Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Tuesday, September 3, 2013

UVCCM Imemtukana Maalim Seif Matusi ya Nguoni


  

       Nilifikiri mada hii anaweza kuiandika mtu kama mwanachama wetu ‘kada wa ccm au xalasinga’ na wengioe kama hao. Naona wamekaa kimya. Juzi katika mkutano wa UVCCM pale Kombawapya, viongozi wa UVCCM walimtukana Maalim Seif (VP-1) matusi ya nguoni, yaani matusi yao siwezi kuyasema katika hadhara hii. Pia alitukanwa mwakilishi wa mji mkongwe, Jussa ladhu, na Mansour Yussuf Himid. Pia matusi yaliyosemwa siwezi kuyataja hadharani. Maswali: hivi akina Ali Mohammed Shein (rais wetu) hayajui haya, hayaoni haya, hayasikii haya. Hivi kweli akina Kinana, Kikwete, Seif Ali Iddi – na kama hao, hawayaoni haya, hawayasikii haya, tuseme inakuaje?
       Tukumbuke kuwa huyu ni makamo wa Rais wa Zanzibar. Na kama rais (mkuu wa nchi !, sic: ya Zanzibar) anatukanwa assistant wake na anakaa kimya, ina-maana kuwa ameridhia kutukanwa kwake huko. Sisi Zanzibar ni sehemu ya commonwealth na katika British common law, tunaambiwa kuwa ‘silent means consent’. Tatizo kubw ala UVCCM na CCM kwa ujumla, wameishiwa na sera kamili ya kuiongoza TZ na ZNZ, hawana plan, hawana roadmap or strategy – kilichobaki ni hii kutoa matusi tu. Kwa mfano, CCM hawana, tuseme ‘way out’ ya kujitetea kuhusu katika mpya na mustakabali wa nchi. Wanataka serikali mbili, CCM mwenzao, Joseph Wrioba ameshawaambia kuwa kinachojadiliwa ni ile rasimu, na hilo halimo – wajadili ‘tatu’, na sio mbili au moja au ‘nkataba’ n.k. Kwa hivyo, kilichobaki ni hilo la kuwa hivi vile; na huyu anafanywa hivi na vile.
   Ninahikijua mimi CCM na chama chochote cha kisiasa kinatakiwa kufika pahala na kusema NO kwa wale ambao wanahisi kuwa wanawaharibia kazi, au turufu zao za kisiasa; ANC cha Afrika Kusini, ilimtoa nje Mwenyekiti wa vijana, Julius Malema, baada ya kuonekana analtea upuuzi wake wa siasa za kikaburu huku akijineemesha na kuiba mpaka amekuwa bilionea, alikuwa anatumia siasa na umaoja wa vijana kwa kula yeye mwenyewe; kama wanavyofanya hawa UVCCM, ni maslahi tu huku wakiifanya nchi kusota na kudumaa kifikra. Chengine ninachoona kinakosekana ni kuwa TZ haina uongozi kabisa kuanzia “top-down”.
       Tumefika pahala tunaambiw akuwa wabunge takriban wote wanauza unga/dawa za kulevya; tumefika pahala judiciary system imekufa kabisa, na rushwa ndio sheria yenyewe, n.k na yanatumika haya — ama ‘amani na utulivu’ au ‘muungano’ kuhalalisha uovu na ukandamizaji –leo kama watunga sharia ndio wauza cocaine, yule anayettungiwa sharia atakuwa nani??? mawaziri wengi na watendaji wakuu wana vyeti fake; iko wapi moral argument ya ‘ethical leadership’ hapo?? Kuna mengi siyamalizi.

Source: Abdisalm (Sept 2013).UVCCM Imemtukana Maalim Seif Matusi ya Nguoni. Retrieved from Mzalendonet

No comments: