tuna imani Chama Makini Cha CCM kitaongoza Mchakato wa kuwatambua Watanzania wote duniani
 
Ahsanteni, 

Rajab M. Mrisho Tel: +64 9 356 2160

Mwenyekiti CCM, New-Zealand 

No comments: