Jimbo la Ukonga ni kati ya majimbo
ambayo CCM ina hali ngumu sana na hii ni kutokana na maendeleo duni katika
jimbo hilo. Mbunge wa Jimbo hilo Eugene Mwaiposa ni kati ya wabunge ambao
hawaongei chochote cha kupigania Jimbo lake. Ni mbunge ambaye ameshindwa
kufanya mkutano wowote wa hadhara Jimboni kwake kwa aibu ya kuzomewa na
kushindwa kujibu kero za wananchi.
Jimbo la Ukonga barabara zake
asilimia 90% ni mbovu na hazipitiki kabisa kipindi cha mvua.Kutokana na ubovu
wa barabara hizo kipindi cha mvua wananchi wanatozwa mpaka shilingi 1000/-
kutoka kituo kimoja hadi kingine. Hali hiyo imekuwa ni kicheko na mbeleko kubwa
kwa chama cha CHADEMA. Kwa sasa CHADEMA ndio inashikilia siasa za Ukonga na
wamekuwa wakifanya mikutano mfululizo kwenye matawi na Kata. Kunawiri kwa
CHADEMA Jimboni Ukonga kunachangiwa pia na viongozi wa chama hicho ngazi ya
Jimbo kushirikiana kwa pamoja kuimarisha chama kwa kufanya kazi bila kuchoka.
CHADEMA wamekuwa wakiwaeleza wazi
wananchi kwamba mateso yao yanatokana na kuichagua CCM kwenye uchaguzi
uliopita. CHADEMA imekuwa ikiwapa mfano wa majimbo ya Ubungo na Kawe
yanayoshikiliwa na CHADEMA jinsi wabunge wake wanavyopiga kelele na jinsi
kulivyo na maendeleo makubwa katika majimbo yao. Ni ukweli ulio wazi kwa hali
ya CCM jimboni Ukonga ni ya kusikitisha sana.Matawi mengi yanafungwa na
kugeuzwa kuwa ngome za CHADEMA.
Na endapo hali ikiendelea hivi hivi
ni wazi CHADEMA itapata ushindi mkubwa kwenye jimbo hili uchaguzi ujao na idadi
kubwa ya madiwani. Wanachpaswa CHADEMA tu ni kuteua wanachama wanaokubalika
kugombea nafasi za Ubunge na Udiwani.
Hii ni Tathmini yangu
binafsi baada ya kuzunguka kata zote za Ukonga kwa ziara binafsi kwa kipindi
cha wiki mbili.
No comments:
Post a Comment