Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Friday, August 30, 2013

CHADEMA wahitimisha mabaraza ya rasimu


  KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, leo anahitimisha siku 15 za ziara ya chama hicho ya kukusanya maoni ya rasimu ya Katiba mpya iliyofanyika nchi nzima, ukiachilia mbali mikoa ya Lindi na Mtwara ambako Jeshi la Polisi lilizuia mikutano hiyo. Taarifa ya ofisa habari wa chama hicho, Tumaini Makene, ilisema kuwa timu ya katibu mkuu leo itahitimisha mabaraza hayo ya wazi katika wilaya ya Temeke, jijini Dar es Salaam. Tangu Agosti 12, mwaka huu, CHADEMA kupitia timu zake mbili za viongozi, wakiongozwa na mwenyekiti na katibu ilianza ziara ya kukusanya maoni ya rasimu ya Katiba mpya kupitia mabaraza ya wazi.

     Timu ya kwanza iliyoongozwa na Mbowe ilipita katika mikoa ya Mara, Simiyu, Mwanza, Geita, Kagera, Kigoma, Shinyanga, Tabora, Katavi, Rukwa, Mbeya, Njombe na kuhitimisha Iringa juzi. Dk. Slaa na timu yake wao walichanja mbunga katika mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Dodoma, Singida, Morogoro, Pwani na Dar es Salaam na kisha timu hizo mbili zitaungana kuelekea visiwani Zanzibar. Katika mikutano yao, wananchi mbalimbali waliweza kutoa maoni yao kwa kuzungumza na kujaza fomu maalumu juu ya mambo wanayotaka yazingatiwe kwenye Katiba mpya.

Source: Tanzania Daima ( August 2013).CHADEMA wahitimisha mabaraza ya rasimu. Retrieved from Tanzania Daima

No comments: