“Kila nchi mshirika (Zanzibar na Tanganyika), ibakie na uraia
wake na mtu kuwa na uraia wa nchi mshirika ndiko kumpe uhalali wa kuwa raia wa
shirikisho,” alisema. Pia kamati imependekeza Rais wa muungano ambaye atakuwa na
madaraka ya juu katika shirikisho lote kwa mambo yote ya Muungano, hivyo nchi
washirika zinapaswa kuwa na haki sawa katika kutoa watu wa kushikilia Baraza la
Mawaziri la Muungano, Bunge na Mahakama. Alisema rasimu inatakiwa itamke wazi kwamba urais wa Muungano
utashikwa kwa zamu na kwa kupokezana baina ya nchi washirika yaani Tanganyika
na Zanzibar na kwamba Rais atangazwe mshindi baada ya kupata kura zaidi ya
asilimia 50 kutoka Tanganyika na Zanzibar.
Mambo ya kuondolewa
Alisema uchumi si suala la Muungano hata katika Katiba ya
sasa na kwamba nyenzo za kuendeshea na kusimamia uchumi wa nchi kwa maana ya
sera za fedha na uchumi zimeendelea kudhibitiwa kupitia Serikali ya Muungano. “Vyombo vikuu vinavyosimamia sera hizo ambavyo ni Benki Kuu
ya Tanzania (BoT), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Wizara ya Fedha ya
Serikali ya Muungano vimekuwa vikifanya uamuzi na kuyatekeleza bila ya
kuzingatia kuwa Zanzibar inategemea uchumi wa utoaji huduma na haiwezi kuwa
sawa na uchumi wa Tanganyika ambao unategemea rasilimali,” alisema. Akizungumzia usajili wa vyama vya siasa alisema Rasimu ya
Katiba haipaswi kujumuisha suala la vyama vya siasa katika mambo ya Muungano na
kwamba Zanzibar na Tanganyika zinatakiwa kuandikisha vyama vyake vya siasa. Alisema badala ya kuendeleza mfumo uliopo sasa wa Makamu wa
Rais kupatikana kutokana na mgombea mwenza, marais wa nchi washirika (Zanzibar
na Tanganyika) moja kwa moja wawe makamu wa kwanza na makamu wa pili wa Rais wa
Muungano.
Source: Wamtambwe (Sept. 2013).Wazanzibari wataka Zanzibar ijitegemee karibu kwa kila kitu. Zanzibar. Retrieved from Mzalendonet
No comments:
Post a Comment