![]() |
Dr. Slaa akiangalia kwa umakini Apollo 16 capsule kwa umakini. Hii ni Capsule iliyorudi kutoka mwezini miaka ya 70 |
Dr.
Slaa amesema kwamba, hadi kufika marekani, wanasayansi wa kimarekani walifika
mwezini baada ya kupata changamoto kutoka kwa Rais keneddy aliyewamba
wanasayansi hao kufikisha mtu mwezini chini ya miaka 10. Wanasayansi hao
walimjibu na kufika mwezini chini ya miaka 8. Hii ilitokana na serikali ya
marekani kuipa kipaumbele elimu
Dr.
Slaa aliendelea kusema kwamba baada ya uhuru, Mwalimu Nyerere aliipa kipaumbele
elimu kwa ujumla. Kwa mfano, Mwalimu Nyerere aliwachukua vijana watano
wanajeshi na kuwapeleka nchini Ireland kusomea mambo ya engineering. Waliporudi
walipelekwa kibaha ambako walibuni na kutengeneza gari ya kwanza iliyoitwa
Nyumbu ambayo ni ubunifu wao.
Baadae
mwalimu Nyerere aliwabunia hao wanajeshi mradi wa Dhaabu wa Buhemba ambao
ungewawezesha kulipia gharama za kutengeneza magari mengi. Bahati mbaya, baada
ya mwalimu kustaafu, mafisadi walijipenyeza na kuuchukua huo mradi. Huu ndio
ufisadi uliozaa meremeta. Mradi wa Nyumbu ukafa na kilichotokea ni ufisadi wa
billion 155 uliohusisha benki ya Nedeland Ya Afrika kusini. Hadi leo, hakuna
maelezo licha ya fedha hizo kutumika kwenye kampeni ya CCM ya 1995
CCM
imekuwa janga la mtanzania. CCM inaua ubunifu wa vijana wetu. Leo 90% ya
wanafunzi wanafeli mashuleni huku viongozi wa CCM wakiwahadaa wananchi kwamba
wanaleta maendeleo. Ni maendeleo gani wanazungumzia wakati watoto wetu hawajui
kusoma wala kuandika alihoji Dr. Slaa. Wanajeshi wetu waadilifu, wabunifu,
wazalendo na wanaojituma wamefikia kuishi maisha ya ajabu.
Ubunifu
wao kama mradi wa Nyumbu umeuwawa na CCM. CCM imefanya maisha yao kuwa magumu
naya kusikitisha. Wanajeshi waliostaafu wamebaki kama omba omba. Wale
wanashiriki kulinda amani nje ya nchi wanadhulumiwa hela zao pale wanarudi
Tanzania. Nchi ambayo haiwezi kuwahudhumia wanajeshi wake, ni nchi isiyofaa
kuwa katika ramani ya dunia. Dr. Slaa amewaomba wanajeshi wasilie, kwani
CHADEMA inatambua michango yao.
Kadhalika
amewaomba vijana watanzania wasikate tamaa. CHADEMA inasikia vilio vyao,
wanatambua kwamba ugumu wao wa maisha umesababishwa na CCM na siyo mwingine.
Wakati hao ma CCM wanajineemesha na hela zetu za kodi, wanajeshi na wananchi
kwa ujumla wanashindwa hata kujenga nyumba ya kujisitiri punde wanapostaafu.
CCM imeua ubunifu ndani ya Tanzania. Wameamua kuwaweka vijana wetu mazezeta ili
waendelee kuwatawala. Wenzetu
wanapeleka watu mwezini, lakini watanzania hata wembe tunanunua kutoka chini
kwa sababu ya CCM alisema Dr. Slaa na kuonya kwamba wakiendelea kuwanyima
wananchi haki zao za msingi, muda utafika watachoka
![]() |
Rover Ambayo imewahi kutumika mwezini |
![]() |
Dr. Slaa akipokea zawadi maalum ambayo rais wa marekani tu ndiye aliyewahi kupewa |
![]() |
Dr. Slaa anapata maelezo na historia ya safari za mwezini |
No comments:
Post a Comment