Kutekwa na kuteswa Mwenyekiti wa Temeke; Mpango
mzima wa kuihusisha CHADEMA huu hapa;
Jana majira ya saa 3.30 asubuhi, watu wapatao
watano ambao ni wanachama wa CHADEMA mamluki wa Timu ya Zitto na CCM, wakiwa
eneo moja la ofisi ya umma wakisubiri huduma ya muhimu sana, walipokea simu ya
taarifa kuwa Mwenyekiti wao wa chama wilaya ya Temeke, Josephat Yona Patrick
alikuwa amekutwa mahali fulani Dar es Salaam baada ya kutekwa, kuteswa na
kuumizwa na watu wasiojulikana.
Wale watu mara tu baada ya kupokea habari hizo,
wakamtafuta mtu waliyekuwa wakimwita kwenye simu jina la Mchange (wala si
mwingine ni Mhange huyo huyo anayefahamika katika masuala hayaya circles za
usaliti dhidi ya CHADEMA).
Wakamwambia habari hiyo (inavyoonekana yeye alikuwa
tayari anaijua na alikuwa mahali fulani kwa mwanasheria). Akawauliza wanaweza
kumtaja mtu (a watu) yeyote wanayetaka ahusishwe kwenye tukio hilo kisha
afunguliwe kesi. Mtu ambaye akihusishwa itakuwa rahisi kwa viongozi wakuu wa
chama na hatimaye chama kizima kuhusishwa kwenye tukio hilo.
Wale watu wakamwambia ili kumalizana na ‘biashara’
ya CHADEMA kabisa kwa kuwahusisha viongozi na hatimaye chama kizima katika
tukio hilo ambalo linaweza kukuzwa na kuoneshwa kuwa ni UGAIDI, wako tayari
kumtajia majina ya watu wawili ambao wamekuwa wakikihami na kukitetea sana
CHADEMA Temeke, hivyo ni kikwazo kwa mikakati yao ya kukihujumu CHADEMA katika
eneo hilo.
Kama inavyojulikana kwa upande wa Dar es Salaam,
mikakati ya kuihujumu CHADEMA imekuwa ikifanyika kwa kiasi kikubwa sana Temeke.
Wale watu wakamtajia huyo mtu waliyekuwa wakimtaja
kwa jina la Mchange, majina ya watu wawili, Mzee Salum Zinga na Bernard
Mwakyembe. Wote hawa ni makamanda kweli kweli hapo Temeke, kiasi kwamba
Mwenyekiti wa sasa wa CHADEMA Wilaya ya Temeke amekuwa akimhofia sana Mwakyembe
kwamba anaweza kuchukua nafasi yake wakati wa uchaguzi ujao wa ndani ya chama hicho.
Baada ya kumtajia majina hayo, wakamwambia
wanapitia ofisi ya wilaya ya chama hicho mara moja, kisha wakutane kituo cha
polisi ili wakafungue malalamiko dhidi ya watu hao wawili kuwa wamehusika na
tukio la kutekwa, kuteswa na kuumizwa kwa mwenyekiti huyo. Mpango mzima ukawa
umekamilika na ukatekelezwa.
Tunavyozungumza hapa sasa tayari Mzee Salum Zinga
ambaye ni Mwenyekiti wa Wazee Jimbo la Temeke ameshakamatwa na polisi na sasa
jeshi hilo linamtafuta Mwakyembe. Lakini kwa namna ambavyo mpango huo umepangwa
na utakavyotekelezwa, lengo ni kuwafikia viongozi wa juu.
Mpango huo uliozungumzwa na watu hao watano pale
Temeke kwa kuwasiliana na Mchange ndiyo msingi wa kauli za Kamanda wa Polisi
Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleman Kova, kutamka kwa kuihusisha CHADEMA
huku akijigamba kuwa watamkamata mtu yeyote bila kujali cheo chake. Akilenga
viongozi wakubwa wa chama hicho.
Huyo Kova ambaye kwa sababu ameshajitambulisha kuwa
ni bingwa wa kugeuza matukio haya ya ukatili kuwa ni ‘filamu’ ya kuficha ukweli
na kuanza kusaka uongo, hatuna haja ya kumjadili zaidi ya hapo. Ila ajue tu
kuwa mpango mzima unajulikana.
Ndiyo maana sehemu ya mpango huo ni kumlazimisha
Yona arudi na kulazwa Moi ambako alikuwa ameagwa jana hiyo hiyo baada ya
kubainika hana majeraha makubwa na angetakiwa kurudi baada ya wiki mbili. Hiyo
ilikuwa ni baada ya CHADEMA kuwa wamesimamia matibabu yake, ikiwemo kumlipia
gharama za hospitali na usafiri kumpeleka nyumbani.
Akiwa hapo hospitalini amezungumza na vyombo vya
habari kwa namna tofauti tofauti, kwa mtazamo wa kila chombo na kadri ya
maelekezo…
Mpango mzima unaandaliwa pia kupitia vyombo vya
habari;
Angalia kutoka magazetini
Kama mlivyoona leo kwenye kurasa za mbele za
magazeti yote yaliyotoka leo, habari hii imepewa uzito mkubwa, ingawa kwa namna
tofauti tofauti, kulingana na uwezo, sera za vyombo vya habari na MALENGO ya
chombo husika, hasa katika kufanya kazi za watawala dhidi ya CHADEMA.
Lengo lingine ni kubeba agenda za makundi ya
kuwania urais ndani ya CCM, ambayo CHADEMA ndiyo tishio pekee la wao kufanikiwa
kwenda ikulu, hivyo yanafanya kila jitihada kukiumiza chama hicho kwa
propaganda nyepesi kama ya tukio hilo.
Kwa upande wako fanyia kazi PICHA zilizotumika leo
katika magazeti yote. Zimepigwa wakati gani? Eneo gani? Saa ngapi huyo mpiga
picha maalum alikuwa ameandaliwa kwa ajili ya kupiga hizo picha zinazooenakaana
kupigwa kwa ustadi na kifaa kizuri? Kuna maswali mengi sana ukizingatia kuwa
picha zilizotumika katika habari hiyo ni za aina moja! Nani kazipiga?
Hapa tunaweza kujadili habari kutoka katika
magazeti kadhaa;
Mtanzania
Gazeti hili limeipatia habari hii kichwa
kisemacho INATISHA.Ndani ya habari gazeti hilo kwa malengo
linalojua yenyewe, labda likiongozwa na kile kinachoweza kuitwa aina ya weledi
wa aina yake wa taaluma ya habari, sera za chombo hicho na malengo ya wamiliki,
limewahusisha viongozi wa CHADEMA katika tukio hilo kwa hali ambayo inaacha
maswali mengi sana.
Mathalani kwenye moja ya nukuu zake,
wamemnukuu Yona akisema
“Bernard na Mwakyembe walinisalimia na kuondoka,
baada ya hapo, wakaja watu wengine wane ambao siwajui, wakajitambulisha kwangu
kuwa ni polisi wanatoka kituo cha kati, hivyo basi wananihitaji kwa ajili ya
mahojiano.”
Waandishi wa gazeti hili wangekuwa na nia ya
kufanya uandishi unaowajibika kwa jamii, wangefanya kazi yao kidogo tu
wangebaini kuwa Yona katika hilo alikuwa amewadanganya au amewaambia kitu
ambacho kinahitaji kufanyiwa kazi zaidi.
Kwa sababu kama umefuatilia mtiririko wa taarifa
hii, kuna mtu anaitwa Bernard Mwakyembe (mtu mmoja), lakini hapa Yona ametaja
kwamba hao ni watu wawili tofauti. Gazeti lilipaswa kufanya kazi yake badala ya
kutumika kuwa karatasi ya kufanyia propaganda za CCM dhidi ya CHADEMA.
Katika aya mbili zinazofuata ndiyo zinaliacha
gazeti hilo uchi kabisa kwamba limeamua kutumika kwenye mkakati unaoandaliwa na
CCM kupitia vyombo vya dola. Limeandika hivi;
“Tulibishana sana tena ni muda mrefu, mwisho
nikawaambia wanionyeshe kibali cha kunikamata lakini walinijibu kuwa wao ni
polisi, napaswa kutii amri kama kuna mahojiano zaidi yatafanyika kituoni,
nikapanda gari lao na kuondoka,” alisema Patrick.
Soma na aya inayofuata ambayo gazeti hilo
limeandika kama vile lilikuwepo wakati tukio linatokea. Kwa sababu lilipaswa
kuandika maneno ya Yona ni madai…allegations.
“Alipohoji sababu ya watu hao kujitambulisha ni
polisi wakati anawajua kuwa si wanausalama, walianza kumshurutisha kuingia
ndani ya gari alipogoma walimsukuma kwa nguvu ndani ya gari hilo na kumwambia
kuwa wanampeleka kituo cha kati.”
Aya hizo mbili zilitosha kabisa kuwashtua waandishi
au wahariri makini kuwa chanzo cha habari wanachozungumza nacho si cha
kuaminika au kinazua maswali mengi mno.
Mtu aliyesema dakika kadhaa tu zilizopita kuwa
walikuja watu wengine wanne hawajui, wanajitambulisha kuwa ni polisi, akawahoji
vitambulisho, wakashindwa kutoa, akabishana nao sana maeneo ya baa (hakuna mtu
aliyesikia?), cha ajabu akakubali kuondoka nao wakati yeye hawajui ni akina
nani, ghafla tena anasema kuwa anawajua kuwa si wanausalama. Kuna maswali mengi
sana?!
Kwa ujumla habari nzima ya Mtanzania kuhusu tukio
hili, ilistahili kuandikwa na yale magazeti ‘crap’ ya ajabu ajabu yaliyoko
mtaani, chini ya waandishi na wahariri ambao hawajui wala hawathamini chembe
hata moja ya maadili achilia mbali weledi wa kitaaluma.
Wameandika habari ile badala ya kutumia madai ya
nafsi ya tatu umoja, wao wameandika kama vile walikuwepo hatua kwa hatua na
mlalamikaji Yona, lengo zima ikiwa ni kuwahusisha viongozi wa CHADEMA na chama
hicho katika sakata zima. Je Mtanzania maslahi yao katika hili ni yapi? Bila
shaka ni makubwa sana.
Angalia aya hizi zilivyoandikwa kwa makusudi,
kimkakati;
Patrick ambaye ni rafiki wa karibu na aliyekuwa
Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Zitto alisema kuwa mgogoro wake na viongozi wakuu
wa chama hicho ulianza tangu alipoitisha mkutano na waandishi wa habari wa
kuitaka Kamati Kuu ya chama hicho kuitisha mkutano wa kujadili suala la kina
Zitto, Samson Mwigamba na Dk. Kitila Mkumbo.
“Niliitisha mkutano ule ili kuwaambia viongozi wa
CHADEMA kujadili suala la kina Zitto, Kitila na Mwigamba ndani ya chama na si
kuwavua uanachama kama ilivyojitokeza jambo ambalo lilipingwa na viongozi wa
chama hicho,” alisema Patrick.
Alisema, kutokana na hali hiyo viongozi wa chama
hicho akiwemo Mwenyekiti wake Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dk. Willibrod Slaa
alimwita na kumuambia aache urafiki na Zitto la sivyo watamfukuza
uanachama. (Walimwita lini, wapi kwa namna gani, hivi kweli viongozi wa
juu namna hiyo wanaweza kumwita kiongozi wa wilaya hivi hivi tu, hicho chama si
CHADEMA labda CHAUMA na viongozi hao hawawezi kuwa Mbowe wala Slaa, lakini
kibaya kabisa, gazeti wala halikuwatafuta kutaka kujua upande wao na kupata
hata ukweli. Uandishi wa hatari sana huu)
“Waliniita na kuniambia niachane na Zitto,
nilipinga ndipo waliponiambia nijiondoe ndani ya chama hicho, niliendelea
kupinga,” alisema.
Alisema kutokana na hali hiyo, viongozi hao
walimwambia aitishe mkutano wa Kamati ya Utendaji ya Wilaya na kuwaambia
wajumbe wa kamati kuwa yeye si rafiki wa Zitto na kwamba hawezi kumuunga mkono
kwenye harakati zake, lakini aliendelea kukataa suala hilo. (Hivi gazeti
makini linaweza kunukuu uongo kama huu na kusema limeandika habari kwa ajili ya
watu kusoma. Kuna tofauti gani na magazeti ya Yule jamaa mtunga hadithi).
“Tangu nilipoitisha mkutano wa waandishi wa habari
wa kupinga uamuzi wa kuwavua uanachama akina Zitto, Mwigamba na Kitila,
nimekuwa kwenye mvutano mkubwa na viongozi wangu wa juu, nimepokea vitisho
vingi ambavyo nilivirekodi kwenye simu yangu ya mkononi waliyoichukua,” alisema
Patrick.
(Kwa trend ambayo chanzo hicho kimeonesha
tanguy huko juu, huna haja ya kwenda hata darasa moja kujua kuwa huu ni uongo
mkubwa unaosemwa na mtu anayejifunza kuzalisha fitna na majungu, lakini pia
mwanafunzi wa kutengeneza mgogoro, lakini kikubwa kupika kesi. Mathalani
mhariri makini hawezi kupitisha uchafu kama huu uwe habari, angeuliza tu, huyo
Yona alifanya huo mkutano lini?, Ulihusu nini? Je ni kweli ulihusu kupinga
kuwavua uanachama watu hao? Kwa nini kutumika kuandika uongo?).
Aliongeza, suala hilo liliendelea hadi Dk. Slaa na
Mbowe walipomwita na kumlazimisha aitishe tena kikao kingine cha kamati tendaji
ili atangaze kujiuzulu mwenyewe nafasi yake kabla ya kumfukuza uanachama, jambo
ambalo alilipinga tena.(Umakini wa waandishi na wahariri wa gazeti hilo
haukuwatuma kuona umuhimu wa kuwatafuta viongozi hao walau wahalalishe huo
uchafu walioamua kuuita ni habari ya kuwapelekea Watanzania. Hii ni hatari
sana.)
“Dk. Slaa aliniandikia barua ya kunitaka niitishe
mkutano nilipoona kelele zinazidi nikaamua kuitisha lakini wajumbe wa kikao
nilichoitisha kwa pamoja wakaniunga mkono na kusema wana imani na mimi, hivyo
basi hawataki niondoke.
“Baada ya hapo, Dk. Slaa akaniandikia barua na
kuniambia kuwa kikao nilichoitisha ni batili na kwamba wanatakiwa
kuitisha kuitisha kikao kingine Januari 10 mwaka huu.”
Kwa ujumla habari nzima ya Mtanzania ni crap. Na
kuonesha dhahiri malengo na nia ovu waliyonayo dhidi ya CHADEMA kupitia tukio
hilo la kusikitisha la kutekwa na kuteswa kwa Yona, gazeti hili ambalo
limeandika mengi sana ya KUUMIZA, yanayokiuka maadili na weledi wa uandishi,
likimnukuu mwenyekiti huyo akisema uongo dhidi ya Mbowe na Dk. Slaa,
halikuwatafuta viongozi hao, lakini likamtafuta Zitto Kabwe.
Wanaandika hivi;
“Nikiangalia tukio langu na mgogoro uliopo ndani ya
chama najua nimeumizwa kwa ajili ya kumtetea Zitto, kwa sababu nimekuwa
nikipokea vitisho kutoka kwa viongozi wa juu wa chama na M4C,” alisema.
Kukamilisha mpango huo wa spinning ya kuwahusisha
viongozi wa CHADEMA na hatimaye chama kizima katika sakata hilo, Zitto
akatafutwa na akasema hivi;
Akizungumzia tukio hilo, Zitto amesema vurugu kamwe
siyo suluhu ya siasa nchini na kwamba ni kitendo kinacholenga
kuwaingiza watu katika woga na kuwatisha.
“Haya ni matendo ya kikatili na ya kumuogopesha
kutokana na kupinga baadhi ya mapendekezo ya upande wa baadhi ya viongozi
Kamati Kuu ya chama.
“Natoa changamoto kwa viongozi zote wa Chadema
kwamba sasa wakanushe kuwa vurugu siyo silaha yao katika siasa,” alihitimisha
Zitto.
Huyu mtu tayari alishajua na kuhitimisha kuwa
viongozi na chama chake kinahusika na tukio hilo? Kwa nini anawahi kuhitimisha
kuwasukumia tukio zito kama hilo ambalo linaweza kuharibu kabisa chama chake
ambacho eti anataka kuwa mbunge na kiongozi wake. Au ni mwendelezo wa mkakati
ule ule, wakakutanishwa kwenye kipindi cha Star tv asubuhi yeye na Mwigulu,
Mwigulu Nchemba akajifanya anatoa habari ya ugaidi wa CHADEMA?
Habari za kiuchambuzi juu ya mkakati huu wa kutaka
kurudisha taswira ya ugaidi na kuihusisha CHADEMA na matukio ya vurugu
yanayohusisha umwagaji wa damu ikipangwa kwa ustadi na wale wale, kwa mtindo
ule ule, kwa malengo yale yale, zitaongezwa baadae katika andiko hili;
No comments:
Post a Comment