Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Wednesday, July 31, 2013

Wingu zito watuhumiwa wa ugaidi CHADEMA


  DANADANA ya uamuzi dhidi ya kesi ya ugaidi inayowakabili viongozi na wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) uliokuwa utolewe jana, imeendelea baada ya kusogezwa hadi Agosti 5 mwaka huu. Uamuzi huo umetolewa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, Simon Lukelelwa kufuatia kuchelewa kufika mahakamani hapo kwa washitakiwa wa kesi hiyo waliohifadhiwa gereza la Uyui mjini hapa. Wakati uamuzi huo unatolewa na Jaji Lukelelwa washitakiwa wote watano wa kesi hiyo; Henry John  Kileo, Evodius Justian, Oscar Kaijage, Seif Kabuta na Rajab Kihawa hawakuwa katika chumba cha mahakama majira ya saa tatu na nusu asubuhi. Hii ni mara ya kwanza kuonekana mkoani hapa kwa kesi nzito kama hii kwa washitakiwa kucheleweshwa kufikishwa mahakamani kukabili mashitaka yanayowakabili.

      Washitakiwa walifikishwa mahakamani hapo majira ya saa nne na dakika arobaini na kujulishwa na wakili mwakilishi, Emmanuel Msyani kuwa shauri limepangiwa siku nyingine. Kesi hiyo ya jinai ilifunguliwa na wakili wa utetezi Peter Kibatala na kuanza kusikilizwa Julai 22, mwaka huu mbele ya Jaji Lukelelwa akiomba miongozo ya kisheria ikiwemo uamuzi uliotolewa na mahakama za wilaya na mikoa. Shauri la maombi ya marejeo liliwakilishwa na wakili Kibatala anayewatetea washitakiwa akiiomba Mahakama Kuu ipitie majalada ya kesi mbili dhidi ya wateja wake zilizofunguliwa mahakama hizo baada ya kuona uamuzi wake haukutenda haki. Wakili Kibatala alibainisha katika maombi hayo kwamba uamuzi huo wa mahakama za chini umeathiri pia haki za waomba rufaa ikiwemo kuwanyima haki ya kupata dhamana. Kwa upande wake, serikali ilishindwa kujibu maombi hayo na badala yake ilijenga hoja kwamba walichelewa kupata nyaraka hizo kwani walizipokea siku moja kabla ya kutajwa shauri hilo hivyo walishindwa kuzijibu.

Source: Murugwa T. (July 2013).Wingu zito watuhumiwa wa ugaidi CHADEMA. Tabora. Retrieved from Tanzania Daima

No comments: