Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Friday, August 30, 2013

Mjadala rasimu ya Katiba waibua mapya




 RASIMU ya Katiba mpya ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania imezua mambo mapya kwenye vikao vya Baraza la Katiba katika kijiji cha Iyogwe na Chakware katika wilaya ya Gairo, mkoani Morogoro. Mambo hayo yameibuka baada ya baadhi ya wananchi kushangaa kama Tanzania ilikuwa na Katiba hapo awali. Mbali na kushangazwa huko kulikoibua mshangao kwa wawezeshaji wa asasi isiyo ya kiserikali ya Conasu, wakishirikiana na Foundation For Civil Society FCS, wanachi hao pia walisema rasimu hiyo ina maneno mengi ya kisheria na kitaalamu, hali waliyodai imelenga kuwagawa.

               George Mbwego (68) wa Iyogwe na Marium Donard (53) wa Kinyolisi kwa nyakati tofauti walihoji kazi na umuhimu wa Katiba pia walipendekeza maneno yaliyoandikwa kitaalamu na kisheria zaidi likiwemo Akidi, Kudurusu, Marupurupu, weledi na mengineyo kuondolewa na kuandikwa kwa lugha rahisi ili kila mmoja aweze kuisoma na kuielewa. “Ndugu zangu, niseme ukweli tangu nizaliwe hadi kufikia umri huu nilikuwa nadhani Tanzania ilikuwa inaendeshwa kiholela tu, sikujua kama kuna Katiba,” alisema Mwengo na kuungwa mkono na Mariam. Awali Mkurugenzi na Mratibu wa Conasu, Anjelus Runji, aliwashauri kuipitia rasimu kwa makini na kurekebisha na kuongeza vipengele ambavyo vitawezesha kufanya mabadiliko yenye tija kwa jamii pasipo kujali nafasi, umri, jinsia, rangi na kabila la mtu.

Soucre: Malembeka J. ( August 2013). Mjadala rasimu ya Katiba waibua mapya. Gairo. Retrieved from Tanzania Daima

No comments: