RAIS Jakaya
Kikwete ametakiwa kuwashauri wabunge kuboresha rasimu ya pili ya Katiba
inayokwenda kujadiliwa hivi karibuni katika Bunge la Katiba, mjini Dodoma
badala ya kuijadili kwa masilahi ya vyama vyao. Ushauri huo
ulitolewa jijini Dar es Salaam jana na mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba,
Profesa Mwesiga Baregu, alipozungumza na waandishi wa habari katika kongamano
la Katiba ambalo lilijumuisha watu kutoka asasi mbalimbali. “Kuna kazi
kubwa ya kuipitia rasimu hiyo na kuirekebisha na tuache mambo ya serikali mbili
au tatu, kwani hiyo ni kupotosha maana nzima ya Katiba wakati Tume ya
Mabadiliko ya Katiba imefanya kazi katika mazingira magumu,” alisema.
Aidha,
alisema anatumaini Watanzania watafika mahali watazungumzia mambo muhimu ya
nchi kuliko kuzungumzia mambo ya kutaka vyeo. Mkurugenzi Mtendaji wa
Taasisi ya Maendeleo ya Tanzania (TAPID), John Malya, alisema Katiba
itakayojadiliwa iwe ni ya manufaa kwa Watanzania na yenye kuleta muafaka kwa
taifa kwa ujumla.
Tanzania Daima
No comments:
Post a Comment