Wakuu picha hizi za video na mnato zinaonesha Shule ya Msingi Ikwazu iliyoko Kijiji cha Ikwazu kata anayotokea bwana mkubwa. Hicho kibanda kinachoonekana miti tu ambacho unaweza kukiita jengo ukipenda, kilikuwa ni nyumba ya Mwalimu ambaye amelazimika kuhama baada ya jengo hilo kubakia hivyo lilivyo. Kahamia sehemu moja inaitwa Kimange ambapo kidogo ni centre lakini ili afike shuleni hapo anapaswa kusafiri mwendo wa takriban km 25 kwenye njia mbovu inayohusisha majaruba. Ni katika njia hiyo msafara wa Chadema uliokuwa unakwenda Ikwazu kwenye kampeni za nyumba kwa nyumba, mtu kwa mtu na mkutano wa hadhara ulilazimika kuacha magari na kutembea kwa miguu ili kuweza kufika upande kijijini hapo. Ilikuwa ni baada ya kukwama kweli kweli kwenye zile njia/majaruba. Picha zingine zinaonesha madarasa na majengo ya shule hiyo ambayo ina madarasa saba mwalimu mmoja. Picha zingine zinaonesha mandhari ya kijiji chenyewe cha Ikwazu. Needlessly to say...one could witness the highest level of poverty.
Kwa mazingira haya ambayo yanawakilisha maeneo mengi nchini, CCM na Kikwete walipaswa kuwa positive na kukubaliana na wazo la Dokta Slaa juu ya sera ya kuboresha makazi kwa wananchi kwa kupunguza au kuondoa kodi kwenye bidhaa za ujenzi km nondo, mabati, saruji na mbao ili wananchi wamudu kujenga makazi bora. Mtakumbuka wakati ule Dokta Slaa alisema kwa standard za kimataifa, makazi duni ni dalili za nchi kuwa na umaskini. Wananchi katika maeneo hayo wamehoji inakuwaje Mwenyekiti wa CCM anaweza kupata ujasiri wa kutumia mamilioni kujenga jengo la kuchezea ngoma lakini ameshindwa kusaidia watoto kupata mazingira ya kupata elimu bora au wananchi kupata makazi bora. Wanahoji CCM wanapata wapi ujasiri wa kuja kuomba kura tena kwa kumtanguliza mgombea asiyejua wananchi hao wanaishi na kuvumilia matatizo gani, maana maisha yao na yake ni mbingu na ardhi.
Juu na chino ni madarasa kwenye jimbo ambalo Mh. Jakaya Kikwete alikuwa Rais kwa miaka kumi na tano. Mwanae Ridhiwani Kikwete anataka kuendeleza umasikini huh
No comments:
Post a Comment