Baada ya kupokea message na wito mbali mbali kuhusu haja ya
kutoa ufafanuzi kuhusu yaliyojiri katika Shauri la Zitto Zuberi Kabwe Vs Baraza
la Wadhamini,CHADEMA na Katibu Mkuu CHADEMA.
Shauri limefunguliwa likiwa na sehemu Kuu mbili,Shauri ama Case
ya Msingi,na maombi madogo ya Zuio la muda.
Katika Shauri Kuu Muombaji anaiomba Mahakama Kuu kwa amri
tatu;
1.Chadema izuiwe kujadili suala la uanachama wake mpaka pale Atapopewa
nakala za mwenendo na uamuzi wa Kamati Kuu kumvua nafasi za Uongozi,na Rufaa
yake dhidi ya Uamuzi huo kusikilizwa na Kamati Kuu ya Chadema.
2.Chadema
iamuriwe kuitisha Baraza Kuu ili kujadili Rufaa hiyo.
Msingi wa Madai ni kwamba wakati mchakato wa Rufaa
haujakamilika,na wakati haja pewa nakala za mwenendo na uamuzi wa kumvua nafasi
za Uongozi,ameitwa na Kamati Kuu kujadiliwa kuhusu Uanachama wake.
Katika Shauri dogo lililotolewa uamuzi Jana,Muombaji aliomba
amri ya Zuio ili Kamati Kuu au Chombo kingine cha Chadema isijadili Uanachama
wake mpaka Shauri la msingi litakaposikilizwa,na kutolewa Uamuzi na Mahakama
Kuu.
Shauri lilifunguliwa tarehe 2/1/2014,na siku hiyo hiyo Mimi na
Wakili Tundu Lissu tulitoa mapingamizi Matatu dhidi ya Maombi;1.vifungu vya
Sheria vilivyotika havikuwa sawa. 2.hati ya kiapo Ina mapungufu.3.mahakama haina
mamlaka kujadili migogoro ya vyama vya siasa,na taasisi zenye Tabia ya uhiari.
Mahakama ilikataa mapingamizi yote Matatu katika uamuzi wake wa
tarehe hiyo 2/1/2014,uliosomwa Saa 12 hivi za jioni.
Pande zote tukabaliana kwamba maombi madogo yasikilizwe tarehe
3/1/2014,na kwamba wadaiwa Walete hati ya kiapo kinzani Saa 2.30 asubuhi ya
tarehe 3/1/2014 ili Saa 3 asubuhi hiyo tusikilizwe maombi Yale madogo
niliyotaja hapo juu.
Mimi Kama Wakili nikala kiapo na kutoa hati ya kiapo kinzani
kwani kwa mazingira Yale ya uharaka isingekuwa rahisi kuwapata wadhamini wa
chama ili watoe hati ya kiapo usiku au asubuhi mapema na kuwahi Mahakama.
Cha msingi zaidi ni kwamba Mawakili tumepewa na Chana mamlaka
kamili kuhusiana na Shauri.
Wakati wa usikilizaji Mahakama yenyewe (suo mottu) ikazitaka
pande zote ziieleze Mahakama Kuu iwapo ni sahihi Wakili kila kiapo kwa niaba ya
mteja katika Shauri Kama lile.
Pande zote ziliieza Mahakama kwamba ni sahihi,ingawa Wakili
Msando alipinga aya ya nne ya hati ya kiapo kwa sababu za kisheria.
Kisha tukajadili maombi yenyewe. Hoja zetu zikawa kwamba
Muombaji amepewa nafasi ya kusikilizwa kwa kuitwa Kamati Kuu,pia tukasisitiza
Mahakama haina mamlaka ya kuingilia mambo ya ndani ya taasisi Kama Vyama vya
siasa.
Katika uamuzi wake wa tarehe 7/1/2014 Mahakama imeamua kwamba
pamoja na pande zote kukubaliana kwamba ni sahihi Wakili kula kiapo kwa niaba
ya mteja anayemuwakilisha Mahakamani katika mazingizira ya Shauri lile,haikuwa
sahihi.
Ilikubaliana pia na Wakili Msando kwamba aya ya nne Ina taarifa
ambazo ilitakiwa zitolewe na mtu aliyekuwa katika Kikao cha Kamati Kuu,na si
Wakili.
Ikaamua kukifuta kiapo.
Mahakama ikaamua pia kwamba mleta Maombi anastahili Zuio la muda
ili suala la Uanachama wake lisijadiliwe mpaka Case ya msingi itaposikilizwa na
kutolewa uamuzi.
Case ya msingi inaendelea,na Chadema kupitia sisi mawakili wake
inaandaa utetezi ambao kwa mujibu wa Sheria unatakiwa Mahakama ifikapo tarehe
23/1/2014.
Kuhusu suala la mwenendo wa Kikao cha Kamati Kuu na kuitisha
Baraza Kuu,Chama kitazungumza kwa namna na muda itaoona unafaa.’’
Peter Kibatala,
Wakili na Mkurugenzi wa Sheria,Katiba na Haki za
Binadamu;CHADEMA.
No comments:
Post a Comment