Waziri wa Mashauri ya
Kigeni wa Rwanda amesema kamwe hawatawafukuza Watanzania wanaoingia na kutoka
nchini Rwanda kwa shughuli mbalimbali kwani tupo ndani ya shirikisho la Afrika
Mashariki na hata kihistoria Rwanda haijawahi kuwa na tatizo na Tanzania. Akizungumzia
sakata la wahamiaji haramu wa Kinyarwanda kufukuzwa na serikali ya Tanzania
amesema, kila nchi inayo mamlaka ya kufanya vile inafaa lakini ingekuwa vizuri
Tanzania ingewasiliana na Rwanda ili kujua wataondokaje na kupokelewa vipi.
Amesisitiza, "Kwa kuwa
wenzetu wameamua kufanya hivyo, tupo tayari kuwapokea wananchi wetu"
Lakini pia, Waziri huyo amesema waasi wa FDRL ni kikundi cha wauaji
wanaojipanga kuangamiza watu fulani nchini Rwanda hivyo wanatakiwa kupingwa kwa
nguvu zote badala ya kuwatambua na kuzungumza nao kama kundi halali na lenye
nia njema.Naye Mtanzania Mohammed, amependekeza Rais Kagame na Kikwete wakutane
na kufikia suluhu.Pia baadhi ya Wanyarwanda wamelalamikia kutokutendewa haki
kwa kutenganishwa na wake,waume, n.k.
Source: Makala Jr. ( August 2013).Serikali ya Rwanda imeapa kutowafukuza Watanzania! Retrieved from Jamii Forums/(DW Kiswahili.)
No comments:
Post a Comment