“Katika ukuaji wa kasi unaoendelea jiji
la Dar es Salaam maeneo yaliyopo katika wilaya hasa ya Kinondoni na Temeke
ndiyo ambayo yanaongoza pia katika ukuaji huo wa kasi wa kimakazi na shughuli
za kiuchumi kama viwanda na uwekezaji hivyo ni vyema zikaongezwa Manispaa za
Ubungo na Kigamboni ili kuongeza ufanisi wa ukuaji wa jiji,” alisema Mnyika.
Aidha
alipendekeza hitaji la kuwapo kwa jiji la Dar es Salaam kama chombo kikuu juu
ya Manispaa zote tano zinazopendekezwa zitakazokuwapo na kwamba Meya wa jiji
hili achaguliwe na wananchi kwani itatoa fursa katika utendaji na uwajibikaji
imara ambao unaweza kupimwa na wananchi.
Source: Geofrey M. (Jan. 2014). Mnyika apendekeza Ubungo iwe Manispaa. Retrieved from Ippmedia/Nipashe
No comments:
Post a Comment