Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Wednesday, August 28, 2013

MANSOUR AMSHUKURU MUNGU KWA KUFUKUZWA CCM


        Aliyekuwa mwakilishi wa jimbo la kiembesamaki ndugu mansour yussuf himid ccm kwa tiketi ya ccm amesema anamshukuru m/mungu kutokana nakufukuzwa kuwa mwanachama wa CCM. akizungumza na idhaa yakiswahili ya sauti ya ujerumani amesema bado ni mapema kuzungumza lolote kuhusu kufukuzwa kwake kuwa mwanachama wa CCM. Amesema ataendelea kutoa maoni yake kupitia mchakato wa katiba unaondelea hapa nchini kama alivyotoa huko nyuma. Hata hivyo ndugu mansour amefafanua kuwa haiwezekani kuwa na katiba iwapo hakuna uhuru wakujieleza.

        Aidha kiongozi huyo wa zamani wa jimbo la kiembesamaki ameshauri kuzingatiwa maamuzi ya wengi katika kupatikana katiba mpya ya jamhuri ya muungano wa Tanzania. Wakati huo huo jumuiya ya umoja wa vijana waccm wilaya ya dimani kichama jimbo lakiembesamaki imesema kuwa inaunga mkono uamuzi wakumvua uanachama uliotolewa huko dodoma na halmashauri kuu ya taifa ya CCM kwa aliyekuwa mwakilishi wao ndugu mansour yussuf himidi.

            Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya khabari na jumuiya hiyo nakusainiwa na katibu wake ndugu yussu ramadhani imesema kuwa wanachama wake wamefarijika kutokana na chama chao kumchukulia hatua zakinidhamu ili kukabiliana na vurugu zilizokuwa zikifanywa na mwakilishi huyo kwa kutumia ukumbi wa baraza la wawakilishi Zanzibar kukishambulia,kukipaka matope na kuigawa ccm mbele ya wananchi. Aidha jumuiya hiyo imeshauri kuwa uamuzi huo usimalizie kwa mansour pekee bali kwa mwakilishi,mbunge na kiongozi yoyote anayekwenda kinyume na sera za CCM.

Source: Harith (August 2013).Mansour amshukuru mungu kwa kufukuzwa CCM. Retrieved from Mzalendo net



No comments: