Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Thursday, August 22, 2013

Mnyika atoa mshahara wake kuchangia elimu Kinondoni


     Mbunge wa Jimbo la Ubungo John Mnyika, na Mwasisi wa Taasisi ya Ubungo Development  Initiative (UDI),  wamezindua kampeni maalum ya kuchangisha fedha na vifaa kwaajili maabara na maktaba kwa shule zote za sekondari zilizopo Manipaa ya Kinondoni. Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi huo, Mnyika  wameanzisha kampeni hiyo baada ya kundua kuwa  wanafunzi wengi wamekuwa wakifeli kutokana na ukosefu wa maabara na maktaba.  “Takwimu za mwaka 2011 mwishoni, zinaonyesha kuwa kati ya shule 139 za Wilaya ya Kindondoni ni shule 23 pekee zenye maabara na maktaba ndiyo maana tumeona ni vyema tukaanza kukomboa elimu na kuongeza idadi ya ufaulu wa wanafunzi katika wilaya yetu kwa kuchangishana sisi wenyewe,” alisema Mnyika.

     Alisema, wakati serikali ikijipanga katika kuweka vifaa hivyo katika shule, ni vyema kila mpenda maendeleo ambaye anaguswa na hali ya elimu akachangia katika kampeni iliyoanza jana rasmi ili kufanikisha lengo la kuwapatia wanafunzi zana muhimu katika masomo yao. “Kwa upande wangu nitajitolea asilimia 20 ya mshahara wangu kila mwezi ili kuwezesha kampeni hii ambayo itasaidia kununua vifaa vya maabara na vitabu kwaajili ya maktaba, wananchi pia wanatakiwa kujitolea vifaa vya maabara na maktaba kama wanavyo na si lazima kuchangia pesa,” alisema Mnyika. Alifafanua kuwa pia maabara na maktaba hiyo itatengenezwa katika mfumo wa kuhamishika ili kusaidia kuzifikia shule nyingi ambazo hazina huduma hizo. “Kampeni itaambatana na ununuzi wa gari aina ya Lori  ambalo litatumika kubebea vifaa hivyo, ambalo litagharimu Sh. milion 330, hivyo litasaidia kufika katika kila shule na wanafunzi kutumia ,” alisema.

Source: Ippmedia (August 2013).Mnyika atoa mshahara wake kuchangia elimu Kinondoni. Retrived from Ippmedia/Nipashe

No comments: