Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Wednesday, August 21, 2013

‘Katiba ni moyo wa taifa’


      MWENYEKITI wa kikundi cha Tume ya Mabadiliko ya Katiba kinachoendesha mabaraza ya mikoa ya Arusha na Manyara, Yahya Msulwa, amesema kuwa Katiba ni moyo wa taifa, hivyo amewataka wajumbe wa mabaraza ya Katiba kuwa makini wanapotoa maoni yao. Alisema wajumbe wa mabaraza hayo wanapaswa  kuhakikisha kuwa wanaacha tofauti zao za kiitikadi, kwani jambo wanaloliandaa si la vikundi bali ni la taifa zima la sasa na vizazi vijavyo. Msulwa alisema hayo alipokuwa akifungua mkutano wa Baraza la Katiba la Halmashauri ya Arusha Mjini kabla ya kuwakaribisha wajumbe wa mabaraza ya Katiba wa ngazi ya  kata ili waweze kujadili rasimu na kutoa maoni kwa lengo la kuboresha ili kupata rasimu ya pili.

      “Nawasihi ndugu wajumbe tuache tofauti zetu za kiitikadi, badala yake tuangalie kitu gani kinafaa kwa ajili ya taifa letu na vizazi vijavyo kwa sababu Katiba hii itakayopitishwa itatumiwa hata na wale ambao bado hawajazaliwa,”  alisema Msulwa. Mojawapo ya upungufu ulioonekana katika rasimu ya sasa ni pamoja na kutokuwapo kwa ibara inayozungumzia utamaduni wa taifa, hasa katika sehemu ya kwanza inayoelezea mipaka, alama, lugha, utamaduni na tunu za taifa, jambo ambalo ni hatari kwa utamaduni wa taifa, ambao unaweza kutoweka endapo utakosa ulinzi wa Katiba. Akitoa mapendekezo hayo, Alute Mugwai, ambaye ni mjumbe wa Baraza la Katiba Kata ya Themi na Mwanasheria maarufu jijini hapa, amesema kuwa ni muhimu Katiba ikaenzi kutunza tamaduni bora zilizopo.

        “Tamaduni nzuri ni vema zikawepo kwa maana ni utambulisho wa taifa. Mfano vazi la taifa, mambo ya jando, ndoa, chakula na mambo mengine yanayohusu utamaduni wa Kitanzania,” alisema Mugwai. Vilevile suala la serikali tatu, mbili ama moja limeendelea kuwa kitendawili kizito miongoni mwa wajumbe wa mabaraza ya Katiba na kufanya baadhi ya maoni na mapendekezo kutojadiliwa kwa misingi ya kuwa hayapo kwenye muungano na kutolea mfano wa suala la ardhi. “Napendekeza kuwa umiliki wa ardhi uwe chini ya Mtanzania na si chini ya mtu mmoja kwani tumeshuhudia wafugaji, wakulima na hata wananchi wa kawaida wakiteseka, ardhi ikiendelea kuwa chini ya rais na ikatokea akawa si mwaminifu, tutageuka watumwa ndani ya nchi yetu,” alisema Henry Lembali kutoka Kata ya Engutoto.

Source: Shayo F. ( August  2013).‘Katiba ni moyo wa taifa. retrieved from Tanzania Daima

No comments: