Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Friday, August 30, 2013

CCM Dar lawamani


     CHAMA cha Mapinduzi (CCM), mkoa wa Dar es Salaam, kimedaiwa kuuza eneo la mtu ambalo lina shule ya sekondari kwa kampuni ya Simba Oil Com kwa thamani ya sh milioni 500. Akizungumza na Tanzania Daima jijini mwishoni mwa wiki, mkurugenzi wa shule hiyo ya sekondari ya Metropolis, Richard Leon, alisema shule hiyo iko eneo la Mbagala Rangi Tatu, wilaya ya Temeke. Alisema uamuzi wa kuuzwa shule hiyo haukufuata taratibu za kisheria, kutokana na CCM kuuza kinyemela bila ya kutoa taarifa mapema kwa mmiliki wa shule hiyo. “Eneo nilipojenga jengo la shule nililipata mwaka 1997 kwa makubaliano ya hiyari na Tawi la CCM Mbagala Rangi Tatu ya kujenga madarasa katika eneo lao na nilikuwa nalipa kodi ya kiwanja na michango mingine ya maendeleo kwenye tawi la chama hicho.

       “Kwa mshangao Mei mwaka 2010, tawi hilo la CCM lilitakiwa kuhama pamoja na shule kwa madai mmiliki halali alikuwa Farid Nahdi, ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya Simba Oil Com. Alisema CCM iliwaarifu kuwa mmiliki huyo ana jukumu la kuilipa shule fidia, wao tayari walikuwa wameshalipwa sh milioni 40 na kujengewa jengo jingine lenye thamani ya sh milioni 10 na kampuni hiyo. Aliyewahi kuwa Katibu wa Tawi hilo Shabani Kifurango ambaye ndiye aliyesaini mkataba wa makubaliano na shule hiyo, alisema shule hiyo inapaswa kulipwa, wanaopinga ni wale walionufaika na uuzwaji huo ambao haukufuata taratibu. Nahd, alisema anamiliki eneo hilo kihalali baada ya kuuziwa na wamiliki kwa kufuata taratibu zote za sheria ya ardhi.

Source: Semtawa S. (August 2013). CCM Dar lawamani. Retrieved from Tanzania Daima

No comments: