Maelefu ya wananchi wa mji wa Kahama na
vitongoji vyake, wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa Mabaraza ya Wazi ya
kujadili rasimu ya katiba mpya, wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),
ambao ulihutubiwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe na Mbunge wa
Ubungo, John Mnyika, uliofanyika mjini Kahama jana (kwa ajili ya kuripoti ni
juzi)
Mbowe kuwasili Shy 1 na 2;
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, alipowasili mjini Shinyanga, akiongozana na
Mbunge wa Ubungo, John Mnyika, ambako walifanya mkutano wa Mabaraza ya Wazi ya
kujadili rasimu ya katiba mpya juzi.
Mnyika kuhutubia Kahama;
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ambaye pia ni Mbunge wa Ubungo, John
Mnyika, akiwahutubia wananchi wa mji wa Kahama, katika mkutano wa Mabara ya
Wazi ya kujadili rasimu ya katiba mpya juzi.
Kada wa CCM;
Aliyekuwa Kada wa Chama Cha Mapinduzi
wilayani Kahama, Malimi Ng'wanabulanhwa, akipkea kadi ya uanachama wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kutoka kwa Mwenyekiti wa chama hicho,
Freeman Mbowe, mara baada ya mkutano wa hadhara wa mabaraza ya wazi ya kujadili
rasimu ya katiba mpya, ulioanyika mjini Kahama juzi.
Mbowe, Mnyika helkopta;
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na Mkurugenzi wa Habari na Uenezi, John
Mnyika, wakiwasili katika moja ya mikutano yao ya Mabaraza ya Wazi ya kujadili
rasimu ya katiba mpya juzi.
Mbowe kuhutubia Malya;
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Malya,
wilayani Kwimba, Mwanza, katika mkutano wa hadhara wa Mabaraza ya Wazi ya
kujadili rasimu ya katiba mpya juzi.
Mbowe, Mnyika kuwasili Bariadi;
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa chama
hicho, John Mnyika, wakilakiwa na wananchi wa mji wa Bariadi mkoani Simiyu,
walipowasili kufanya mkutano wa Mabaraza ya Wazi ya kujadili rasimu ya katiba
mpya juzi.
Makamanda wa CHADEMA wakiwapokea Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe na Mkurugenzi wa Habari na Uenezi, John Mnyika kwenye mkutano wa hazara baraza la katiba Kahama.
No comments:
Post a Comment