Na Tumain makene
Nimelazimika
kukatisha safari baada ya kusikia taarifa za CCM kuanza kutekeleza agizo
alilolitoa Nape Nnauye leo mjini Mwanza kwamba Green Guard waanze kufanya kazi
yao. Kweli wameanza. Muda mfupi
uliopita, Mwandishi wa Habari Christopher Maregesi amepewa kipigo kikali na
CCM, huko Bunda. Ilikuwa ni baada ya kitu kinachodaiwa au kuonekana kuwa
nimtego kumnasa, kisha watu wa Green Guard, wanaopewa mafunzo kwenye makambi ya
CCM yanayoanzishwa kila wakati wa uchaguzi, wakafanya kazi yao.
Taarifa
zinasema, waandishi wa habari waliitwa kwenda Ofisi ya CCM ambako eti ilikuwa
watoe taarifa kwa vyombo vya habari. Hakukuwa na taarifa yoyote wala kitu cha
namna hiyo. Mara baadhi ya waandishi wakaanza kuondoka mmoja baada ya mwingine.
Mmoja wa waandishi aliyeondoka ni kiongozi wa CCM. Akabakia Maregesi peke yake.
Watu wa CCM wakatekeleza maagizo ya kiongozi wao. Wakamshushia kipigo. Baada ya
kipigo, wamempeleka kituo cha polisi ambako hawajafungua kesi yoyote. This is
very sad and unbecoming.
Kitendo hiki
kimetokea muda mfupi baada ya Nape Nnauye kutoa kauli akiwa mjini Mwanza
kuwataka Green Guard, lile jeshi la CCM, waanze kazi. Taarifa zilizopo ni
kwamba baada ya press conference kiongozi huyo wa CCM aliekea Bunda. Huko
alikopigwa mwandishi. Baada ya tukio Nape amekimbilia Mwanza. Wakati Nape
anakimbilia Mwanza baada ya tukio hilo, Waziri Wassira ameonekana
kuchanganyikiwa. Alipotafutwa na waandishi amesikika akisema kuwa majukwaani
CCM wanajitahidi kuwarubuni wananchi kuwa wanaopiga watu ni CHADEMA, punde
inadhihirika kinyume chake. Kumbe CCM ndiyo wanafanya vitendo hivyo. Yeye
anadaiwa kusema kuwa hiyo ni aibu.
Tunamwambia
Wassira hiyo si aibu. Ni dhambi. Umwagaji wa damu wanaoufanya kulazimisha
ushindi au kuwatisha wapiga kura, kisha wanatumia ngao ya vyombo vya dola
kulinda uhalifu wao dhidi ya Watanzania wanaowakataa, itawawinda na kuwaondoa
madarakani. Pamoja na kuwa
msibani, nimefuatilia kwa ukaribu sana press conference ya Nape Mwanza. Amechochea
kuni za kutosha. Tukio hilo la Bunda jioni hii limedhihirisha nilichowaambia
baadhi ya waandishi walionipigia simu kutaka ufafanuzi wa upande wa pili.
Chama gani
kinaweza kufanya vitendo vya ugaidi zaidi ya kile kinachoweka vijana makambini,
wakifundishwa matumizi ya silaha, mafunzo ya kijeshi, wakifundishwa namna ya
kupiga, kuteka, kutesa na hata kuua? Nikawaambia,
hakuna waandishi wenye uzoefu na unyama wa CCM kama walioko Kanda ya Ziwa.
Nikawakumbusha vitu vitatu. Kwanza tukio la
kuvamiwa, kukatwa mapanga na mashoka wabunge wa CHADEMA, Kiwia na Machemli.
Kazi iliyofanywa na vijana wa CCM wanaojulikana kwa sura na majina, mbele ya
askari polisi wenye silaha. Si tu kwamba polisi hao hawakuzuia uhalifu wala
kuwakamata wahalifu, hadi leo hakuna hatua imechukuliwa dhidi ya watu hao. Kama
ni ugaidi unataka zaidi ya huo?
Nikawakumbusha
namna ambavyo Green Guards waliwahi kumshushia kipigo cha mbwa mwizi mmoja wa
waandishi wa habari, tena mbele ya umati wa watu waliohudhuria mkutano wa
hadhara wa kampeni za mgombea wa chama hicho, ambaye leo ni mbunge, Ndugu
Ndassa. Tatu,
nimekumbusha kwamba wao wanajua vizuri kuliko hata sie wengine kwamba kama kuna
mahali CCM wanafanya siasa za kihuni, completley thug politics ni Kanda ya
Ziwa. Jiko lake liko Mwanza. Zinapikwa kweli kweli. Matokeo yake ndiyo hayo
yaliyodhihirika tena leo kwa maagizo ya kiongozi mwandamizi wa CCM.
Imekuwa kawaida
sasa kwa CCM kuweka vijana wao kwenye makambi kila kinapokuwa na uchaguzi.
Wanawapatia mafunzo ya kijeshi, ikiwemo matumizi ya silaha, mbinu za kupiga,
kuteka, kutesana hata kuua. Taarifa hizi Jeshi la Polisi linazo. Zimeripotiwa
kwao na viongozi wa CHADEMA karibu kila uchaguzi. Dhahiri imekuwa wakati wa
chaguzi ndogo; Taja zote;
kuanzia Tarime, Biharamulo, Busanda, Kiteto, Igunga, Arumeru, zote. Wanaowekwa
makambini hutumika mahali ambapo CCM inaona kuna ukinzani mkubwa na ushindi
haupo. Wanaweza kutembea na silaha kama mapanga, wakionesha shari hadharani
kabisa.
Katika uchaguzi
huu utakaofanyika keshokutwa, moja ya makambi hayo lilikuwa huko Mbarali,
Mbeya. Tayari wamefanya kazi yao huko. Wamepiga na kujeruhi watu vibaya kwenye
kata inayofanya uchaguzi, Njombe mjini.Mmoja amevunjika taya. Taarifa za
uwepo wa kambi hiyo zilitolewa mapema kwa polisi mkoani Mbeya. Maana awali
walipanga wafanye fujo kwenye mkutano wa Dt. Slaa alipofika Chimala kwenye
M4C-OPD. Mpango ukashindikana baada ya taarifa kunaswa na CHADEMA. Ilitarajiwa
kuwa polisi wangechukua hatua ya kuzuia na kuwakamata! Si hivyo ilivyotokea.
Sasa matokeo ya
mafunzo ya makambini yameendelea kudhihirika leo, tena kwa amri iliyotolewa
hadharani kweupe. Kama ilivyodhihirika Igunga kw akifo cha Mbwana Masoud. Mfano
mmoja kati ya mingi ya 'kazi' za vijana wanaowekwa makambini kwa kazi maalum. Kitu
alichokifanya leo Nape ni kile ambacho wamekuwa wakiagiza kwa maficho usiku.
Polisi wanataka ushahidi zaidi upi? Uchaguzi wa
kata 27 unaoendelea nchini utakaohitimishwa Jumapili kwa upigaji w akura ni
JARIBIO la kwanza la aina yake kwa IGP Ernest Mangu, kwamba chini ya uongozi
wake mpya, tunaweza kuwa na jeshi lisilotumika kubeba chama fulani ambacho kwa
sababu ya kuishiwa ushawishi na kukataliwa na watu, kinatumia mbinu hizo za
msituni.
IGP Mangu
tunataka kuona Jeshi la Polisi linalofanya kazi yake ipasavyo likifuata weledi
na maadili, likizingatia sheria kwa ajili ya kutenda haki, si kukimbia
kutekeleza maelekezo ya kisiasa ya wanasiasa walioko madarakani leo, kwa
manufaa ya kisiasa ya CCM. Tunataka kuona
chini yake, CCM kama wanavyofanya Arusha mjini na mahali pengine, hawatumii
tena majambazi kupiga watu. Tunataka kuona dismantling ya hizo kambi na vijana
hao wakifikishwa mahali panapowastahili, badala ya polisi kuwageuzia kibao
viongozi, wabunge, wanachama, wafuasi na wapenzi wa CHADEMA, wakati watendaji
wa matukio wakiachwa kutamba mitaani.
Hakuna Jeshi la
Polisi linaweza kujijengea imani kwa wananchi iwapo double standards za wazi
kabisa zitaendelea kama inavyofanyika hivi sasa, kwa makusudi ya kushughulikia CHADEMA
au wananchi wanaopinga CCM! IGP Mangu this
is the test...matukio yaliyotokea au yanayotokea katika uchaguzi huu wa marudio
katika kata 27, yataonesha Watanzania pasi na shaka mwelekeo wa jeshi unalotaka
kuliongoza huko tunakokwenda hasa katika kukabiliana na changamoto za kisiasa
zinazohusisha matukio ya kikatili na kinyama kama yanayofanywa na Green Guards,
kwa usimamizi wa walioko madarakani, huku polisi wako wakionekana 'kushikwa'
mikono katika kuchukua hatua stahili. Zaidi ya hapo,
yatawaonesha Watanzania utakuwa IGP wa namna gani katika hali ambayo ni dhahiri
kuwa CCM iko ukingoni na anguko lake ni wazi mno, tena kupitia sanduku la kura.
Tumain Makene
No comments:
Post a Comment