Dr. Wilbroad Slaa, amealikwa kwa mahojiano na WPFW Radio ya Washington, D.C. U.S.A. siku ya jumatano tarehe 13 Machi, 2013. Saa saba mchana, saa za Amerika ya mashariki ( 1pm U.S Eastern time)/ Saa mbili usiku saa za Afrika mashariki (8pm East Africa time). Kumefanyika jitihada za kuushirikisha ubalozi wa Tanzania nchini Marekani kushiriki mahojiano haya bila kuwa na mafanikio. Bado jitihada za kuushirikisha ubalozi zinafanyika.
Baadhi ya mambo yatakayo jadiliwa ni hali ya siasa Tanzania, hali ya kijamii, hali ya kiuchumi, amani na usalama wa Tanzania na mengineo.
No comments:
Post a Comment