MASTAA wawili wanaotamba katika filamu za Kibongo, Kajala Masanja na Wema
Isaac Sepetu hivi karibuni walifunga safari hadi Gereza la Ukonga jijini Dar
kwa ajili ya kumuona Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ anayetumikia kifungo cha
maisha gerezani humo.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, mara baada ya mastaa hao kufika na kuonana na
Papii Kocha ambaye anatumikia kifungo cha maisha sambamba na baba yake Nguza
Viking ‘Babu Seya’ inadaiwa kuwa Papii aliangua kilio cha nguvu.
“Nimewaona Kajala na Wema Gerezani Ukonga,wameenda
kumuona Papii Kocha. Sasa nimeamini kuwa Kajala amejifunza mengi kutokana na
kuwekwa mahabusu kipindi kile,” kilisema chanzo chetu kwa sharti la kutotajwa
jina lake gazetini.
Baada ya kupata taarifa hizo Risasi Mchanganyiko liliwatafuta mastaa hao
ili kutaka kujua undani wa safari yao hiyo. Gazeti hili liliwapigia simu na kuzungumza na Kajala baada ya namba ya
Wema kutokuwa hewani. “Kweli mimi na Wema tulienda gerezani kumuona Papii ilikuwa ni safari ya
majonzi sana, Papii aliangua kilio sana alipotuona,” alisema kwa kifupi Kajala
na kukataa kusema kilichojiri zaidi.
GPL
No comments:
Post a Comment