Siku
ya Nne ya ziara ya CHADEMA Kanda ya Magharibi imetupeleka Wilaya ya Sikonge
Mkoa wa Tabora.
Nikiwa (Zitto Kabwe) na Wenyeviti wa chama wa mikoa ya Kigoma, Katavi na
Tabora pia Mwenyekiti wa Kanda ya Magharibi Ndg. Mambo tumefanya mikutano 4.
Kero
ya Wakulima wa Tumbaku
Kero ya wakulima wa Tumbaku bado ni kubwa sana na
tumekuwa tunaelezwa kila tunapokwenda. Hapa Sikonge mwaka 2012/13 Chama Kikuu
cha Ushirika kimewakata wananchi fedha za mbolea ambayo wananchi hawakupata.
Wananchi wanakaa msimu mpaka msimu kupata fedha za mauzo ya Tumbaku. Makato ni
mengi na kufanya mkulima ashindwe kuvunja mzunguko wa umasikini.
Nimetoa
mawazo ya kisera kwamba imefikia wakati wakulima kupitia vyama vya msingi
wajiunge na mifuko ya hifadhi ya jamii ili kuweza kwanza kuweka akiba, pili
kupata mikopo nafuu kupitia vyama vyao vya kuweka na kukopa na hivyo kuweza
kuwalipa wakulima pindi wauzapo tumbaku.
Nimetoa wito kwa SSRA waangalie
uwezekano wa kuanzisha scheme maalumu ya hifadhi ya jamii kwa wakulima ambapo
Serikali ishiriki kwa kuchangia kiwango maalumu katika kila michango ya
wakulima. Hii itawezesha wakulima kupata mafao kama bima ya afya, bima ya
mazao, mikopo midogo midogo, tofauti za bei na hata elimu kwa watoto
wategemezi.
Hili
ni wazo jipya lakini linapaswa kutazamwa ni kuinua wakulima wa Tanzania.
Tusiendelee kuwasahau wakulima. Watanzania wapo Vijijini, tusiwasahau.
Umasikini wa Tanzania unaonekana vijijini (rural phenomenon), tutokomeze
umasikini kwa kuwekeza kwa mkulima.
No comments:
Post a Comment