Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Saturday, March 23, 2013

Mahakama: Madiwani CHADEMA wakamatwe


MAHAKAMA ya Hakimu mkazi mkoani Arusha imetoa hati ya kukamatwa waliokuwa madiwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Jimbo la Arusha Mjini kwa kushindwa kulipa fedha za gharama ya kesi iliyokuwa ikiwakabili. Kwa mujibu wa hati ya mahakama ya Februari 19, 2013 iliyotolewa na hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo, Charles Magesa, ilionesha kuwa madiwani hao; Charles Mpanda (Kaloleni) na John Bayo (Elerai) walitakiwa kila mmoja kuilipa CHADEMA sh milioni 3.1 ndani ya miezi miwili kama gharama za kesi. Wakili wa CHADEMA kwenye shauri hilo, Method Kimomogolo alisema kuwa wateja wake (CHADEMA) wameshawasilisha mahakamani hapo fedha kwa ajili ya kuwahudumia waliokuwa madiwani wakiwa gerezani. Madiwani waliotekeleza amri ya mahakama na kata zao kwenye mabano ni pamoja na Estomih Mallah aliyekuwa diwani wa Kimandolu, Rehema Mohamedi (viti maalumu) na Reuben Ngowi wa Themi. Novemba 22, 2012 Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha iliwaamuru madiwani watano waliotimuliwa CHADEMA kulipa gharama za kesi waliyokuwa wamefungua kupinga kufukuzwa uanachama, vinginevyo watapelekwa magereza.


Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Magesa alitoa hukumu hiyo baada ya CHADEMA kushinda kesi hiyo na kuwaamuru kulipa sh milioni 15 ndani ya miezi miwili, wakishindwa watapelekwa gerezani. Katika kesi hiyo ya madai, CHADEMA waliwakilishwa na wakili Kimomogoro, wakati wadaiwa walijitetea wenyewe baada ya aliyekuwa wakili wao kujitoa. Awali, kulikuwa na mvutano kati ya wadaiwa hao jambo lililosababisha kesi hiyo kusikilizwa kwa kipindi kirefu ambapo walitakiwa kueleza mahakama hiyo sababu ya kutokupelekwa gerezani, huku kila mmoja akitamka kiwango cha fedha ambacho angeweza kulipa kwa mwezi. Kwa upande wake, Ngowi alisema ana uwezo wa kulipa sh 25,000 kwa mwezi, Mpanda sh 20,000, Mallah sh 20,000, Rehema sh 15,000 na Bayo sh 15,000 kwa mwezi bila kuonesha mchanganuo wa kipato chao, jambo lililopingwa vikali na Kimomogoro kwamba ni kidogo.

Hakimu Magesa alisema kisheria mtu akishinda kesi ana uwezo wa kuchagua hukumu ya kulipwa kwa kuchukua mali za mdaiwa au mlalamikiwa kupelekwa kifungoni. “Kimsingi mtu anaposhinda kesi lazima alipwe gharama aliyotumia na iwapo mahakama itaridhia alipwe kwa kiwango hicho, itachukua muda mrefu kati ya miaka 10 na 16 kumaliza deni hilo, jambo litakalosababisha aliyeshinda kushindwa kuona matunda ya ushindi wake,” alisema Magesa. Alisema fedha hizo wanapaswa kuzilipa mara mbili,  awamu ya kwanza inatakiwa kila mmoja kulipa zaidi ya sh milioni 1.5 na  wawe wamemaliza kwa miezi miwili na kwamba, iwapo watashindwa mdai anaweza kupeleka mchanganuo wa gharama za kumtunza mfungwa na mahakama kuupitia na baadaye kutoa amri wapelekwe gerezani.

Source: Macha G. (March 2013). Mahakama: Madiwani CHADEMA wakamatwe. Retrieved from Tanzania daima

No comments: